Mtikisiko CCM: Vigogo watano kutoa msimamo hivi karibuni

Mtikisiko CCM: Vigogo watano kutoa msimamo hivi karibuni

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,418
Reaction score
39,523
Vigogo watano wa Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kutoa msimamo wao juu ya ni nini watakifanya juu ya chama chao mwishoni mwa wiki ijayo.

Miongoni mwa vigogo hao yupo kigogo mmoja ambaye ataisambaratisha kabisa jumuiya moja maarufu ndani ya chama hicho.

Wadokezi wangu wameninyetisha kuwa kwa sasa ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa ambao haujawahi kukikumba chama hicho tangu kuanzishwa kwake ingawa mambo bado hayajaonekana hadharani.

Baadhi ya vigogo wanatarajiwa kutoa misimamo yao, wapo ambao wamekuwa ni watu wa karibu kabisa kwenye kampeni za mgombea urais wa Chama hicho John Magufuli katika siku za awali ingawa kwa sasa wamejiweka pembeni.

Wiki hiyo kutashuhudiwa kigogo mmoja wa kamati ya maadili ya chama hicho akitoka hadharani na kueleza waziwazi msimamo wake juu ya yaliyotokea ndani ya CCM na mwenendo wake kwa ujumla.

Habari nzito zinasema kuwa mgombea mwenza wa chama hicho bi Samia Suluhu amelalamikia kutengwa kabisa na wanawake wenzake huku wakibaki wawili ambao ni Angela Kairuki na Ummi Mwalimu wakijikongoja pamoja na wasanii mbalimbali.

Aidha hakuna kampeni za baadhi ya makundi kumsaidia mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho zaidi ya Abdulrahaman Kinana pekee huku vigogo wengine wengi wakijichimbia mafichoni jambo lililotafsiriwa kama hujuma dhidi ya mgombea huyo.
 
Umbea wa kwenye saluni za kike.....Mwanaume mzima rijali huwezi shabikia habari za kimbea mbea
 
Yaani TWAWEZA watajuta kupokea rushwa na kuudanganya umma.
 
Vigogo watano wa Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kutoa msimamo wao juu ya ni nini watakifanya juu ya chama chao mwishoni mwa wiki ijayo.

Miongoni mwa vigogo hao yupo kigogo mmoja ambaye ataisambaratisha kabisa jumuiya moja maarufu ndani ya chama hicho.

.

Unamaanisha Mama Sofia Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake?

:A S-confused1:
 
G Sam
Wewe ni mwana-UKAWA mwenzangu; ila katika ubashiri kama huu, sikuungi mkono. Mara kadhaa umekuja na kauli za namna hii, lakini hakuna kilichotokea.

Katika fani hii, gamba la mafisiem aitwaye lizabon ni wa kuaminika zaidi.
Ni wachache wanaoweza kuongea ukweli kama wako.!
 
Rais mtarajiwa amesha waambia akina G Sam kuwa KUOTA siyo tatizo na hasa kama ukiota USIKU ni hali ya kawaida..Lkn unapoota MCHANA huku ukiwa macho hujalala ni hatari..inaonyesha una TATIZO katika Ubongo wako..So msimshangae G Sam anathibitisha asemacho Rais anayesubili kuapishwa Dr.JPM
 
CCM wanadhani wao wako salama

Walichokosea wametumia silaha zao muhimu mapema sana

UKAWA watazitumia mwezi huu wa kumi.....

Kila wiki wataondoka vigogo.....Tabiri siku ya Tar 25 itakuwaje
 
Back
Top Bottom