VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Hapa Dar, Dr. Mwele Malecela alitoa taarifa juu ya ugonjwa wa zika kupitia Taasisi aliyokuwa akiiongoza ya NIMR. Kwanza, taarifa zake zikakanushwa kwa haraka. Akatumbuliwa. Akakubali matokeo na anasonga mbele.
Mkoani Singida, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida 'ameficha' taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu katika Wilaya yake ya Singida. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi akamsweka rumande kwa saa kadhaa.
Kwanini viongozi wetu hamsomeki? Au zika inaogopesha kuliko kipindupindu?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam