Mtihani kwa CDM

Sionagi mchango au point yeyote kwa kila anachoongea lwaitama, zaidi ya kutoka mapovu tu.

Kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo na unafikiri kwa tumbo badala ya ubongo utauonaje mchango au point ya Lwaitama aliyekwenda shule?
 
Sijaona hoja ya maana katika makala yako na hata hayo ya Mwanakijiji unayoelekea kuyasifia hapa zaidi ya kuonesha ushabiki wako wa CCM kimgongo mgongo (kinyumenyume). Huko mnakokusifia kujisafisha kwa CCM kuko wapi?Unafikiri CCM hata ikijisafisha itabadilika? Uliona wapi Simba au Mbwa mwitu akajikarabati sura au ngozi yake na kisha kwenda kwenye kundi la Kondoo na kudai eti na yeye sasa ni kondoo na hivyo asiogopewe tena. Acheni kuja na propaganda za kutaka kupima upepo kupitia watu maarufu kama Lwaitama.

Kwa bahati mbaya sana siasa haziko unavyofikiri mkuu, si kinadharia wala vitendo.
Kama unaamini kuwa kashfa za ufisadi ni sababu ya ushindi hafifu kwa Ccm 2010 ambayo pia ndiyo mafanikio kwa Chadema 2010 then utakubali kuwa Chadema kitakufa kwa kukosa lishe (kashfa za ufisadi) ikiwa Ccm watakinyima chakula kwa kuendelea na kampeni yao ya kujivua gamba ambayo wewe unaibeza pengine kwa kujifariji kuwa si chochote, si lolote.
Siamin huna macho ya kuona...
 
CCM haitanii na ndio kwanza safari imeanza na wanakwambia si nguvu ya soda.Kumbuka uzoefu wa CDM kisiasa ni mdogo kulinganisha na CCM hivyo na adui CCM ameishatambua silaa ilizonazo CDM sasa kilichobaki ni mchakato wa kukimaliza kisayansi.

Kweli CCM kwenye udhalimu haitanii; uzoefu wa CCM ni ule wa kikasuku hata siku moja hawajatafsiri maneno yao kwa vitendo CDM wanalijua na wananchi wanajua. Mbona CCM kwa udhaifu huo tayari anayumba kama kalewa? Kwa dozi ya utangulizi tu ya CDM kwa CCM tayari anaweweseka kukipasua chama lake ndio ujue CCM ni chui wa karatasi kama washirika wake wa aina yake.

Changamoto anayotoa Mwanakijiji kwa CDM ni kubwa kutokana na maswali haya. Je! CDM watauweza mziki wa CCM?.

CDM hawajawahi, hawatacheza na wala hawafikirii kucheza muziki wa CCM kwa sababu ni makelele tu yasiyo na mvuto.

Je! CDM wanauwezo wa kucheza bila kusikiliza mziki wa CCM?..

CDM hawajui na hawataki kujua wala kusikiliza makelele ya CCM.

Ikumbukwe kuwa Watanzania watampigia kura Yule mwenye uwezo wa kumiliki Jukwaa.

Watanzania wanalinganisha hoja na ukweli wa maisha yao bila kupanda fuso kwenda kwenye upuuzi wa majukwaa ya CCM
 
miziki ya CCM ni ya KIDUKU NA TAARAB MANA HATA KWENYE KAMPENI ZILIKUWA MIPASHO MIZIKI YA CDM NI SIASA SAFI NA SERA ZENYE AKILI SIO KWENDA KUBEBA WANANCH NA MALORY

Let me be open CCM is no Longer exist since 2010 now its just the shadow of CDM is coming to be realistic so dont waste your time my friend I have ana experience on this you cant compare CCM Versus CDM for anything

CCM is :sleepy:
 
mimi nadhani hii hoja ya CCM kujivua gamba au kijirekebisha mwanakijiji kaitoa mapema sana, ukizingatia ukweli kwamba CCM bado ina gamba na chafu mbele ya wananchi, labda baada ya siku 90 walizotoa kwa mafisadi,
kama watafukuzwa basi hii hoja inaweza kuplay, maana gamba sio makamba na kama wao wanadhani kulopoka kwa makamba na kuchakachua kwake mchakato kura za maoni kupata wagombea wa ubunge wa ccm ni gamba basi imekula kwao,
ili ni gamba kwa upande wa CCM, Lakini magamba tunayotaka wananchi wajivue ili tuwarudishie imani ni ufisadi na HII NINAKULA MPAKA KWA KIKWETE rejea list of shame, kwa kifupi hakuna gamba walilovua mpaka .
lakini pia CHADEMA ni chama makini kuliko wengi wanavyoweza kufikilia
 
Kaka umetoa maelezo mengi ila umesahau kuwa watanzania walio wengi wa sasa wanaHitaji maisha bora na wala SIO SIASA ZA KWENYE MAJUKWAA,Watanzania wataendelea kuipenda ccm iwapo itaweza kuwaondolea ugumu wa maisha.Sasa basi naomba nikuulize swali mpaka sasa ccm wamefanya jambo gani la msingi ili kutufanya maisha yetu yawe bora?Kama kunajitihada zakimaendeleo ambazo zimefanyika basi ccm kweli itaongeza wapenzi lakini kama mambo ni yaleyale Madini,Bahari,Misitu,Mbuga za wanyama,Mito,mabonde yenye rutuba hayaleti maendeleo kwa watanzania ukiongezea na uduma mbovu za kijamii basi tegemea anguko kubwa zaidi kwa ccm yako 2015.
 
umemaliza kila kitu apo ,ila wafuasi wa chadema wanajifanya roho za paka mpaka watiwe kwenye gunia wapigwe marungu ndio wanakufa...tatizo kubwa la chadema wanafikiria in short run yani average of 2,5 ,years.forestance ccm strategic plan zao ni si chin ya miaka 20 na kuendelea.....simple chadema kufa kama wakinyimwa kuingia madarakani kwa term mbili tu =10 years...dr slaa hatakua tema wa kulipua mabomu maana atakua ka babu,watu kama kina zitto kabwe wanaokubalika takriban nchi nzima achilia ukanda wao wenyewe wanawaua kisiasa,wenzao ccm wanaanza ku build corparate images za chipukizi kama kina januari,nape etc....wangeangalia mfano mzuri zanzibar cuf walivyofanyiwa umafya mpaka leo maalim seif amekua babu hajiwezi juzi katoka india kupata mshono
 
Umeandika sana lakini mwisho wa siku wewe mwenyewe utaonekana mshabiki zaidi ya Lwetama na utabakia kuwa mlamba viatu wa CCM.

ungecrush point zb jamaa badala ya kuponda it just show that huna point
 
Kweli CCM kwenye udhalimu haitanii; uzoefu wa CCM ni ule wa kikasuku hata siku moja hawajatafsiri maneno yao kwa vitendo CDM wanalijua na wananchi wanajua. Mbona CCM kwa udhaifu huo tayari anayumba kama kalewa? Kwa dozi ya utangulizi tu ya CDM kwa CCM tayari anaweweseka kukipasua chama lake ndio ujue CCM ni chui wa karatasi kama washirika wake wa aina yake.

CDM hawajawahi, hawatacheza na wala hawafikirii kucheza muziki wa CCM kwa sababu ni makelele tu yasiyo na mvuto.

CDM hawajui na hawataki kujua wala kusikiliza makelele ya CCM.

Watanzania wanalinganisha hoja na ukweli wa maisha yao bila kupanda fuso kwenda kwenye upuuzi wa majukwaa ya CCM

uko sahihi kabisa ,watanzania wanafuata hoja,ndo maana wakakipigia kura CCM,ulikuwa wapi naona hawakukuambia.kaka ila kujifariji sio dhambi bali kujidanganya.POLE
 
Nimesoma kwa makini maoni ya Mwanakijiji pamoja na maoni ya Slaa,Zitto,Lwetama n.k.Nilichokibaini cha msingi hapa ni kuwa Mwanakijiji ameanza kupata wasiwasi na mbinu inayotumiwa na CDM katika harakati za kushika dola.Kwa Mwanakijiji anaona kivuli cha CCM kinaanza kuongezeka hasa baada ya mkakati wa kujivua gamba ambao kimsingi unanafasi yake kubwa katika mabadiliko ya Chama.Hapa Mwanakijiji anaona CCM katika uvuaji gamba haikomei kwenye mabadiliko ya CC na Sekretarieti yake,bado inamikakati makini ya kimafia yenye kuhakikisha CDM inapotea katika masikio ya Wananchi.

Upande wa pili,Mwanakijiji anaitizama CDM kama chanzo cha kuipa nguvu CCM badala ya kuidhoofisha.Mwanakijiji anaitizama CDM mbali na kupuuza mabadiliko ndani ya CCM bali pia imekuwa msaada mkubwa kwa mabadiliko hayo.CDM hapa inashindwa kutambua ni wapi CCM inapaswa kutokomezwa?na ni silaa gani ya kuitokomeza CCM?.

Maoni ya DR. Xavier Lwetama ambayo yameonekana wazi kupinga maono ya Mwanakijiji inadhihirisha uvivu wa kufikiri alionao.Lwetama mbali na kuwa na focus ya kutamani CCM ife ata Leo lakini inaonyesha njia ya CCM kufa haioni zaidi ya kutanguliza chuki binafsi na wala si " strategy".Dr. Lwetama akiwa anajinadi kama Mwanachama mfu wa CCM ,hii pia inaongeza changamoto ya kutokukubalika kwa hoja yake kwani ni dhahiri anaonyesha ushabiki wake kisiasa ni katika mlengo wa "opportunistic".Maoni yake ya kudai ushindani wa kimaadili (kutokutumia mbinu ya kudhoofishana) ila CCM ife hapa ndio njia na mbinu ya Lwetama inaposhindwa.CCM haiwezi kufa bila kudhoofika,ajali kwa binadamu ni sawa lakini si mfano wa CCM kufa kama ajali ya basi.

CDM imeonyesha ku-survive kwa makosa ya CCM,hii inamaana CCM ikijirekebisha kutokana na makosa yake CDM haipo.Mwanakijiji anapata wasiwasi kwani mwazoni CDM ilikuwa inampa nguvu na kuona kifo cha CCM kinakaribia sasa wasiwasi unatanda baada ya kuona CDM imempa kikombe CCM (adui) sasa karudi kazini na dhana za kummaliza mtoa kikombe.
Mwanakijiji hajakosea kwani anajua CCM si chama cha kawaida kama CDM inavyodhani.Anatambua na kusifu katika mada yake kuwa hawa ni watu wa siasa za Kisayansi na mbinu za kimafia kwa maana ya ubingwa wa kuuwa vyama pinzani.Ni kweli CCM inauwezo huo na kama CDM haitofikiri njia mbadala za kujiimalisha (kuachana na nyimbo za list of shame,remix etc.) ambazo CCM imeisha zirekodi kwa jina lake itakufa kabla ya 2015.

CCM haitanii na ndio kwanza safari imeanza na wanakwambia si nguvu ya soda.Kumbuka uzoefu wa CDM kisiasa ni mdogo kulinganisha na CCM hivyo na adui CCM ameishatambua silaa ilizonazo CDM sasa kilichobaki ni mchakato wa kukimaliza kisayansi.

Changamoto anayotoa Mwanakijiji kwa CDM ni kubwa kutokana na maswali haya.
Je!CDM watauweza mziki wa CCM?Je! CDM wanauwezo wa kucheza bila kusikiliza mziki wa CCM?.Ikumbukwe kuwa Watanzania watampigia kura Yule mwenye uwezo wa kumiliki Jukwaa.

Naomba utudhihirishie kama wewe ni mtanzania au ni mnyarwanda. Unachoongea ni ideas zilizotoka dodoma na kama bado unafikiri utawapata wananchi wanaosikiliza mawazo kama haya ya Ridhiwani na January basi pole. Nenda vijijini labda utapata babu zetu wanaongojea kumpigia kura nyerere. Try something else or another field.
 
Kuna mawili: Either una akili sanaaa au ni mbumbumbu mnooo! Hebu nikufuatilie, ntafahamu tu soon.
eti Lwaitama anaongea povu? kweli either huyo bwana ana akili saaaaaana (ingawa sidhani) au mjinga kuliko kawaida
 
Sionagi mchango au point yeyote kwa kila anachoongea lwaitama, zaidi ya kutoka mapovu tu.
Lwaitama ni Lecturer wa CRITICAL THINKING AND ARGUMENTATION, wengi walioshia FORM IV huwa wanapata shida sana kumuelewa, Jamaa huwa anatumia maneno na mifano ambayo lazima uwe umefika level flani kumuelewa
 
Haya wewe mwenye macho bepari tuwekane sawa hapa. Kwenye red,mie sijui kama wewe unaamini au la. Lakini kwa mujibu wa ripoti ya consultant wa CCM ambayo ndiyo haswaa inaendesha huu mpango mzima wa kujivua magamba, miongoni mwa sababu kubwa mbili zilizoipa CCM ushindi dhaifu 2010 ni:

  1. Kashfa za ufisadi miongoni mwa makada wake
  2. Siasa za makundi zilizotokana na kura za maoni.
Sasa hebu tuiangalie response ya kuvua magamba tuone kama hii ndio itakua pona ya CCM au la? Kwa akili yako na macho yako unayo-boast kuwa nayo, unaona kabisa kwamba kama CCM itafanya kwa DHATI tendo la kujivua gamba la ufisadi (huku ndio hasa mfumo na mpango mzima unaotajwa kumuweka mwenyekiti wake,JK madarakani) itasalimika? Macho yako hayawezi kuona kuwa ufisadi haumwachi kamwe JK salama kama ukiwa adressed katika kweli? Na kama wataamua kutekeleza KISANII ili chama kisalimike,huoni kwamba unahitaji watanzania wawe usingizini kabisa ili dhana hiyo iuzike?
Unaonaje kuwa kuwa-single out EL,RA na AC kuwa eti ndio mafisadi wa CCM, kutaondoa siasa za makundi na si kwamba itakua ni kujaribu kuzima moto kwa petroli? Mwenye macho tuambie ni kwa vipi CCM itaibuka chama kilichopona katika huu msitu mnene walimojitumbukiza (to me more precise,walimotumbukizwa)? Huu ni mtihani kwa CDM au CCM? TAFAKARI!
Kwa bahati mbaya sana siasa haziko unavyofikiri mkuu, si kinadharia wala vitendo.
Kama unaamini kuwa kashfa za ufisadi ni sababu ya ushindi hafifu kwa Ccm 2010 ambayo pia ndiyo mafanikio kwa Chadema 2010 then utakubali kuwa Chadema kitakufa kwa kukosa lishe (kashfa za ufisadi) ikiwa Ccm watakinyima chakula kwa kuendelea na kampeni yao ya kujivua gamba ambayo wewe unaibeza pengine kwa kujifariji kuwa si chochote, si lolote.
Siamin huna macho ya kuona...
 
Apples, we ni mental slavery. Nimeangalia avatar yako ina mnyororo shingoni, na hukuiweka kwa bahati mbaya. Anyway, unaweza kuendelea maana JF huchangii kuwa member na hakuna qualification yoyote ili kujiunga. Lkn, ni Forum ya Great Thinkers, hivyo tafadhali isome post yako vizuri halafu uone kama kuna great thinking hapo. I am sorry..!

Nimesoma kwa makini maoni ya Mwanakijiji pamoja na maoni ya Slaa,Zitto,Lwetama n.k.Nilichokibaini cha msingi hapa ni kuwa Mwanakijiji ameanza kupata wasiwasi na mbinu inayotumiwa na CDM katika harakati za kushika dola.Kwa Mwanakijiji anaona kivuli cha CCM kinaanza kuongezeka hasa baada ya mkakati wa kujivua gamba ambao kimsingi unanafasi yake kubwa katika mabadiliko ya Chama.Hapa Mwanakijiji anaona CCM katika uvuaji gamba haikomei kwenye mabadiliko ya CC na Sekretarieti yake,bado inamikakati makini ya kimafia yenye kuhakikisha CDM inapotea katika masikio ya Wananchi.

Upande wa pili,Mwanakijiji anaitizama CDM kama chanzo cha kuipa nguvu CCM badala ya kuidhoofisha.Mwanakijiji anaitizama CDM mbali na kupuuza mabadiliko ndani ya CCM bali pia imekuwa msaada mkubwa kwa mabadiliko hayo.CDM hapa inashindwa kutambua ni wapi CCM inapaswa kutokomezwa?na ni silaa gani ya kuitokomeza CCM?.

Maoni ya DR. Xavier Lwetama ambayo yameonekana wazi kupinga maono ya Mwanakijiji inadhihirisha uvivu wa kufikiri alionao.Lwetama mbali na kuwa na focus ya kutamani CCM ife ata Leo lakini inaonyesha njia ya CCM kufa haioni zaidi ya kutanguliza chuki binafsi na wala si “ strategy”.Dr. Lwetama akiwa anajinadi kama Mwanachama mfu wa CCM ,hii pia inaongeza changamoto ya kutokukubalika kwa hoja yake kwani ni dhahiri anaonyesha ushabiki wake kisiasa ni katika mlengo wa “opportunistic”.Maoni yake ya kudai ushindani wa kimaadili (kutokutumia mbinu ya kudhoofishana) ila CCM ife hapa ndio njia na mbinu ya Lwetama inaposhindwa.CCM haiwezi kufa bila kudhoofika,ajali kwa binadamu ni sawa lakini si mfano wa CCM kufa kama ajali ya basi.

CDM imeonyesha ku-survive kwa makosa ya CCM,hii inamaana CCM ikijirekebisha kutokana na makosa yake CDM haipo.Mwanakijiji anapata wasiwasi kwani mwazoni CDM ilikuwa inampa nguvu na kuona kifo cha CCM kinakaribia sasa wasiwasi unatanda baada ya kuona CDM imempa kikombe CCM (adui) sasa karudi kazini na dhana za kummaliza mtoa kikombe.
Mwanakijiji hajakosea kwani anajua CCM si chama cha kawaida kama CDM inavyodhani.Anatambua na kusifu katika mada yake kuwa hawa ni watu wa siasa za Kisayansi na mbinu za kimafia kwa maana ya ubingwa wa kuuwa vyama pinzani.Ni kweli CCM inauwezo huo na kama CDM haitofikiri njia mbadala za kujiimalisha (kuachana na nyimbo za list of shame,remix etc.) ambazo CCM imeisha zirekodi kwa jina lake itakufa kabla ya 2015.

CCM haitanii na ndio kwanza safari imeanza na wanakwambia si nguvu ya soda.Kumbuka uzoefu wa CDM kisiasa ni mdogo kulinganisha na CCM hivyo na adui CCM ameishatambua silaa ilizonazo CDM sasa kilichobaki ni mchakato wa kukimaliza kisayansi.

Changamoto anayotoa Mwanakijiji kwa CDM ni kubwa kutokana na maswali haya.
Je!CDM watauweza mziki wa CCM?Je! CDM wanauwezo wa kucheza bila kusikiliza mziki wa CCM?.Ikumbukwe kuwa Watanzania watampigia kura Yule mwenye uwezo wa kumiliki Jukwaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom