Mkutano wa Kampeni za Udiwani wa CCM wilayani Mbulu zimeingia dosari baada ya wananchi kuwazomea kwa nguvu.
Zomeazomea hiyo ilianza tangu mwanzo lakini hali ilikuwa mbaya zaidi alipopanda Kada wa CCM aliyefukuzwa CHADEMA Mtela Mwampamba ambapo badala ya kutoa sera alianza kuwaporomoshea matusi ya nguoni CHADEMA na viongozi wake.Hali hiyo ililazimisha wananchi kupiga makelele na kumshusha kwa nguvu jukwaani kitendo alichotii Mwampamba kuepusha ghasia zaidi.
Mkutano huo ulikuwa unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba ambaye hata hivyo kwa kusoma upepo alishindwa kutoa matusi kwa CHADEMA kama ilivyo kawaida yake.
Nchemba alifuatana na kijana aliyemwagiwa tindikali Igunga na kusema ni kazi iliyofanywa na CHADEMA.Pia alidai yeye ndiye aliyeletewa Mkanda anaodai ni wa Ugaidi wa Lwakatare.
Kwa ujumla kulikuwa na watu wengi uwanjani lakini hata hivyo zaidi ya robo tatu ilikuja kuonekana ni wafuasi wa CHADEMA kutokana na mwitikio wao hali iliyomlazimu Mwigulu kushindwa kutumia Salaam ya CCM Hoyeee...badala yake ikabidi mara zote aseme Mbulu Hoyeee...!!!