Mtazamo: Upinzani Bungeni kwaheri?

Mtazamo: Upinzani Bungeni kwaheri?

Kama umefatilia vizuri, nidhahiri nia ya chama tawala ni kuchukua viti vyote vya ubunge nchini.

Fatilia uzuiaji wa mikutano kwa Wapinzani kwa miaka mitano, vyombo vya habari kufungwa midomo na kuanza kus-support chama tawala, kauli za utata za NEC, wakurugenzi kupigwa mkwara endapo watatangaza wapinzani na ilihali yeye kawateua, kesi ya kupinga wakurugenzi kusimamia uchaguzi kupingwa chini, vioja vya kusimamishwa na NEC, polisi kuvuruga mikutano ya upinzani bila kusahau matukio ya leo ya kura.

Usisahau kuna wabunge 28 wamepita bila kupingwa tayari.

Hofu yangu kuna uwezekano kipindi hiki wabunge wa upinzani wasifike hata kumi kama sio watano, ngoja tuone mchezo.
Muhimu amani tu msisahau kama wote tupo kwenye jahazi moya likizama tumezama wote na likavuka tumevuka wote
 
Huu si uchaguzi bali ni maigizo ya NECCCM Tumeccm kumpachika Mkoloni kaburu mweusi ikulu kwa njia haramu za kishetani
Mzee bado una nguvu za kuzungumza tuu mimi nilifikiria umebakiza za kusukumia go..go tuu, wenzio wanalia huko mlidhania uchaguzi ni sawa na kucheza rede?

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Wapinzani wametendewa sivyo ndivyo..
Nilisema awali pasina tume huru ya uchaguzi siharibu muda wangu kushiriki "uchafuzi" matokeo haya yalijulikana awali na hakuna pa kuyahoji. Nadhani shinikizo la kimahakama iwe iwavyo laweza kusaidia kupiga hatua kupinga upuuzi huu.
 
Back
Top Bottom