Kama budget ya upinzani ni nzuri au mbaya, hiyo si hoja na wala siyo sababu itakayomfanya JK aonekane ni kiongozi jasiri.
Udhaifu wa JK ukianza kuorodheshwa itakuwa ni makala ndefu sana. Udhaifu wake zaidi upo katika vision, strategies, planning and supervision. Katika hivyo vyote ameonesha udhaifu mkubwa. JK ametufanya wote tushindwe kujua tunataka na tunajenga Taifa la namna gani. JK ni kiongozi ambaye anaongoza nchi kwa unafiki bila msimamo na ndiyo maana hata viongozi wa chini yake hawaelewi wafanye nini maana hawajui anataka nini, anatafuta kupendwa na wevi na wanaoibiwa, wachapa kazi na wavivu, wanaouchukia udini na wanaoupenda, wanaouchukia mwungano na wanaoupenda, wanaovunja sheria na wanaotaka utawala wa sheria, n.k. Kiongozi hustahili kuwa hivyo, ni lazima ueleweke unataka nini na unasimamia nini, na hiyo ndiyo huacha landmark yako katika Taifa.
Viongozi wote makini Duniani hueleweka misimamo yao, haijalishi itakuwa mizuri au mibaya. Lakini huwezi kuwa kinyonga, mtu usiyeeleweka unataka nini na unasimamia nini. Unatamka kuwa unataka utawala wa sheria, lakini Magufuli akisema atabomoa nyumba za wale wote waliokiuka sheria ya barabara, unasema tena, ooh hapana usifanye hivyo. Wewe kweli ni kiongozi unayesimamia sheria? Tunasema wahujumu uchumi na mafisadi wapelekwe kwenye vyombo vya sheria, wewe tena unasema, tukipeleka wahujumu uchumi wote mahakamani uchumi utayumba. Huku unawaambia wananchi kuwa tumewapa meno TAKUKURU lakini nyuma ya pazia unawaambia wasiwapeleke watu fulani fulani (rejea taarifa za Weakleaks).
Rais wetu hata kama tukitaka kumtetea namna gani, ukweli ni kuwa ni dhaifu sana, na anayependa kujipendekeza kwa kila mtu. Kiongozi hustahili kuwa hivyo, unatakiwa uwe na msimamo, na hapo ndipo utawatafuta wasaidizi wanaoendana na msimamo wako, nao watakuwa na ujasiri wa kusimamia ambayo wana uhakika ndiyo unachosimamia.