Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,565
15,920
Aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Bi.Mwele malecela ameposti katika akaunti yake ya twitter maneno haya. Nadhani huu ni mrejesho baada ya tamko la Mwenye nyumba kuwa Daktari Mwele malecela alikua anatumika na MABEBERU.


02872CDD-A21A-4640-9320-A40ACF9FD28E.jpeg

A5F625BA-F9B1-4C91-967C-2EBDEC49A9F5.jpeg

2A40F74F-62EC-423E-A805-3105D0560992.jpeg


=====

RAIS John Pombe Magufuli, amesema moja ya sababu kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya NIMR, Mwele Malecela, ni kiongozi huyo kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusiana na ugonjwa wa Zika.

Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Songwe, wakati alipofika kwenye ziara ya kikazi na kufanikiwa kuzindua kiwanda cha kahawa kilichojengwa na wajasiriamali wa Tanzania, ambapo amesema moja ya mambo ambayo yalipelekea kumtoa kwenye nafasi hiyo Malecelea ni kutangaza ugonjwa.

“Maneno huwa hayaishi, kuna wakati walitangaza kuna ugonjwa wa Zika nchini Tanzania, alipotangaza hivyo wakati mimi najua haupo nilimfukuza saa 7:30 usiku, wala hakuna cha Zika iliyotokea. Baada ya wiki moja wakamteua akawa bosi wao, hii ilionyesha alitumwa kusema aliyoyasema; hizi ni mbinu za kibeberu,” amesema Rais Magufuli.
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
 
Na nikweli, ukweli utabaki pale pale.
Cha ajabu, wazalendo ndo wanaopukutishwa awamu hii kuliko kutuzwa...
Yaani wazalendo ndo wanyamaze kisha tutumie nguvu kubwa kuwaaminisha watu mzalendo ni nani.
Kila siku naiombea Tz yangu, na stakaa chini kumwombea mtu anayeenda kanisani ila matendo yake anayajua moyoni kwake kwamba Mungu hapendi.
 
Back
Top Bottom