Sabung'ori
JF-Expert Member
- Jul 19, 2011
- 2,166
- 1,248
…kama wewe mwenyewe haujiamini ni vigumu sana kuwaamini wengine…
Hujajibu suala la Magufuli kuingilia sehemuambazo hatakiwi kuingilia.Naam, wakati watu wanalia vitanda hamna mahospitalini wewe unafanya sherehe ya mamilioni? Inaingia akilini hiyo?
Kuhusu mzee wa upako, ni safi sana. Hebu soma hiki kipande "...wenye mahitaji ya kuabudu waabudu...".
Ukitaka "context" ya hicho kipande, pitia hapa: Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
Hujajibu suala la Magufuli kuingilia sehemuambazo hatakiwi kuingilia.
Rais anatakiwa sio tu kufanya vitu vizuri (kusaidia hospitali ipate vitanda ni kitu kizuri) lakini pia anatakiwa kufanya vitu vizuri kwa njia nzuri (kuliamrisha bunge kusaidia hospitali kunakiuka misingi ya separation of powers, na hivyo si kitu kizuri).
Magufuli hana weledi wa kujua hilo, ama hajali.
Kaingilia ovyo ovyo kote huko nilikokutaja, kama nchi haina misingi ya uongozi.
Hilo haliteteeki.
Sasa ikiwa ripoti zitatofautiana; ataiamini ripoti ipi na ataiamini kwa kutumia vigezo gani?!! Kama miongoni mwa wale atakaowatuma; anamuamini mmoja wapo; kwanini hiyo kazi asimpe huyo huyo?!!!CAG naye ni binadamu, na hii issue ni nyeti. Huko nyuma tuliona Ma CAG wakishambuliwa bungeni kwa kupindisha ukweli.
Kwa kuunda timu kadhaa, Rais anataka tu kujiridhisha na ukweli ..! Nafikiri ni strategy nzuri kwa kiongozi yeyote.
kLeo katika kufatilia taarifa ya habari katika kituo kimoja cha television hapa nyumbani, imeonesha Mkaguzi Mkuu wa hesabu wa Serikali amekabidhi ripoti yake kwa Mh. Rais ikulu.
Katika makabidhiano hayo, Rais ameenda mbali zaidi na kumpa kazi nyingingine, "akimtaka" Mkaguzi huyo akakague migodi ya madini na aje na ripoti ya kuonesha taifa/serikali ina nufaika vipi na mchanga unaosafirishwa kwenda nje.
Mbali na kumuagiza huko, Rais kasema kwamba, ataunda tume nyingine ichunguze suala hili hilo, na ataunda "timu" nyingine hisiyojulikana (invisible team) kuchunguza jambo hilo hilo pia.
Sasa hapa najiuliza, kuna ulazima gani tena Rais aunde tume na invisible team, wakati ameishamwagiza CAG kufanya jambo hilo?
What if, kama hiyo tume na team zikaja na majibu tofauti na ya CAG?
Je Kazi anayofanya CAG haiaminiki kwa serikali au Rais ndio hana imani na CAG?
Hao wabunge wa Tanzania hata wakijua zaidi yangu wamefungwa na mfumo wa kifashisti unaowafanya wamuabudu mtu mmoja hata kama anapeleka nchi kuanguka katika korongo.Wewe unajuwa zaidi ya wabunge wote?