FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,776
Leo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.
Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.
Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.
Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?
What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?
Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
Hiyo ni kawaida sana kwenye masuala ya kiuchumi.
Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa intelligence.
Nnafurahi sana kusikia Rais kuyasema hayo.
Hilo ni dongo kwa wale wanaosema "anakurupuka".
Hongera Magufuli, hivyo ndiyo sahihi, lazima upate information kutoka sehemu tofauti kwa miono tofauti ili ufanye maamuzi sahihi.
Ndiyo maana ulipomtunbua Anne Kilango nikasema yule mwanamke ni bogus kabisa kutokuelewa kuwa Rais anapokutuma kazi ana njia nyingi nyingine za kupata taarifa.
Mleta mada usiwe kama Anne Kilango. Tumia kichwa chako kufikiri japo kiduchu na usikiwache kuwa ni mzigo tu juu ya mabega yako.