Mtego wa Rais kwa CAG

Mtego wa Rais kwa CAG

CAG hana mandate ya kukagua kampuni binafsi. Ni kutokuelewa tu kwa Mheshimiwa.
 
Leo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.

Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.

Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.

Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?

What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?

Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
Kichaa at work
 
Wanawake wenye payo namna hii, wana msongo wa mawazo sana. Zungumza na unayemuamini uliye nae karibu akusaidie kimawazo. Pole sana, yatakwisha.

Ha ha ha haaaaaaaaa

Usijaribu kuniambukiza matatizo yako, kaa na hayo uliyoyandika huko huko.
 
Leo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.

Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.

Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.

Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?

What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?

Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
siyo hivyo tu na Bunge 'ameliagiza' liunde tume ya uchunguzi! What a waste of resources?
 
Kwa nn mnamsaidia kusema? Yeye ni binadamu hakuna asiye na mapungufu na km amechemka sehemu ni sawa pia its part of life. Hakuna rais amewahi kulalamikiwa km huyu kwa maamuzi yake yenye utata.

Wanaolalamikia JPM ni wale wahuni. Tena sitaki hata kuwasikia. Walizoea kufanya Tanzania shamba la bibi. No more!
 
Mkuu kwanza amini kila kazi ifanyikayo kwaajili ya taifa ni muhimu, tatizo pengine linaweza kuja kwenye priority au strategy katika jambo husika. Je Rais akiamua kufanya au kijiaminisha katika kila kitu hapo kulikuwa kuna haja gani ya kuteua wasaidizi wake tena ambao amewaamini na kiwafanyia uchunguzi wa kujiridhisha?
Hata yeye aliaminiwa ndio maana akateuliwa kugombea mpaka kuchavuliwa, Je tuamini kwamba kwa baadhi ya makosa yanayotokea yanatokana na waliomuamini ndio maana katufikisha hapa?
Na daima mjinga ndio anayeuliza mkuu, na ni bora, kuliko yule mwelevu hasiuejua akaa kimya wakati hajui, huyu atakuwa hana tofauti na mpumbavu.

Rais anapanga mambo yake kwa kuondoa kabisa hali ya wahuni kuhonga wasaidizi wa Rais. Ni kwa njia hiyo tu ndipo tutaweza kupata matokeo chanyA+ kwasasa. Watanzania hawaaminiki tena. Hata mimi sitaki kuaminiwa muda huu. Ni mguu kwa mguu.
 
WA TANZANIA SIO MNACHANGIA PUMBA KWAKUA KILA MTU ANAWEZA CHANGIA. HILI NI SWALA NYETI SANA NA NI MASLAI YA TAIFA HATA ZIKIUNDWA TIMU 10 NISAWA MAANA HAPO KUNAUDANGANYIFU WA WAZI HATUWEZI JILIDHISHA NA MAJIBU YA TIMU MOJA. ANGEKUWA AAMINIKI ASINGE TUMWA. HATA MIMI NINGE KUWA RAIS NINGE FANYA HIVYOHIVYO. NA KUNA HAJA YA KUBORESHA KITENGO CHA INTEREGINCIA ILI KIWE NA VITENGO MBALIMBALI VYAKUWEZA PAMBANA NA MAMBO KAMA HAYA. DUNIA IMEBADILIKA TEKNOLOGIA IMEONGEZEKA NA HUALIFU UNAKUA TUSILALE HAKUNA MUDA WA MCHEZO TENA. WA TANZANIA TUACHE KUISHI KWA MAZOEA
 
Hakukuwa na haja ya kutangaza kuwa ataunda invisible team.
Hii itamfanya CAG asifanye kazi yake kwa uhuru na weledi.
Inamaana CAG atahongwa na hayo makampuni ya madini ili apindishe ukweli?
 
Kwa nini asiende mweyewe kukagua hiyo migodi,?
 
CAG naye ni binadamu, na hii issue ni nyeti. Huko nyuma tuliona Ma CAG wakishambuliwa bungeni kwa kupindisha ukweli.

Kwa kuunda timu kadhaa, Rais anataka tu kujiridhisha na ukweli ..! Nafikiri ni strategy nzuri kwa kiongozi yeyote.
Si alisema kwenye uongoz wake hamna mambo ya kuunda tume yeye ni maamuzi tu?.. wabongo tuache unafiki
 
Rais ameonyesha udhaifu mkubwa sana , hii INA maana kwamba hamwamini CAG
Haaminiki mtu hapa ili kujiridhisha lazima kuwa na vyombo zaidi ya kimoja,siku hizi kuna ujanja mwingi kutoka kwa hawa wataalamu,na nyie hamna zuri kila kitu ni kuloloma tu,yakitokea mabaya ni wa kwanza kulaumu kuwa oh mbona serikali haikufanya hivi na vile
 
Nimeangalia maelekezo ya JPM ni kama hamuamini mtu, anataman angewatuma hata malaika
 
Ukweli ni kuwa, watanzania wamekuwa waongo, wapigaji, wazandiki...

Ukitaka kujua hilo pita kwenye viwanja vikubwa vya ndege duniani, wakiona pasi yako ya kusafiria ndio utajua raha ya kuitwa mtanzania miaka hii.

Ngoja tu aunde hata timu kumi, hatiaminiki tena. Sasa kama hata wabunge, wawakilishi wetu tuliowachagua, wakiwa kwenye kamati za bunge wanapewa mlungula ili tu kuzima baadhi ya madudu ya haya mashirika yetu, unadhani kuna wa kuaminika tena...
 
Back
Top Bottom