Mtego wa Rais kwa CAG

denoo49

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
6,113
6,950
Leo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.

Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.

Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.

Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?

What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?

Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
 
Mkuu uliwazalo ndio lililokuwa kichwani mwanga pia, maana kuna siku kadhaa zilizopita, CAG aliwahi kusema kuna pesa zilitumika na serikali pasipo kibali cha bunge. Na hapa nafikiri ndio kama mwiba unaomuwasha Bob mpaka leo sasa anataka kupoozea machumgu kwa hilo agizo alilotoa mara ya pili kwa CAG.
 
CAG naye ni binadamu, na hii issue ni nyeti. Huko nyuma tuliona Ma CAG wakishambuliwa bungeni kwa kupindisha ukweli.

Kwa kuunda timu kadhaa, Rais anataka tu kujiridhisha na ukweli ..! Nafikiri ni strategy nzuri kwa kiongozi yeyote.
Inaweza kuwa mbinu nzuri, ila inategemea inatumika Je, na wakati gani?
Kwa hili mpaka kumuambia moja kwa moja kuwa kafanye hivi ila na mimi nitafanya hivi kujua nilichokuambia ukafanye kuona kama kipo sawa, sidhani kama ni sahihi. Kwanza unaonesha wazi pengine huna imani na ninachofanya au nifanye iwapo ikitokea nimekosea sehemu basi ndio itumike kama sehemu ya kunisemea.
 
Rais makini wakati wote huweka msisitizo kuonesha kazi hiyo ni muhimu. Hapa sio issue ya kuaminiana bali ni kulinda maslahi ya Taifa. Na kama CAG yupo tentative lazima atakwenda kufanya kazi bora zaidi. Mazoea ya kuaminiana ndiyo yamefanya nchi imekuwa na ulaji na walaji kila kona. Ni mjinga pekee anayeweza kuhoji ubora wa Rais tuliyenaye Tanzania kwasasa. Ukifuatilia kwa makini utaona wanaohoji ni wale waliokuwa kwenye mtandao wa kuifanyia maovu nchi yetu Tanzania. Either wapiga deals haramu au wauza unga. You are no more. Go to hell. Leave our country alone.
 
Mkuu kwanza amini kila kazi ifanyikayo kwaajili ya taifa ni muhimu, tatizo pengine linaweza kuja kwenye priority au strategy katika jambo husika. Je Rais akiamua kufanya au kijiaminisha katika kila kitu hapo kulikuwa kuna haja gani ya kuteua wasaidizi wake tena ambao amewaamini na kiwafanyia uchunguzi wa kujiridhisha?
Hata yeye aliaminiwa ndio maana akateuliwa kugombea mpaka kuchavuliwa, Je tuamini kwamba kwa baadhi ya makosa yanayotokea yanatokana na waliomuamini ndio maana katufikisha hapa?
Na daima mjinga ndio anayeuliza mkuu, na ni bora, kuliko yule mwelevu hasiuejua akaa kimya wakati hajui, huyu atakuwa hana tofauti na mpumbavu.
 
Ahsante sana kwa kunifungua macho kuhusu hilo la invisible team. Kwanini kuwepo na invisible team kwa kazi ambayo imeshakamilishwa na CAG!?

Huku si kuongeza gharama za uendeshaji za Serikali ambazo tuliambiwa zinapunguzwa!?

Hii invisible team inaleta wasiwasi mkubwa sana na nadhani dhumuni lake kubwa ni kumpinga CAG huku wakiendelea kufichwa nyuma ya pazia. HATARI!

Leo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.

Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.

Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.

Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?

What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?

Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
 
shida wabongo kila kitu tunatakaga eti tukiangalie kwa jicho la tatu pia kila kitu kukipa big picture... kwan ni lazima kila kitu mkichambue, mbona hili ni la kawaida.. yaani rais kutaka apate taarifa sahihi na iliyoshiba juu ya suala husika nalo ni tatizo? kuna haja gani sasa ya makampuni na taasisi kualeta external auditors kama tungekua tunaridhika na report za internal auditors! ujuaji mwiiingi na jicho lenu la tatu lililo na mtoto wa jicho, mnachosha bana
 
Kwa nn mnamsaidia kusema? Yeye ni binadamu hakuna asiye na mapungufu na km amechemka sehemu ni sawa pia its part of life. Hakuna rais amewahi kulalamikiwa km huyu kwa maamuzi yake yenye utata.

Back
Top Bottom