Payson
Member
- Oct 28, 2020
- 35
- 16
Kama umefatilia vizuri, nidhahiri nia ya chama tawala ni kuchukua viti vyote vya ubunge nchini.
Fatilia uzuiaji wa mikutano kwa Wapinzani kwa miaka mitano, vyombo vya habari kufungwa midomo na kuanza kus-support chama tawala, kauli za utata za NEC, wakurugenzi kupigwa mkwara endapo watatangaza wapinzani na ilihali yeye kawateua, kesi ya kupinga wakurugenzi kusimamia uchaguzi kupingwa chini, vioja vya kusimamishwa na NEC, polisi kuvuruga mikutano ya upinzani bila kusahau matukio ya leo ya kura.
Usisahau kuna wabunge 28 wamepita bila kupingwa tayari.
Hofu yangu kuna uwezekano kipindi hiki wabunge wa upinzani wasifike hata kumi kama sio watano, ngoja tuone mchezo.