Mtikila aomba kuunganishwa kesi ya Kafulila

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
10570416_1501650860070060_1815731930637391272_n.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ameomba kuunganishwa katika kesi ya madai inayomkabili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), imefungua kesi ya madai dhidi ya Kafulila katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ikiomba aamriwe kuilipa fidia ya sh. bilioni 310 kutokana na kutangaza taarifa za kashfa dhidi yao.

... Kafulila akizungumza kwenye mjadala katika eneo la Urusi Mwanga mjini Kigoma jana, alisema Mchungaji Mtikila ameomba kuwa mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo huku Chama chake cha DP kikiwa mshitakiwa wa tatu.
Pia Kafulila alisisitiza kuwa kamwe hakukurupuka kuibua kashfa hiyo ya ufisadi katika akaunti ya Escrow na kwamba, yuko tayari kwa lolote.

Mchungaji Mtikila amethibitisha kukubali kwake kuunganishwa kwenye kesi hiyo inayomkabili Kafulila kwa kusema "Nimekubali kuunganishwa katika kesi hiyo ili kutetea haki ya wananchi wa nchi yetu kama Katiba inavyosema"
 
Nina hakika baada ya siku mbili Haya mafisadi ya escrow yatafuta kesi lets wait

BACK TANGANYIKA
 
Kiboko yake huyo ni Rostam, alivyomletea za kuleta, Rostam akatoa ushahidi wa yeye kupewa pesa na Rostam na kasaini. Toka siku hiyo kimya, hajamtaja tena Rostam

Ukiwa muongo inataka uwe na kumbukumbu.

Hapo anajidhihirisha kuwa he is simply an opportunist.
 
U ddnt talk anythng about the thread,u just brust out ur views not even tryn to connect to the thread.
 
Hili sasa linanoga!!!!!

UKAWA re surfacing on this???!!!
 
Mtikila ni Kiboko ya serikali ya CCM!
 
Kiboko yake huyo ni Rostam, alivyomletea za kuleta, Rostam akatoa ushahidi wa yeye kupewa pesa na Rostam na kasaini. Toka siku hiyo kimya, hajamtaja tena Rostam

Ukiwa muongo inataka uwe na kumbukumbu.

Hapo anajidhihirisha kuwa he is simply an opportunist.

Unatutoa kwenye hoja ya msingi. Hoja hapa ni Kafulila + Mtikila + Escrow. Kama una ishu ya Rostam, hiyo ni nyingine
 
Ile m3 walikopeshana kirafiki, siasa ilipowatofautisha ndipo Rostam akafichua vitu nje ya siasa, we vip bwana!
 
Kweli Mtikila kiboko, watu wanavyoziogopa kesi, yeye ndiyo kwanza anafanya kuombwa aunganishwe nayo, kesi ya Mtikila?!

Hapo sasa ndiyo patanoga, huyo jamaa aliyemuita Kafulila 2+2, aliyesema kuwa hizo pesa za Escrow hazikuwa na mwenyewe, ndiyo maana wenye meno ya kuzitafuma walijichotea kiulaini, tumwone sasa kama ana uwezo wa 'kuzichapa' na Mchungaji Mtikila?
 
Kiboko yake huyo ni Rostam, alivyomletea za kuleta, Rostam akatoa ushahidi wa yeye kupewa pesa na Rostam na kasaini. Toka siku hiyo kimya, hajamtaja tena Rostam

Ukiwa muongo inataka uwe na kumbukumbu.

Hapo anajidhihirisha kuwa he is simply an opportunist.

Mwezi mtukufu si kufunga kula tu bali ni pamoja na kutenda mema. Siasa za kuchumia tumbo tuweke kando tuweke utaifa mbele. Kuna watu wanateseka kutokana na mikataba mibovu iliyosainiwa na wachumia tumbo wasio na huruma hata kidogo inawagarimu wanyonge wasio na hatia hata kidogo.
 
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ameomba kuunganishwa katika kesi ya madai inayomkabili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), imefungua kesi ya madai dhidi ya Kafulila katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ikiomba aamriwe kuilipa fidia ya sh. bilioni 310 kutokana na kutangaza taarifa za kashfa dhidi yao.

... Kafulila akizungumza kwenye mjadala katika eneo la Urusi Mwanga mjini Kigoma jana, alisema Mchungaji Mtikila ameomba kuwa mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo huku Chama chake cha DP kikiwa mshitakiwa wa tatu.
Pia Kafulila alisisitiza kuwa kamwe hakukurupuka kuibua kashfa hiyo ya ufisadi katika akaunti ya Escrow na kwamba, yuko tayari kwa lolote.

Mchungaji Mtikila amethibitisha kukubali kwake kuunganishwa kwenye kesi hiyo inayomkabili Kafulila kwa kusema “Nimekubali kuunganishwa katika kesi hiyo ili kutetea haki ya wananchi wa nchi yetu kama Katiba inavyosema.”

See More
Huyo jamaa anafahamika kwa aka ya mzee wa kununua kesi!
 
Mwezi mtukufu si kufunga kula tu bali ni pamoja na kutenda mema. Siasa za kuchumia tumbo tuweke kando tuweke utaifa mbele. Kuna watu wanateseka kutokana na mikataba mibovu iliyosainiwa na wachumia tumbo wasio na huruma hata kidogo inawagarimu wanyonge wasio na hatia hata kidogo.

Wacha porojo wewe, nani anaeteseka? wewe ulimsaidia vipi huyo anaeteseka?

Mikataba? kuna mkataba mbovu zaidi ya chama kuuziwa fuso chakavu mbili kwa millioni mia sita?
 
Unatutoa kwenye hoja ya msingi. Hoja hapa ni Kafulila + Mtikila + Escrow. Kama una ishu ya Rostam, hiyo ni nyingine

Na mimi si nimemuongelea Mtikila hapo, au huoni? au ukisoma huelewi? unanchekesha!
 
Back
Top Bottom