Mtihani kwa CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani kwa CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Apr 20, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nimesoma kwa makini maoni ya Mwanakijiji pamoja na maoni ya Slaa,Zitto,Lwetama n.k.Nilichokibaini cha msingi hapa ni kuwa Mwanakijiji ameanza kupata wasiwasi na mbinu inayotumiwa na CDM katika harakati za kushika dola.Kwa Mwanakijiji anaona kivuli cha CCM kinaanza kuongezeka hasa baada ya mkakati wa kujivua gamba ambao kimsingi unanafasi yake kubwa katika mabadiliko ya Chama.Hapa Mwanakijiji anaona CCM katika uvuaji gamba haikomei kwenye mabadiliko ya CC na Sekretarieti yake,bado inamikakati makini ya kimafia yenye kuhakikisha CDM inapotea katika masikio ya Wananchi.

  Upande wa pili,Mwanakijiji anaitizama CDM kama chanzo cha kuipa nguvu CCM badala ya kuidhoofisha.Mwanakijiji anaitizama CDM mbali na kupuuza mabadiliko ndani ya CCM bali pia imekuwa msaada mkubwa kwa mabadiliko hayo.CDM hapa inashindwa kutambua ni wapi CCM inapaswa kutokomezwa?na ni silaa gani ya kuitokomeza CCM?.

  Maoni ya DR. Xavier Lwetama ambayo yameonekana wazi kupinga maono ya Mwanakijiji inadhihirisha uvivu wa kufikiri alionao.Lwetama mbali na kuwa na focus ya kutamani CCM ife ata Leo lakini inaonyesha njia ya CCM kufa haioni zaidi ya kutanguliza chuki binafsi na wala si " strategy".Dr. Lwetama akiwa anajinadi kama Mwanachama mfu wa CCM ,hii pia inaongeza changamoto ya kutokukubalika kwa hoja yake kwani ni dhahiri anaonyesha ushabiki wake kisiasa ni katika mlengo wa "opportunistic".Maoni yake ya kudai ushindani wa kimaadili (kutokutumia mbinu ya kudhoofishana) ila CCM ife hapa ndio njia na mbinu ya Lwetama inaposhindwa.CCM haiwezi kufa bila kudhoofika,ajali kwa binadamu ni sawa lakini si mfano wa CCM kufa kama ajali ya basi.

  CDM imeonyesha ku-survive kwa makosa ya CCM,hii inamaana CCM ikijirekebisha kutokana na makosa yake CDM haipo.Mwanakijiji anapata wasiwasi kwani mwazoni CDM ilikuwa inampa nguvu na kuona kifo cha CCM kinakaribia sasa wasiwasi unatanda baada ya kuona CDM imempa kikombe CCM (adui) sasa karudi kazini na dhana za kummaliza mtoa kikombe.
  Mwanakijiji hajakosea kwani anajua CCM si chama cha kawaida kama CDM inavyodhani.Anatambua na kusifu katika mada yake kuwa hawa ni watu wa siasa za Kisayansi na mbinu za kimafia kwa maana ya ubingwa wa kuuwa vyama pinzani.Ni kweli CCM inauwezo huo na kama CDM haitofikiri njia mbadala za kujiimalisha (kuachana na nyimbo za list of shame,remix etc.) ambazo CCM imeisha zirekodi kwa jina lake itakufa kabla ya 2015.

  CCM haitanii na ndio kwanza safari imeanza na wanakwambia si nguvu ya soda.Kumbuka uzoefu wa CDM kisiasa ni mdogo kulinganisha na CCM hivyo na adui CCM ameishatambua silaa ilizonazo CDM sasa kilichobaki ni mchakato wa kukimaliza kisayansi.

  Changamoto anayotoa Mwanakijiji kwa CDM ni kubwa kutokana na maswali haya.
  Je!CDM watauweza mziki wa CCM?Je! CDM wanauwezo wa kucheza bila kusikiliza mziki wa CCM?.Ikumbukwe kuwa Watanzania watampigia kura Yule mwenye uwezo wa kumiliki Jukwaa.
   
 2. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeandika sana lakini mwisho wa siku wewe mwenyewe utaonekana mshabiki zaidi ya Lwetama na utabakia kuwa mlamba viatu wa CCM.
   
 3. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sijaona hoja ya maana katika makala yako na hata hayo ya Mwanakijiji unayoelekea kuyasifia hapa zaidi ya kuonesha ushabiki wako wa CCM kimgongo mgongo (kinyumenyume). Huko mnakokusifia kujisafisha kwa CCM kuko wapi?Unafikiri CCM hata ikijisafisha itabadilika? Uliona wapi Simba au Mbwa mwitu akajikarabati sura au ngozi yake na kisha kwenda kwenye kundi la Kondoo na kudai eti na yeye sasa ni kondoo na hivyo asiogopewe tena. Acheni kuja na propaganda za kutaka kupima upepo kupitia watu maarufu kama Lwaitama.
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Hayo ni maoni binafisi ya Mwanakijiji na sio lazima iwe reality. Tatizo la watanzania wengi hata wasomi ni uvivu wa kufiukiri na kutaka kazi hiyo ifanywe na watu wengine. Ningekuelewa zaidi Apolycaripto kama ungekuwa unakuja na mada yako. Lakini umesubiri Mwanakijiji aumize kichwa ndipo uongeze nyama.
   
 5. k

  kuruti Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtazamo unaoonekana hapa kwamba CDM haimiliki jukwaa au CCM haijajisafisha sina ujuzi nao. Ila kwa maoni yangu, CCM inacheza michezo bila kuwa na long term strategic planning wakati CDM wanacheza pale CCM wanapoamua kuweka Muziki. Kumekuwa na tatizo kubwa la vyama vya siasa kupingana badala ya kuweka wazi njia mbadala kisera. Nimeona katika majimbo mawili ambayo CDM wanaongoza halmashauri wakifanya vema, kule Mara na swala la elimu na kule Hai na swala la chakula. Lakini alternative Better plan ya CDM over ile ya CCM iko wapi? CCM hawaonyeshi KUHAMA kutoka kwenye sera za Oysterbay na kuhamia Manzese kwa walala hoi, sana wanaonekana kutembelea Manzese kushangaa umasikini ambao wao nao hawaujui. Lazima tufike mahala tuwe na Objective solution. Ila kwa sasa ni maigizo tu, CDM wakiendelea kukosoa CCM na CCM bila aibu wakikiri kupotoka na kuahidi kurekebisha kwa maneno. KWA SASA HATUENDI POPOTE TUMESIMAMA!
   
 6. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,226
  Trophy Points: 280
  Sionagi mchango au point yeyote kwa kila anachoongea lwaitama, zaidi ya kutoka mapovu tu.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Naona umechambua kwa kina sana na kuona mapungufu yao katika hoja zao.

  Mimi nilichogundua na kubainisha kwao kwa Mwanakijiji na Daktari Lwetamwa ni kuwa wameghumiwa na USHABIKI na wamesahau kabisaa kuwa wana wajibu wa kuelimisha jamii na kuhabarisha jamii kutokana na maandiko yao ya mada husika
   
 8. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuna mawili: Either una akili sanaaa au ni mbumbumbu mnooo! Hebu nikufuatilie, ntafahamu tu soon.
   
 9. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  shaka ondoa utaona mwaka 2015 moto wa chadema..
   
 10. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kina ni relative term bana. Sisimizi ndani ya kisoda ni kama ametoswa ziwani vile. Kuna kina gani katika kuamini kuwa "kujivua gamba" kwa CCM ni jambo halisi na si kuwachezea shere wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla? Kuna kina gani katika kutaja taja Mwanakijiji na Dr Lwaitama na unazoziita "chuki binafsi" zake? Kuna kina gani hapa mfano:

  Hayo ni maswali kwasababu yana ishia na alama ya kuuliza au kwasababu yanahitaji majibu? Mziki gani CDM wantakiwa waucheze na wakati huohuo wanatkiwa kucheza bila kuusikiliza? If this qualifies for an in-depth thinking, I demand the dimensions of the depth first!
   
 11. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ahhh,nani so far anayecheza muziki wa mwenzie?
  Yah,Dkt Lwaitama was very right.Kinachoisukuma CCM kuichukia Chadema ni sababu za kibinafsi zaidi kulikoni nyinginezo.Practically,jambazi huwa na chuki na polisi kwa vile the latter poses a threat kwa survival of the former.CCM haina itikadi kwa sasa,inaendeshwa kwa mtindo wa zimamoto,na uhai wake ni kwa msingi wa siku hadi siku.Usisahau umri wa chama hiki wakati unakilinganisha na Chadema.Lakini shoka dogo linaelekea sio tu kuyumbisha mbuyu bali pia kuuangusha ("Small Axe"~Bob Marley).

  Wachambuzi wetu wakati mwingine wanakuwa kama wanasiasa.Very good at predicting the worse.Unfortunately,and with all due respect,background ya mahusiano kati ya Mwanakijiji na Chadema sio ya kupendeza sana.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Mimi sikusoma huo Mtihani wa Mwanakijiji kwa CDM kutokana na kwamba siamini CDM wana mapungufu ya kiuongozi na zaidi ya hapo CDM haina sababu za KUIGA kila kinachotendeka CCM nao wakifanye.

  Ikumbukwe tu kwamba CCM wanajivua magamba leo kwa sababu wanaamini kuwepo kwa Mafisadi ndani ya chama chao, hii ikiwa na maana zaidi kwamba kuwepo kwa Lowassa, Rostam na Chenge ndani ya Uongozi wa chama kunawadhoofisha badala ya kuwajenga...this has nothing to deal with national interest..

  Labda niwakumbushe tu kwamba ndani ya CCM kuna mgawanyiko mkubwa uliopelekea mabadiliko haya na hadi leo hawana ushahidi wa kutosha kuwaondoa vigogo hao madarakani isipokuwa ni kutokana na TUHUMA.. Hivyo kukifanya chama kujivua gamba lakini bado wana sumu ile ile ya Ufisadi usiotuhumiwa. CCM wameweza kuchukua ushindi wa chaguzi zote za nyuma kwa Ufisadi wa makundi makundi hivyo ni vita baina ya mafisadi toka kundi moja kwenda jingine ndani ya chama, lakini Kitaifa bado chama hakijakubali kuacha Ufisadi ktk utekelezaji wa agenda zake.

  On the other hand tuna Chadema ambao chini ya uongozi huu uliopo, chama kime gain popularity kubwa sana na mikakati yake imeonyesha wazi kufanya kazi kubwa kupambana na CCM pamoja na vyama ambavyo vilikuwa na malengo ya kukiangusha kabla hata ya uchaguzi wa mwaka 2005.

  Pia Chadema imeonyesha kuteteza zaidi national interest badala ya zile za chama kwa kuwaonyesha madudu yote yanayofanyika chini ya chama CCM na uongozi uliopo. Hivyo kikufanya chama kiwe kioo na somo zuri kwa wananchi kufahamu jinsi mfumo mbaya wa CCM unavyofuja maliasili na rasilimali zao. Na huwezi kurekebisha vizuri zaidi azma kwa kubadilisha viongozi ikiwa silaha hii inafanya kazi vizuri sana.

  Sasa sii busara hata kidogo kwa CDM kubadilisha uongozi wake kwa sababu tu CCM wamebadilisha au kujivua gamba, hali CCM wana kila sababu ndani ya chama chao kufanya mabadiliko hayo ingawa binafsi sioni kama yatawasaidia, na CDM wamefanya vizuri sana chini ya uongozi uliopo hivyo kufanya mabadiliko ni kukubali kupunguza nguvu ya chama au kukubali kuna mapungufu ambayo ningependa yaorodheshwe ili umuhimu wa kufanya hivyo ufahamike.

  Ikiwa kweli swala kubwa la CDM kuondoa uongozi uliopo unatokana na TUHUMA zinazosambaa, basi dawa yake sii lazima iwe kujivua gamba kwa sababu hawana maradhi sawa na CCM isipokuwa ni kuongeza nguvu ya chama kiwafikie wananchi kona zote za taifa na kikubalike..
  Ni imani yangu kwamba chama kuitwa cha Kikabila au kidini haiwezi kutokana na washiriki wake wakubwa bali kuchukua mila na desturi za kabila fulani au dini fulani na kuziweka ktk katiba au sera za chama..

  CDM inaweza tu kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi ikiwa watuhumiwa ni Wakabila au Wadini lakini chama kizima kinapotuhumiwa kuwa ni chama cha kikabila au kidini basi huwezi kuwaondoa baadhi ya viongozi ili kurudisha hadhi isipokuwa ni swala la chama kizima kubadilisha au kujijena Kitaifa zaidi. jambo ambalo nina hakika CDM wanalifanyia kazi kwa nguvu zote na hakika leo hii CDM sii chama kinachokisiwa na Ukabila wala Udini zaidi ya washabiki wa CCM na CUF..

  Uongozi wa CDM na sekretariet yake unastahili sana kupongezwa zaidi ya kutafuta mchawi ndani ya chama. Na hakika migogoro mingi ya Chadema imetokana na matamanio ya kibinadamu ambayo kila mmoja wetu angependa kushika wadhifa fulani ili apate umaarufu ambao ndio sifa kubwa ya kiongozi wa Kitanzania. Na kibaya zaidi ni watu kushabikia mtu ili kumpa au kumwondolea Umaarufu ili mradi tu matatizo ya chama yamekuwa ni ya kibinafsi zaidi ya agenda ya chama kiutawala.

  CDM ongeza makali yako haya ya kujivua gamba ni matatizo ya CCM ambao hawana dawa zaidi ya kutuliza homa kali waliyokuwa nayo, gonjwa lipo palepale. Sii vizuri kwa CDM ambayo haina maradhi kuanza kutumia madawa kuondoa virusi vya Ufisadi, ila ni vizuri kwa CDM kuchukua kinga against virusi vya mapungufu wanayotuhumiwa..Na kinga hiyo sii uongozi wa chama bali muundo mzima wa chama hiki.
   
 13. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Dr. Lwaitama.
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  :spy: zaidi!!!

  Mpasuko ndani ya CCM ndo kwanza umeanza!! Wanajila wenyewe kwa wenyewe!!!
   
 15. k

  kany Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaribu kulivua hilo gamba uone kama hutaona mchango wake!
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Apo, kwanza sijajua kwa nini umechambua mawazo ya wenzako badala ya kutoa ya kwako huko huko mada ilipobandikwa

  Hata hivyo umewasaidia sana Chadema kupata ushahidi kwamba kazi waliyofanya imefanikiwa sana. Kazi kubwa na ya kwanza ya chama cha upinzani ni kukosoa sera na utendaji wa chama tawala. Umedhihirisha Chadema wameifanya
   
 17. m

  mzungukichaa Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Sioni haja ya wewe kuanzisha topic nyingine wakati una quote topic ya mwanakijiji. Ni bora haya mawazo yako ungechangia kwenye topic ile tu badala ya kuwa na topic nyingi za ku copy and paste.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tathmini, uchambuzi, sijui vitu gani vinavyoandikwa sasa hivi kutokana na CCM 'kujivua gamba'.!!! Mtaandika sana lakini mwisho wa siku mtabaini kuwa CCM inafanya usanii tu -- haiwezi kujivua gamba -- maana kama gamba ni ufisadi -- basi imo katika damu, siyo juu ya ngozi.

  Hata vigogo 100 'mafisadi' wakiondoka CCM -- ufisadi utabakia katika system nzimna ya serikali yake maana kansa hiyo imeshakuwa institutionalised.

  Kwangu mimi 'kujivua gamba' ni kuitokomeza CCM into dustbin of history -- kwani yenyewe haiwezi kabisa kujitakasa. Na Chadema wasiridhike na wanachofanya CCM sasa hivi -- wahakikishe chama kinaondoka.

  Gazeti la Raia Mwema leo limesema eti Slaa anatumiwa na mafisadi bila ya yeyte kujijua. Sijaona nonsense kama hii. Ni mbinu tu za mafisadi! Yaani Slaa aache kuibana CCM na JK wao kwa ufisadi eti tu kwa sababu akina RA na EL au/na mawakala nao wanaonekana kuibana CCM kuhusu ufisadi huo huo -- hivyo Slaa na hao mafisadi wanakula sahani moja sasa!!!

  Msisahau kwamba kama akina RA na EL wanaonekana kumbana JK kwa ufisadi basi wana lengo lao -- kujaribu kumtisha JK kwamba asiwatose kwani mbona walifanya yote yale pamoja naye? Yeye Slaa ana malengo tofauti kabisa -- na kama yanaonekana yanalingana -- basi ngoma inogile!
   
 19. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Guys, am not getting it here! Kwa hiyo hapa ni kwamba hili gamba la ccm kulivua tu cdm inakufa? Hivi imethibitishwa pasipo shaka kwamba hili gamba ljtaiacha ccm salama? Nadhani tunatakiwa kufanya upembuzi yakinifu na ni mapema kutabiri usafi wa ccm baada ya hilo gamba.
   
 20. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
   
Loading...