VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya liliofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?
Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzanzi Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?
Usalama wa Taifa ni watuhumiwa nambari moja wa sakata la Dr.Ulli.Lazima walihusika kupeleleza na kulikamata 'Jambazi la kikenya'...Hebu tufafanulie kidogo mkuu, hapo Usalama wa Taifa wanahusika vipi?
Endelea na zako. Ntakuja kukuuliza hapo unapofanyia kazi baadaye...Sioni hoja ya msingi hapo. Thread yako si ya kufikirika.
Waandishi wa habari wamfuate huko huko ,kama wale waandishi wa Kimataifa wanaweza kuifanya kazi hiyo ,au hata madaktari wanaweza kumfanyia mazungumzo na kuhusisha masuali mazito kwake ,kama anawafahamu waliomteka ,kuwataja majina kiasi ya kuelezea kisa kizima kwa yale anayoyakumbuka na kuwa yenye usaili wa kideo sio audio.
Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?
Hebu tufafanulie kidogo mkuu, hapo Usalama wa Taifa wanahusika vipi?