Mtikila Kuzuia Uchaguzi Mkuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila Kuzuia Uchaguzi Mkuu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by RRONDO, May 31, 2010.

 1. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,782
  Likes Received: 20,717
  Trophy Points: 280
  Mtikila akusudia kuzuia Uchaguzi Mkuu

  Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Chritopher Mtikila, ameungana na azma ya Chama Cha Jamii (CCJ), kutangaza kusudio la kuiomba Mahakama Kuu isimamishe Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

  Tofauti na CCJ inayoazimia kuzuia uchaguzi huo iwapo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, haitatoa usajili wa kudumu kabla ya kuanza kwa mchakato wake (uchaguzi), Mchungaji Mtikila, anaainisha sababu mbili.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila, alitaja sababu hizo kuwa ni marekebisho ya kifungu cha Sheria ya Uchaguzi kinachozuia matokeo ya mgombea urais kuhojiwa na chombo chochote baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


  Mchungaji Mtikila, alisema kifungu hicho kinapaswa kufutwa ili kukidhi matakwa ya haki za binadamu na misingi ya demokrasia.

  Mchungaji Mtikila alitaja sababu nyingine kuwa ni kutoa fursa kwa mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, aruhusiwe hata kama hana kitambulisho cha mpiga kura.


  Pia Mchungaji Mtikila, alitoa rai kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, kuharakisha hukumu ya rufaa ya kesi ya mgombea binafsi, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea, kutokana na ucheleweshaji wa hukumu hiyo.

  Alisema kitendo cha kutomtambua mtu asiyekuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kumzuia kutochagua viongozi wake, ni kumnyima haki ya msingi.

  Alitoa mfano kuwa sheria nchini Australia inatamka kuwa raia wake wenye sifa za kupiga kura wanastahili kufanya hivyo na kwamba ni kosa la jinai kuzuiwa kupiga kura.

  Alisema sheria kama hiyo inapaswa kutumika hapa nchini ili wadau wa uchaguzi ikiwemo serikali, waelewe umuhimu wa kura za wananchi.

  Alisema yapo mambo mengi katika Katiba ya nchi, ambayo yanatakiwa yabadilishwe ili Watanzania waweze kuwa na wigo mpana wa kufanya uamuzi kuhusu nchi na rasilimali, viwe mikononi mwao na vizazi vijavyo.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  anahaki ya kwenda Mahakamani kuidai haki anayoona inabakwa na Watawala.
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutaona mengi toka kwa wachungaji walio wacha professinal zao na kukimbilia kwenye siasa. Kuna nchi nyingi Mr. Mchungaji hazimruhusu raia kupiga kura mpaka ujiandikishe.

  Hoja zako MR. Mchungaji unaweza kuzipeleka mahakamani sababu huko wakotayari kusikiliza utumbo wowote lakini hakuna sababu za kuzuiya uchaguzi usifanyike October Bwana asifiwe!
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na hata wanajeshi walioachana na huko na kwenda kwenye siasa!
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi chadema bado hawaja li-support hili la Mchungaji? Nawasubiri watatamka, nikawaida yao kuunga mkono pumba za wachungaji!

  Halooo Mchungaji Slaa are you there? can you hear me ?
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwani wachungaji wamekukosea nini, yeye kama mwananchi wa tz anayo haki kufanya chochote, unaonekana una chuki na wachungaji, umesahau kuwa hata mashehe wako kwenye siasa, na mwinyi ambaye alishawai kuwa rais wa jamhuri ni shehe na ana msikiti wake kule mikocheni...achana na chuki zako juu ya wakristo..
   
 7. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni hivyo vyama butu kuongea tu kama makopo tika bila vitendo. Kama vingekuwa viko serious na kufanya kazi kwa pamoja hata Katiba ingekuwa imeisharekebishwa au kuandikwa upya. Hawana mbinu yoyote ya kuwahamasisha wananchi kutumia people's power. People's power ndiyo njia pekee iliyobaki ya kuleta mageuzi ya kweli. Kesi mahakamani zinachukua muda mrefu na inategemea ziko kwa hakimu gani. Kama ni hakimu kada wa CCM hamtapata kitu. Amani, amani, tunayoubiliwa kila siku ni kasumba ya kutupumbaza.
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Coward coward, watu kama hawa Dr. Slaa akiingiaga hapa wao wanaingia Mitini LoL
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kina slaa wanajua fika Mtikila hawezi kuaminika, ni msaliti na ana uchu wa hela. Hili suala serikali ikimtupia vihela kidogo basi atawaumbua wapinzani wote. Mnasahau vijihela vya RA vilivyomuabisha.

  Ni bora akina Slaa wakaachana naye kabisa.
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu Bull katokea wapi tena na chuki zake binafsi? Unajua watu wengine mapandikizi eh!
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Wazo lako zuri sana lakini kwa jinsi ulivyo represent linaleta ukakasi, mahakama acha zifanye kazi yake - Peoples power inakuwa suruhisho la mwisho kabisa endapo mambo yanakuwa yanaharibika 100% - lakini kusimamia ukachochea kitu kama hiki bila sababu za maana hiyo inakuwa uhaini na ni dhambi pia. Tuendelee kudai haki zetu kupitia mahakama bado mimi ina imani nazo, hata hili la mgombea binafsi lipe muda tu utaona matunda yake. Upande wa pili mimi bado nina imani ya katiba yetu ingawa pia ina mambo yanayotakiwa yafanyiwe marekebisho.

  Mchungaji wacha aendelee na kudai mambo ambayo ameamua kuyasimamia hakuna kilichoharibika - najua mzee unataka wotee kwa pamoja tudai :- Marekebisho ya katiba tukimaliza tu then tuingie hili la Tume huru ya uchaguzi then tumalizie na la mgombea binafsi kabla ya uchaguzi mkuu octoba. kumbuka mzee mambo huwa yanaenda hatua kwa hatua, tutafika tu weka subira - hakuna haja ya kukurupuka ghafla tutajichanganya wenyewe.
   
 12. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  goood
   
 13. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kweli hili la matokeo ya urais kutohojiwa na chombo chochote ni kosa kubwa. Kumbuka tume ya uchaguzi si mahakama hata kama mwenyekiti wake ni jaji. Kumbuka pia mgombea urais si mmoja, anakuwa na wapinzani wake sasa ukisema tume ikitangaza basi wasihoji, je kama wanaona mahali fulani haki haikutendeka waende wapi? Msituni?
   
Loading...