Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Imeonekana kwamba lockdown ya Corona inasababisha athari kubwa sana za kiuchumi duniani. Watu wanapoteza kazi, kampuni zinakufa, serikali zinakosa mapato nk. Ni dhahiri sasa kwamba lockdown zinatikisa hata mataifa makubwa kama Marekani kiuchumi - na ndio maana hata Tanzania imeepuka sana kuweka lockdown.
Matarajio ya mataifa mengi ilikuwa kwamba lockdown zingedumu kwa muda usiozidi miezi miwili na corona ingekwisha. Lakini haijawa hivyo. Sasa imeonekana haiwezekani kuendelea na lockdown isiyo na kikomo. Japo watu wa uchumi wanakuambia nchi haiwezi kufilisika, lakini lockdown inaweza kuifilisi nchi, na mataifa yameamua kuzuia hilo lisitokee.
Mataifa yameamua liwe liwalo. Kwamba kuwe na Corona au kusiwepo, lockdown ziondolewe ili kunusuru dunia na muanguko mkubwa wa uchumi. Hata watu wamesema kwamba ikiwa homa ya Hispania (Spanish Flu au Influenza) ya mwaka 1918 iliua watu karibu milioni 20 duniani na bado dunia ikaendelea, kwa nini tunafikiri corona itaangamiza watu wote duniani? Watu hawaelewi kwa nini dunia nzima ina panick kwa vifo ambavyo wala havijafika hata 500,000 duniani, wakati mafua ya Hispania yaliua watu milioni 20 duniani na bado dunia ili-survive.
Kwa hiyo basi, ni kwamba lockdown zitaondolewa. Si kwamba hakutakuwa na tahadhari, la. Watu wataendelea kuhimizwa kujikinga na Corona. Pia kutawekwa utaratibu wa maisha tukiwa na Corona ili kupunguza maambukizi lakini maisha yataendelea kama kawaida. Kwa mfano, utaratibu unafanywa jinsi ambavyo watu wataendelea kusafiri katika ndege kwa kuhakikisha hewa inachujwa kwa namna fulani na abiria wanapewa mask. Katika shughuli zote ni kwamba, maamuzi yanatolewa sasa katika msingi kwamba watakaokufa hatuna la kufanya na watakaopona basi ni vema kwao.
Kuna watu hata wameonyesha kwamba suala la watu kufa kama nzige wanaopuliziwa dawa katika kipindi hiki haliepukiki, na hata liko katika vitabu vya unabii kama Ufunuo. Kwa hiyo imeonwa kwamba hata dunia ifanyeje, hili halizuiliki. WHO imeshasema kuna uwezekano mkubwa Corona itaendelea kuwapo na tukubali hilo. Wengine wanasema vifo vingi kama hivi ni mzunguko wa kawaida katika dunia katika suala la kubalance mambo, kwamba kwa sasa idadi ya watu duniani ni bilioni 7.6, hivyo hata watu bilioni 2 wakifa sio tatizo, hatutakwisha wote!
Kwa sasa juhudi kubwa zinafanywa kutafuta chanjo, lakini hadi itakapopatikana, mtazamo ni kwamba watakaokufa watakufa na watakaopona watapona, lakini dunia itaendelea kuwa na watu kama ilivyokuwa kwenye tatizo la homa ya Hispania.
It is every man for himself now!