Mtikila: Slaa alishinda kwa 71%

Mtikila siku hizi naye kabadilika na kuwageukia mafisadi kama walivyo fanya wana-ccm wachache walio unga mkono Chadema na Slaa
 
Sasa hamjamsikia Dovutwa? hata sura yake siifahamu inafananaje naombeni mwenye picha ya Dovutwa aweke hapa
 
Mwanamayu:

Ibara ya 41 (7) Inasema: Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate.

Kimantiki ibara hii inasema kuchunguza. Hakuna mahakama inayofanya uchuguzi. Kazi ya mahakama ni kutoa maamuzi ya kisheria baada ya kusikiliza hoja kutoka pande zinazopingana.

Je umeshawahi kusikia kuwa mahakama inamfanyia uchunguzi mtuhumiwa wa mauaji au mwizi? kusema ukweli hata lugha ya kiswahili inarudishwa nyuma kwa kufanya arbitration na Investigation kuwa kitu kimoja.

Dah kweli apo mkubwa ndo nimefunguka
 
wow opportunist at wok, kazee kaudini kalikuwa kanasubiri mgombea yoyote akate chochote ili kampigie debe kakakosa maana kalishachuja kitambo! sasa kamekuja na mpya ya 71%, uliza mwenzako mzee wa kufuga majini ya kuangusha watu kanisani @#$kakobe@#@ akwambie alitumia mbinu gani akazipata za chadema.teh teh teh



Hakuna tafsiri nyingine zaidi ya Ujinga.
 
we mwanamayu wewe unaielewa katiba maana kama unaielewa ungeuona upungufu mkubwa wa katiba mbovu. au unataka kueleza nini? hebu rudia tena...
 
Mwanamayu:

Ibara ya 41 (7) Inasema: Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate.

Kimantiki ibara hii inasema kuchunguza. Hakuna mahakama inayofanya uchuguzi. Kazi ya mahakama ni kutoa maamuzi ya kisheria baada ya kusikiliza hoja kutoka pande zinazopingana.

Je umeshawahi kusikia kuwa mahakama inamfanyia uchunguzi mtuhumiwa wa mauaji au mwizi? kusema ukweli hata lugha ya kiswahili inarudishwa nyuma kwa kufanya arbitration na Investigation kuwa kitu kimoja.

- Simply Great Thinking, saafi sana mkuu!

William.
 
Gazeti la Mwannchi leo limeandika marekaebisho yaliyofanywa na NEC kwenye jimbo la Vunjo la Mhe.Mrema Lyatonga wa TLP ambapo mwanzo walimpa 50% na sasa wamempa 54% ilhali yule wa CCM akipewa 32% badala ya 39%!Sababu ya makosa haya kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi ni kwamba walikokotoa harakaharaka kutokana na shinikizo la wapiga kura kutaka wapewe matokeo ya kura haraka!!!!

Soma hii:
''..........Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.
Kadhalika katika matokeo hayo mapya ambayo Mwananchi inayo nakala yake, kura za mgombea wa CCM, Chrispin Meela zimeshuka kutoka 23,870 hadi 17,498, tofauti ambayo ni sawa na asilimia 39.
Katika matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi Moshi Vijijini, Annah Mwahalende mbele ya wagombea hao, Mrema alikuwa amepata kura 30,810 tofauti
lakini matokeo ya awali yanaonyesha alipata kura 29,047.
Kwa matokeo hayo mapya, Mrema alishinda kwa asilimia 54 huku Meela wa CCM akiibuka wa pili kwa kupata asilimia 32 na si 39. John Mrema wa Chadema alipata asilimia 12 na si 10, huku David Lyimo wa NLD akipata asilimia 2 badala ya 1............''.


Source:Mwananchi


Sasa hii ni kwa jimbo la Vunjo peke yake kwa Mhe. Mrema. Vipi kwenye maeneo yaliyokuwa na upinzani mkali wa CHADEMA? Huko ndiko kutakuwa na madudu ya ajabu sana!. Kwa hiyo chondechonde CHADEMA tukusanyeni ushahidi tuwahi Mahakamani tuweze kupewa haki yetu.

 
Ccm imekiri nayo kuwa watz hawaitaki......wanajua kuwa tunajua walivyoiba kura.......wamechoka wamebaki kuichukua chao mapema kwa miaka hii mitano wanayotaka kututwala kwa nguvu na ambapo tunaendelea kuwakataa kwa nguvu zetu....................acha wateuane...acha wagawane madaraka..........acha wagane ardhi ya tz....kikwte ajue sisi hapo baadaye hatutasema aachwe apumzike tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria kwa kuwalinda mafisadi na kujitengenezea kampuni feki kwa kushirikiana na akina lowasa na rostamu
 
I missed much you mtikira....mtetezi wa wanyonge kwa vitendo na mtu mwenye uwe4zo wa kuthubutu
 
A great thinker wants us to believe election results announced by one person not an institution!!!. If one don't want to trust institutiona results how can that same person trust results announced just by one person. Tunaelekea wapi great thinkers?
 
KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU
TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA
Edward Lowasa ni balaa kwa Taifa!

Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha
CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine,
kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa
kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni
ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.
1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowasa na
wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya
wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa
kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa ameanza kampeni ya urais
Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu
na kumwaga rushwa ya kutisha!
2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake,
katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na
Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowasa
amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi
katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa
kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa
Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo
ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi,
kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini,
upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu
sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa
nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani,
kumehusika ‘’Money laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo
yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa
ajili ya Taifa.
Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa
kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na
Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa
nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na
taratibu za Utawala wa Sheria
4 Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia
kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya
mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza
nchi nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano
makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na
wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu
Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa
mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa
asilimia 95 ya wananchi!
Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea
kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu
ya “Kilimo kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!
5 Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa
sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na
kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi
zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6 Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa
sababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli
wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu
mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua
mvua Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia
kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi. Ni mlemavu
wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa,
anayeweza kumruhusu fisadi Edweard Lowasa agombee urais.
Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward
Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu
Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa
kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza
hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili
ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la
kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!
Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh
Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward
Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi
Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa
Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema
wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha
ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.
Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake
wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi
kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa
kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima
mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila
mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha
kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:
a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote
ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa
utendaji wa akili zake.
c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote
yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia
utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa,
hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye
kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote
d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na
udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo
kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa
matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa
mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!
e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa
mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje
ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya
dhamana kubwa aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa
macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa
hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya
afya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa
dhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais
kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha
udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya
anagombea asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli
tunalithamini na kuliheshimu Taifa.
Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya
maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA. Ni dhana potofu
sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa
sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati
wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’.

 
2010 waliiba kura ila inaonekana kulikuwa na sense ya aibu kidogo lakini this time wameamua kutuambia kabisa in advance kuwa goli la mkono haliepukiki huku wakisahau kuwa hiyo ndio akili anayoitumia Nkurunzinza na inampelekea kwenye laana ya juu na kuzimu!
 
Mtikila has spoken true,the last election was been interfearing due to some error...great thinker mtikila
 
Mch. Christopher Mtikila amesema kwamba Dr. Slaa alishinda uchaguzi wa urais kwa 71%, na anamshangaa Dr. Slaa kwa kutokuchukua hatua za kisheria kudai haki yake.

Hata hivyo CHADEMA wametoa tamko rasmi kuwa hawayatambui matokeo ya urais, na hawamtambui Kikwete kama rais wa Tanzania.


source: Mwananchi.

Vip kuna utata gani hawa watu kutokuwepo siku ya alhamis kuvunja bunge?? Maana atakuwepo huyohuyo!!
 
Back
Top Bottom