Mtei akoleza moto wa Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtei akoleza moto wa Mnyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 20 June 2012

  [​IMG]
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akizungumza na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika katika viwanja vya bunge jana. Mnyika amerejea kuhudhuria vikao vya bunge baada ya juzi kutimuliwa bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai. Picha na Edwin Mjwahuzi

  Habari imeandikwa na Moses Mashalla, Arusha | Mwananchi


  MWASISI wa Chadema, Edwin Mtei amemtetea Mbunge wa Ubungo, John Myika kuwa alikuwa sahihi kusema kwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kwa kuwa kuna matukio mengi yaliyohitaji uamuzi wake na hakuutoa kwa wakati.

  Pia Mtei amelaumu Kanuni za Bunge zilizomwezesha Naibu Spika, Job Ndugai kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge mbunge huyo.

  Juzi, Mnyika alitolewa nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya kukukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu'.

  Akitetea kauli hiyo, Mtei alirejea baadhi ya matukio aliyodai yanaonyesha udhaifu huo, ukiwamo uamuzi ya Rais Kikwete juu ya hatua za kuwachukulia walioiba fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Mtei alifafanua kwamba, kitendo cha Rais Kikwete kuwataka wezi hao warudishe fedha walizoiba badala ya kuwakamata, kinadhihirisha udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo.

  "Rais Kikwete ana udhaifu wa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu taifa kwa ufisadi…udhaifu wa Rais ni kama kutowadhibiti wezi wa fedha zetu kama fedha za EPA. Aliwaambia wezi warudishe fedha, badala ya kuwatia ndani wanabaki wanatamba kwa kuiba fedha zetu," alisisitiza Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu.

  Alisema kibaya zaidi ni kwamba, nchi inayumba kutokana na uongozi mbovu kuanzia ngazi ya urais hadi chini, kwa kuwa tunaongozwa na watu wasiojua na kuisimamia Katiba.


  Kauli kuhusu Bajeti

  Akitoa maoni yake juu ya Bajeti ya Serikali ya mwaka huu, Mtei alisema Bajeti hiyo haina jipya kwa kuwa haishughulikii matatizo na kero za wananchi.

  Alisema Bajeti hiyo ambayo mjadala wake unahitimishwa kesho, haiwezi kukabilina na mfumuko wa bei unaolikabili taifa.

  Kuhusu suala la deni la Taifa linalofikia Sh20.2 trilioni, alisema nchi ipo njia panda, hali ambayo ni hatari kwa kuwa ni mzigo kwa taifa na linazidi kuongezeka kila mwaka.

  Mwanasiasa huyo ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, aliponda vitendo vya Serikali kukopa fedha kila mara kwenye mabenki ya kibiashara nchini, na kuomba kwa wahisani.
   
 2. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hakuna asiyetambua kama huyu bwana ni dhaifu na kila mtu anajua udhaifu wake ila ila mnyika ameonyesha uthubutu
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Mnyika ameonyesha uthubutu wake mapema ila wengine wote wakiwemo media watasema sana JK akimaliza muda wake hapo ndipo utasikia hata yasiyosemwa!!
   
 4. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi nzima inajua kuwa JK ni dhaifu na kuna mzungu mmoja katika gazeti fulani aliandika makala ambayo iliwekwa hapa jamvini akisema kuwa "JK is a global laughing stock" yaani hata watu wa nje wanalijua hilo. Magamba wote wanalijua hilo na wamshukuru sana Mh.Mnyika kuwasemea kwa sababu kwenye chama chao hakuna mwenye udhubutu.

  Kwa hiyo basi kama JK anataka kuondokana na fedheha hii hana budi kutimiza kile wananchi wanacho tarajia kutoka kwake. This guy is tired and he is not the man of action. Hivi sasa tunanyemelewa na mgomo wa madaktari, mtaona jinsi atakavyo ushughulikia kama siyo kupanda ndege na kukimbia.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  amesema kinachozungumzwa na wengi mitaani
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Huyu Mzee naye anazeeka vibaya, anasifu ujinga.
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 652
  Trophy Points: 280
  Kwani rais kazi yake ni kuwatia ndani wezi?
  Na hiyo bajeti ya upinzani ina tofauti gani na bajeti ya serikali?
   
 8. k

  kamalaika Senior Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni Tanzania tu ambapo wezi wanaambiwa warudishe hela walizoiba, na kusamehewa.Ni mfano gani tunawaonyesha watoto wetu?
   
 9. k

  kamalaika Senior Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa nini watu wanajulikana na hawachukuliwi hatua. There is more than what meets the eye
   
 10. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Yaani hivi nchi hii hakuna kanuni kama ile ya Bunge ya kumtoa nje ya nchi mtu kama huyu anayesema kuwa Raisi kikwete ni Dhaifu??????

  Mh. Lukuvi kwa nini na hapa usiombe Mwongozo wa Spika ili Bw. Mtei atolewe nje ya nchi, kwani hatuwezi kumtoa Bungeni kwa sababu siyo mbunge hivyo inabidi atolewe nje ya nchi kwa kutoa maneno yanayofanana na ya Mh. Mnyika.

  Lukuvi fanya kazi yako:  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 11. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280


  Hapa ina maana Mh. Lukuvi anamuomba jamaa kifaa cha CDM ili asiipinge tena bajeti. Kama kawaida yao magamba wanampa vitisho ili aogope.


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 12. u

  umsolopagaz Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jk ni raisi dhaifu kutokea ktk jamhuri ya muungano...lkn kutuletea taarifa ati kuna "mzungu" aliwahi kuandika kuwa raisi wetu ni loughing stock ya ulimwengu...that was too much frm mzungu...haijatokea na wala haitatokea tanzania yetu inayopata raisi wake kwa uchaguzi (mind u, chaguzi zetu zote tho r nt perfect, but thy r very, very credible..!)..ati kupata raisi ambaye ni loughing stock ya ulimwengu...that was too much, na ni tusi kwa watanzania(wapiga na wasiopiga kura)..hakuna cha kufurahiya ktk maoni ya mzungu wako..ila tu kwa vibaraka wa wazungu(na ni wengi sana siku hizi ktk kaumu ya "wahitimu" wetu)
   
 13. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,592
  Likes Received: 2,976
  Trophy Points: 280
  Kama budget ya upinzani ni nzuri au mbaya, hiyo si hoja na wala siyo sababu itakayomfanya JK aonekane ni kiongozi jasiri.

  Udhaifu wa JK ukianza kuorodheshwa itakuwa ni makala ndefu sana. Udhaifu wake zaidi upo katika vision, strategies, planning and supervision. Katika hivyo vyote ameonesha udhaifu mkubwa. JK ametufanya wote tushindwe kujua tunataka na tunajenga Taifa la namna gani. JK ni kiongozi ambaye anaongoza nchi kwa unafiki bila msimamo na ndiyo maana hata viongozi wa chini yake hawaelewi wafanye nini maana hawajui anataka nini, anatafuta kupendwa na wevi na wanaoibiwa, wachapa kazi na wavivu, wanaouchukia udini na wanaoupenda, wanaouchukia mwungano na wanaoupenda, wanaovunja sheria na wanaotaka utawala wa sheria, n.k. Kiongozi hustahili kuwa hivyo, ni lazima ueleweke unataka nini na unasimamia nini, na hiyo ndiyo huacha landmark yako katika Taifa.

  Viongozi wote makini Duniani hueleweka misimamo yao, haijalishi itakuwa mizuri au mibaya. Lakini huwezi kuwa kinyonga, mtu usiyeeleweka unataka nini na unasimamia nini. Unatamka kuwa unataka utawala wa sheria, lakini Magufuli akisema atabomoa nyumba za wale wote waliokiuka sheria ya barabara, unasema tena, ooh hapana usifanye hivyo. Wewe kweli ni kiongozi unayesimamia sheria? Tunasema wahujumu uchumi na mafisadi wapelekwe kwenye vyombo vya sheria, wewe tena unasema, tukipeleka wahujumu uchumi wote mahakamani uchumi utayumba. Huku unawaambia wananchi kuwa tumewapa meno TAKUKURU lakini nyuma ya pazia unawaambia wasiwapeleke watu fulani fulani (rejea taarifa za Weakleaks).

  Rais wetu hata kama tukitaka kumtetea namna gani, ukweli ni kuwa ni dhaifu sana, na anayependa kujipendekeza kwa kila mtu. Kiongozi hustahili kuwa hivyo, unatakiwa uwe na msimamo, na hapo ndipo utawatafuta wasaidizi wanaoendana na msimamo wako, nao watakuwa na ujasiri wa kusimamia ambayo wana uhakika ndiyo unachosimamia.
   
 14. Jaji

  Jaji Senior Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaposema rais ni strong hiyo ni sifa yake kutokana na vitu alivyovifanya. Pia unaposema ni dhaifu ni sifa yake kutokana na vitu alivyofanya. Acha ushabiki MTEI kafafanua hadi vitu vinavyofanya kiwete awe na sifa ya udhaifu.
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sikutegemea Mtei (chadema) angesema Ndugai (CCM) alikuwa sahihi kumtoa nje mnyika...... tutafute maoni ya wananchi ambao hawana itikadi za vyama vya siasa tutapata kilicho sahihi na bora.


  Hata kabla hajasema nilijua tu hiyo ndio ingekuwa kauli ya Mtei kama ataulizwa maoni yake juu ya bajeti na kutolewa nje bungeni kwa Mnyika..... maoni kutoka upande wa chama kimoja ni aghalabu yakatofautiana.
   
 16. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  1. Hapana, kazi ya rais ni kuwaambia wezi warudishe fedha walizoiba. Na anaweza kuifanya kwa ufanisi zaidi kwasababu amepewa mamalaka ya kuteua DPP ambaye anaweza kumwamuru asiwashitaki wezi,ili wasije "kutiwa ndani" kabla hawajarudisha fedha!
  2. Bajeti ya upinzani haina tofauti yeyote na ile ya serikali! Wanaongea-ongea tuu kwasababu ni "silly season" unajua tena. Kwa mfano mtu eti anazungumzia kupunguza kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima, kwani VX V8 lingekua si la lazima mjapani angehangaika kulitengeneza na akili yake yote?! Silly wapinzani!

  Yours are very insightful questions,kobello!
  :A S wink:
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,794
  Trophy Points: 280
  wewe ndio unazeeka vibaya kushindwa kujua kuwa kikwete ni dhaifu sana,najua hata ulio nao karibu wanajua hilo.
   
 18. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Tukiachana na mambo ya bajeti, mimi nataka wana JF wanifafanulie EPA ilihanzishwa kwa madhumuni gani?
   
 19. Pastor Achachanda

  Pastor Achachanda JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 3,011
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mh!Tupate wapi tena mtu kama Nyerere,mwenye uchungu sio kama JK yaani maisha magumu anasababisha yeye.Au amechoka kazi?
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,794
  Trophy Points: 280
  kama hujui mamlaka aliyonayoa rais si unyamaze kwan lazima uchangie?

  Sishangai wewe kutojuaa kikwete ni dhaifu sana,pamoja na kusoma hapo juu bado huelewi,we niaje?
   
Loading...