Mtazamo mpya wa dunia kuhusu Corona ni kuwa dunia imefikia breaking point; vizuizi vitaondolewa, watakaokufa watakufa, watakaopona watapona

Watetea lockdown mna shida kweli,!

Sikia bwana mdogo, duniani huko wameonaa lockdown ni upuuzi ndio maana leo wanaondoa, watu wanarudi makazini pamoja na visa vya mambukizi kuripotiwa kila siku...
Huyu haelewi athari za muda mrefu lockdown kwa uchumi duniani. Watu wamesaamua haiwezekani kuendelea ku-lockdown. Watu wataishije? Shughuli duniani zitafanywaje? Wameshaamua kwamba it is inevitable watu wengi watakufa, lakini sasa maisha yataendelea kwa wanaobaki

Halafu Trump anaona kama hizi lockdown zinawanufaisha China peke yao kiuchumi, na wanazidi kumkaribia USA kwa economic strength baada ya kumpita Japan. Hilo USA hawawezi kulikubali hata siku moja, wako tayari kufanya lolote kwa China ili wa-maintain position yao ya kwanza kama biggest world economy. Hii G-5 tu ya mawasiliano USA wamewafanyizia China ili kuwstop hadi wakaweza kufanikisha ya kwao!
 
Mkuu watu watakufa ndio na hakuna jinsi, lakini sio lazima awe Raisi wa Tanzania atakaekufa😅
So tutegemee ataendelea kuwa Chato kwa miezi mingi zaidi?Arudi ikulu kupiga kazi ili aache natural selection ifanye kazi yake!
 
Imeonekana kwamba lockdown ya Corona inasababisha athari kubwa sana za kiuchumi duniani. Watu wanapoteza kazi, kampuni zinakufa, serikali zinakosa mapato nk. Ni dhahiri sasa kwamba lockdown zinatikisa hata mataifa makubwa kama Marekani kiuchumi - na ndio maana hata Tanzania imeepuka sana kuweka lockdown.

Matarajio ya mataifa mengi ilikuwa kwamba lockdown zingedumu kwa muda usiozidi miezi miwili na corona ingekwisha. Lakini haijawa hivyo. Sasa imeonekana haiwezekani kuendelea na lockdown isiyo na kikomo. Japo watu wa uchumi wanakuambia nchi haiwezi kufilisika, lakini lockdown inaweza kuifilisi nchi, na mataifa yameamua kuzuia hilo lisitokee.

Mataifa yameamua liwe liwalo. Kwamba kuwe na Corona au kusiwepo, lockdown ziondolewe ili kunusuru dunia na muanguko mkubwa wa uchumi. Hata watu wamesema kwamba ikiwa homa ya Hispania (Spanish Flu au Influenza) ya mwaka 1918 iliua watu karibu milioni 20 duniani na bado dunia ikaendelea, kwa nini tunafikiri corona itaangamiza watu wote duniani? Watu hawaelewi kwa nini dunia nzima ina panick kwa vifo ambavyo wala havijafika hata 500,000 duniani, wakati mafua ya Hispania yaliua watu milioni 20 duniani na bado dunia ili-survive.

Kwa hiyo basi, ni kwamba lockdown zitaondolewa. Si kwamba hakutakuwa na tahadhari, la. Watu wataendelea kuhimizwa kujikinga na Corona. Pia kutawekwa utaratibu wa maisha tukiwa na Corona ili kupunguza maambukizi lakini maisha yataendelea kama kawaida. Kwa mfano, utaratibu unafanywa jinsi ambavyo watu wataendelea kusafiri katika ndege kwa kuhakikisha hewa inachujwa kwa namna fulani na abiria wanapewa mask. Katika shughuli zote ni kwamba, maamuzi yanatolewa sasa katika msingi kwamba watakaokufa hatuna la kufanya na watakaopona basi ni vema kwao.

Kuna watu hata wameonyesha kwamba suala la watu kufa kama nzige wanaopuliziwa dawa katika kipindi hiki haliepukiki, na hata liko katika vitabu vya unabii kama Ufunuo. Kwa hiyo imeonwa kwamba hata dunia ifanyeje, hili halizuiliki. WHO imeshasema kuna uwezekano mkubwa Corona itaendelea kuwapo na tukubali hilo. Wengine wanasema vifo vingi kama hivi ni mzunguko wa kawaida katika dunia katika suala la kubalance mambo, kwamba kwa sasa idadi ya watu duniani ni bilioni 7.6, hivyo hata watu bilioni 2 wakifa sio tatizo, hatutakwisha wote!

Kwa sasa juhudi kubwa zinafanywa kutafuta chanjo, lakini hadi itakapopatikana, mtazamo ni kwamba watakaokufa watakufa na watakaopona watapona, lakini dunia itaendelea kuwa na watu kama ilivyokuwa kwenye tatizo la homa ya Hispania.

It is every man for himself now!

Huo ni msimamo wa Magufuli wala si serikali wala CCM achilia mbali dunia.

Dunia unaijua? Unayoiongelea hata china wamo? Na hawa je?

How Australia and New Zealand are emerging from the coronavirus crisis
 
Bila source ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada mmurua kabisa hii ila msichukulie kupunguza idadi ya watu masikini duniani itapelekea wengi kufa hasa Afrika hii ni uongo na haiwezi kuwa hivyo.

Uzuri au Ubaya wa corona inamchapa binadamu yeyote yule na ndiyo maana ukipata evidence za wanaokufa utaona watu wenye kipato cha chini ni wachache sana wanaokufa.

Kwa upande wa lockdown naweza kumpongeza JPM kwa ushauri mzuri aliopewa kwa watanzania maana soon ataonekana shujaa japo ni vigumu kuja kumkubali maana atatafutiwa penye udhaifu.
Mkuu upo sahii
 
Wewe muongo sana,wewe unafikiri caranteen au lockdown zimeanza leo?
Hivi hujawahi kusikia kwamba tokea zamani yalipotokea magonjwa hatari kama ndui,hiyo sehemu ilitengwa hadi pale ugonjwa ulipodhibitiwa.
Wewe una uhakika gani law of the jungle yaani survival for the fittest ndio solution?
Uoni kusafiri wa ndege labda hujapanda ndege ya masafa marefu,unaposema wasafiri wavae masks kwa muda wote wakiwa angani je wakati wa kula hawatavua barakoa?
Uoni social distancing katika ndege kwa kipindi kirefu itakuwa gharama kubwa kwa owners,kwamba ndege itabeba theruthi ya wasafiri itakayopelekea watu wengi kushindwa gharama za kusafiri na ndege?
Je mkishajichanga kila mahali si ndio mwanzo wa kuwa na intermediate lockdown na caranteen kwa kipindi kirefu.
Kwa Afrika mashariki kwa pammoja na kwenye nia mmoja tungefunga real lockdown kama Uganda ya Museveni kwa siku 15 hadi 20 huo ugonjwa ungetokomea kabisa,kuliko haya maigizo ya kupoteza muda.
Unaposhindws ku solve equation simply you dont know,usiseme ni impossible wape wengine wakuonyeshe njia.
Kwa taarifa yako wewe uliyepanda ndege. Usiwe unakurupuka kuita watu waongo wakati wewe ndio hujui kinachoendelea
1589468585151.png

1589468079204.png

1589469073171.png
 
Kila MTU atakufa , usitake kumuombea mabaya raisi wetu.
Cha msingi tuendelee kumuomba mungu atuepushe na balaa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Balaa lipo tu, uombe usiombe

Revelation 6:7-8; When he opened the fourth seal, I heard the voice of the fourth living creature say, “Come!” 8 And I looked, and behold, a pale horse! And its rider's name was Death, and Hades followed him. And they were given authority over a fourth of the earth, to kill with sword and with famine and with pestilence and by wild beasts of the earth.

Kulingana na Revelation, 25% ya watu duniani wanakufa = watu karibu bilioni 2!
 
Back
Top Bottom