Mwanamayu:
Ibara ya 41 (7) Inasema: Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.
(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate.
Kimantiki ibara hii inasema kuchunguza. Hakuna mahakama inayofanya uchuguzi. Kazi ya mahakama ni kutoa maamuzi ya kisheria baada ya kusikiliza hoja kutoka pande zinazopingana.
Je umeshawahi kusikia kuwa mahakama inamfanyia uchunguzi mtuhumiwa wa mauaji au mwizi? kusema ukweli hata lugha ya kiswahili inarudishwa nyuma kwa kufanya arbitration na Investigation kuwa kitu kimoja.