Mtikisiko CCM: Vigogo watano kutoa msimamo hivi karibuni

Mtikisiko CCM: Vigogo watano kutoa msimamo hivi karibuni

Mmh..ndio yale ya mchana ccm usiku ukawa yanaanza kufumuka hadharani nini........yetu macho
 
G Sam
Wewe ni mwana-UKAWA mwenzangu; ila katika ubashiri kama huu, sikuungi mkono. Mara kadhaa umekuja na kauli za namna hii, lakini hakuna kilichotokea.

Katika fani hii, gamba la mafisiem aitwaye lizabon ni wa kuaminika zaidi.
Mwana-UKAWA Gani unasifia gamba? Wewe ni Gamba tu!!
 
Afazali kipasuke ccm police wanapiga sana RAIA NA umafya kwa watumishi wanao dai khaki Zhao kama Dr Ulimboka
 
Kwa habar hii kama ni kweli naanza iona nchi mpya yaja
 
Wewe jamaa, huchoki kuleta uwongo wako.

Juzi ulisema Makongoro Nyerere amekaa pembeni wakati huo huo Makongoro alikuwa katika Jimbo la Chalinze akipiga kampeni.

Hivi unapata faida gani kwa kueneza uwongo?

Kama unaamini kuna Mungu, lazima uelewe kuna malipo kabla na baada ya maisha ya hapa duniani.
 
CCM wanadhani wao wako salama

Walichokosea wametumia silaha zao muhimu mapema sana

UKAWA watazitumia mwezi huu wa kumi.....

Kila wiki wataondoka vigogo.....Tabiri siku ya Tar 25 itakuwaje
Mkuu uko sahihi, silaha zao kubwa walizotanguliza zilikuwa Lipumba, Slaa, Twaweza na REDET itakuwa ya mwisho kabisa.

Sasa wanategemea silaha ndogo ndogo kama yule mama wa NCCR na kuhonga viongozi ngazi za wilaya.
 
Vigogo watano wa Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kutoa msimamo wao juu ya ni nini watakifanya juu ya chama chao mwishoni mwa wiki ijayo.

Miongoni mwa vigogo hao yupo kigogo mmoja ambaye ataisambaratisha kabisa jumuiya moja maarufu ndani ya chama hicho.

Wadokezi wangu wameninyetisha kuwa kwa sasa ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa ambao haujawahi kukikumba chama hicho tangu kuanzishwa kwake ingawa mambo bado hayajaonekana hadharani.

Baadhi ya vigogo wanatarajiwa kutoa misimamo yao, wapo ambao wamekuwa ni watu wa karibu kabisa kwenye kampeni za mgombea urais wa Chama hicho John Magufuli katika siku za awali ingawa kwa sasa wamejiweka pembeni.

Wiki hiyo kutashuhudiwa kigogo mmoja wa kamati ya maadili ya chama hicho akitoka hadharani na kueleza waziwazi msimamo wake juu ya yaliyotokea ndani ya CCM na mwenendo wake kwa ujumla.

Habari nzito zinasema kuwa mgombea mwenza wa chama hicho bi Samia Suluhu amelalamikia kutengwa kabisa na wanawake wenzake huku wakibaki wawili ambao ni Angela Kairuki na Ummi Mwalimu wakijikongoja pamoja na wasanii mbalimbali.

Aidha hakuna kampeni za baadhi ya makundi kumsaidia mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho zaidi ya Abdulrahaman Kinana pekee huku vigogo wengine wengi wakijichimbia mafichoni jambo lililotafsiriwa kama hujuma dhidi ya mgombea huyo.


Hii habari yako ina mahusiano na hii mkuu?

Nimeambiwa kuwa ile ya kampeni ya CCM iliyoundwa kwa kumsaidia Dr. Magufuli na Mama Samia imesambaratika jana usiku baada ya kikao cha kimkakati. Nimearifiwa na mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kuwa kusambaratika kwa timu hiyo kunatokana na sababu mbalimbali. Wapo wajumbe waliosusa baada ya kuona wananchi hawaelewi somo la CCM na kuielewa Ilani. Wananchi wamekuwa hawaelewi wanachoambiwa na sasa wajumbe wanaishiwa cha kusema.

Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa wanatuhumiana, na hata na Dr. Magufuli mwenyewe, kuwa ni popo wa kisiasa. Wanaunga mkono harakati za wapinzani kwa kificho na kumharibia Dr. Magufuli majukwaani kwa kutamka maneno ya kukwaza na kukera yanayochochea hasira za wananchi dhidi ya wagombea wa CCM wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.

Wapo wajumbe waliosusa kutokana na kutotimiziwa matakwa yao hasa ya malipo kwa kila siku wanayoifanyia kazi. Wajumbe hao wamesema kuwa hawana muda wa kusubiri kulipwa baadaye kwakuwa uchaguzi ni bahati nasibu na lolote laweza kutokea. Wanasisitiza kulipwa marupurupu yao sasa kwa mujibu wa makubaliano ya kichama na kutoahidiwa kulipwa baada ya uchaguzi.

Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa hawapewi uzito na umaarufu kama ilivyotarajiwa. Wanamlaumu Dr. Magufuli na viongozi waandamizi chamani, kwa mfano, kumuamini sana Abdallah Bulembo ambaye hana hadhi kichama, kisera na kihela kupewa nafasi ya kutawala majukwaa kama afanyavyo sasa. Wanalalama kuwa watu maarufu wamewekwa kando na sasa wanaanza kuota utando.

Sasa timu imesambaratika. Dr. Magufuli yuko njiapanda kikampeni. Itambidi kupambana kiume ili kuendelea kujieleza mbele ya wananchi. Apambane kivyake sasa na watakaobaki naye!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mafisadi na majizi yote hata yakienda Chadema hayatapona lazima yashughulikiwe ipasavyo kokote yalipo
 
Ni habari nzuri. Mwishoni mwa wiki ijayo sio mbali ngoja tusubiri.
Nadani mwishoni mwa wiki hii tutakwa tumepata angalau majina ila wao wanasubiri kutangaza rasmi
Km kweli basi naomba nitumie wasaa huu kubashiri
Nchimbi
Kingunge
Mwandosya
Warioba
Kikwete
 
Wewe jamaa, huchoki kuleta uwongo wako.

Juzi ulisema Makongoro Nyerere amekaa pembeni wakati huo huo Makongoro alikuwa katika Jimbo la Chalinze akipiga kampeni.

Hivi unapata faida gani kwa kueneza uwongo?

Kama unaamini kuna Mungu, lazima uelewe kuna malipo kabla na baada ya maisha ya hapa duniani.
Lisemwalo lipo kama halipo linakuja.
 
Ni habari nzuri. Mwishoni mwa wiki ijayo sio mbali ngoja tusubiri.
Nadani mwishoni mwa wiki hii tutakwa tumepata angalau majina ila wao wanasubiri kutangaza rasmi
Km kweli basi naomba nitumie wasaa huu kubashiri
Nchimbi
Kingunge
Mwandosya
Warioba
Kikwete

Kikwere Noooooo.....Ni Mwiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom