Mtazamo mpya wa dunia kuhusu Corona ni kuwa dunia imefikia breaking point; vizuizi vitaondolewa, watakaokufa watakufa, watakaopona watapona

Kwa sasa dunia imetopea kwa maovu ya kila namna hadi mengine hayaelezeki, mfano, wanaume kuoana na kuingiliana wao kwa wao, chuki, fitina, majungu, mauaji, dhuluma, ushirikina, uchawi, ulozi, roho mbaya, husda, tamaa mbaya, uasherati, wizi, ufisadi, kutomwabudu Mungu nk. nk. Sasa utaona ni kitu gani korona inajaribu kufanya.....kuisafisha dunia kutokana na uovu na watenda maovu, matukio yaliyoelezwa kwenye kitabu cha ufunuo kama alivyoeleza mdau hapo juu yameshaanza ni swala la muda, kufumba na kufumbua dunia inaweza kuingia katika hali mbaya sana ya machafuko.....kitu cha muhimu ni kuwa waangalifu tusije kuangamia na watenda maovu.
 
Kwa sasa dunia imetopea kwa maovu ya kila namna hadi mengine hayaelezeki, mfano, wanaume kuoana na kuingiliana wao kwa wao, chuki, fitina, majungu, mauaji, dhuluma, ushirikina, uchawi, ulozi, roho mbaya, husda, tamaa mbaya, uasherati, wizi, ufisadi, kutomwabudu Mungu nk. nk. Sasa utaona ni kitu gani korona inajaribu kufanya.....kuisafisha dunia kutokana na uovu na watenda maovu, matukio yaliyoelezwa kwenye kitabu cha ufunuo kama alivyoeleza mdau hapo juu yameshaanza ni swala la muda, kufumba na kufumbua dunia inaweza kuingia katika hali mbaya sana ya machafuko.....kitu cha muhimu ni kuwa waangalifu tusije kuangamia na watenda maovu.
Mmmh! Lakini Mkuu, Corona inaua hata walio wema na wasio mashoga! Sasa sijui hapo utasemaje.
 
Wewe una wazimu
Umejiona eeh, usivyo na maana! Umeumbuka sana na point zako zisizo na mshiko. Eti sijapanda ndege watu wakivaa mask kwenye ndege watakulaje. Unawaza kula tu saa zote! Ulifurahia sana chakula cha kwenye ndege eeh!

Halafu mie sio ligi yako kwenye kupanda ndege - angalia hizi link

Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!


Tumepanda Airbus 380 kwa ngazi!


Wakuu nilikuwa Ujerumani ikabidi tupandishwe Airbus 380, ile ndege ya double decker kwa ngazi. Nadhani kulikuwa nahitilafu kwenye zile bridges za kupandia

View attachment 69442
 
Mmmh! Lakini Mkuu, Corona inaua hata walio wema na wasio mashoga! Sasa sijui hapo utasemaje.
Mkuu watu wema wewe unawatambua? imeandikwa hakuna atendaye mema kwenye hii dunia, wote wametenda dhambi......sema rehema au tuseme neema inafanya kazi kwa baadhi ya watu..
 
Hahaha! Mkuu hiyo point inasemwa sana, kwamba ni Corona ni natural control measure kupunguza idadi ya watu na kurekebisha uhalibifu wa mazingira duniani ambao umefikia hatua mbaya (critical point)! Na wapo wanaodai ni suluhisho kupunguza umasikini katika nchi za Afrika!
Hapo kwenye sentensi ya mwisho fafanua kidogo mkuu maana weupe ndio wako hoi halafu inakuaje afrika inufaike na hilo
 
Umejiona eeh, usivyo na maana! Umeumbuka sana na point zako zisizo na mshiko. Eti sijapanda ndege watu wakivaa mask kwenye ndege watakulaje. Unawaza kula tu saa zote! Ulifurahia sana chakula cha kwenye ndege eeh!

Halafu mie sio ligi yako kwenye kupanda ndege - angalia hizi link

Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!


Tumepanda Airbus 380 kwa ngazi!
Wewe tatizo lako your reading a different page.Hata hiyo unayoisoma unashindwa kuchuja pumba na scintific evidence based facts
 
Hapo kwenye sentensi ya mwisho fafanua kidogo mkuu maana weupe ndio wako hoi halafu inakuaje afrika inufaike na hilo
Assumption ni kwamba Africa na nchi masikini kwa ujumla, huduma zetu za afya ziko chini sana, na mijini tunabanana mno. Katika nyumba (household) tunajazana mno. Nyumba moja inayokaliwa na watu wanne au watano ulaya sie kwetu tunafika hadi ishirini. Ukienda mjini, city centres, watu wamejaazana kama kumbikumbi - na hii ni kweli city centres za ulaya haziko crowded

Kwa hiyo ilitazwamiwa kwamba Corona virus ikitugonga tutakufa mno na idadi ya watu katika nchi zetu kupungua. Hivyo matumizi ya serikali kwa huduma za jamii, kama maji, hospitali, chakula nk, yangepingua na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo badala ya kuhudumia watu
 
Wewe tatizo lako your reading a different page.Hata hiyo unayoisoma unashindwa kuchuja pumba na scintific evidence based facts
Okay. Labda tatizo ni kwamba ulianza kwa kusema wewe muongo, hujapanda ndege. The rest sikuona tena.
 
Mkuu watu wema wewe unawatambua? imeandikwa hakuna atendaye mema kwenye hii dunia, wote wametenda dhambi......sema rehema au tuseme neema inafanya kazi kwa baadhi ya watu..
Mkuu, tofautisha kati ya dhambi za matendo, maneno na mawazo na dhambi ya asili.Japo hakuna anaeweza kusema hatendi dhambi, dunia hii ina mashahidi wengi wa wanaotenda mema - righteous people.
 
Mwanzo kabisa nilijua ugonjwa huu utaisha kabla ya mwisho wa mwezi May,niliwafariji marafiki zangu na ninaofanya nai kazi nikiwaamisha kwamba tuatarejea makazini mapema ila kwa sasa naona hali haipo hivyo,tahadhari dah.
WHO hawana suluhisho,WHO wamekata tamaa,hawasemi njia mbadala ya kuzima gonjwa hili.
 
Una flying hours ngapi?
Flying hours ni ma-pilot. Mie sio pilot. Lets just say kwenye frequent flier programme niliyonayo niko level ya Platinum. Na sasa hatujui kama airline itatushusha kwa kuwa mwaka there was litle travelling na sio kosa letu, tatizo la Corona limezuia ku-maintain status zetu.
 
Dunia itamuomba radhi Rais Magufuli.

Magufuli amewashangaza wanadunia kwa msimamo wake.

Watu watagundua kuwa kumbe tunaweza kuishi kwa tahadhari dhidi ya ugonjwa kuliko kukaa ndani tukisubiri ugonjwa uishe.

Magufuli katika hii vita amekuwa mshindi namba moja duniani.

Alikaa kimya sana,hakuwa anaongea ongea lakini alikuwa akiangalia namna gani afanye ili kunusuru uchumi na watu wake shughuli ziende.

Nampongeza sana magufuli katika hii vita,kujificha ndani ni sawa na kumkimbia adui vitani na upo uwanjani,ingia uwanjani chukua tahadhari.

Sidhani kama mtu akidumu na barakoa yake na akavaa gloves na akazingatia umbali baina ya mtu na mtu ati ataambukizwa ama tutaambukizana kwa kasi.

Muhimu tahadhari.
 
Huu ugonjwa ulitengenezwa kuua wagonja sugu na hawafi,

Mfano kama una ngoma ukupitie ili kubalance na kupunguza wagonjwa duniani wa maradhi mbalimbali.

Naunga hoja mweshimiwa mwenyekiti.

Sent using ubishi.com
 
Imeonekana kwamba lockdown ya Corona inasababisha athari kubwa sana za kiuchumi duniani. Watu wanapoteza kazi, kampuni zinakufa, serikali zinakosa mapato nk. Ni dhahiri sasa kwamba lockdown zinatikisa hata mataifa makubwa kama Marekani kiuchumi - na ndio maana hata Tanzania imeepuka sana kuweka lockdown.

Matarajio ya mataifa mengi ilikuwa kwamba lockdown zingedumu kwa muda usiozidi miezi miwili na corona ingekwisha. Lakini haijawa hivyo. Sasa imeonekana haiwezekani kuendelea na lockdown isiyo na kikomo. Japo watu wa uchumi wanakuambia nchi haiwezi kufilisika, lakini lockdown inaweza kuifilisi nchi, na mataifa yameamua kuzuia hilo lisitokee.

Mataifa yameamua liwe liwalo. Kwamba kuwe na Corona au kusiwepo, lockdown ziondolewe ili kunusuru dunia na muanguko mkubwa wa uchumi. Hata watu wamesema kwamba ikiwa homa ya Hispania (Spanish Flu au Influenza) ya mwaka 1918 iliua watu karibu milioni 20 duniani na bado dunia ikaendelea, kwa nini tunafikiri corona itaangamiza watu wote duniani? Watu hawaelewi kwa nini dunia nzima ina panick kwa vifo ambavyo wala havijafika hata 500,000 duniani, wakati mafua ya Hispania yaliua watu milioni 20 duniani na bado dunia ili-survive.

Kwa hiyo basi, ni kwamba lockdown zitaondolewa. Si kwamba hakutakuwa na tahadhari, la. Watu wataendelea kuhimizwa kujikinga na Corona. Pia kutawekwa utaratibu wa maisha tukiwa na Corona ili kupunguza maambukizi lakini maisha yataendelea kama kawaida. Kwa mfano, utaratibu unafanywa jinsi ambavyo watu wataendelea kusafiri katika ndege kwa kuhakikisha hewa inachujwa kwa namna fulani na abiria wanapewa mask. Katika shughuli zote ni kwamba, maamuzi yanatolewa sasa katika msingi kwamba watakaokufa hatuna la kufanya na watakaopona basi ni vema kwao.

Kuna watu hata wameonyesha kwamba suala la watu kufa kama nzige wanaopuliziwa dawa katika kipindi hiki haliepukiki, na hata liko katika vitabu vya unabii kama Ufunuo. Kwa hiyo imeonwa kwamba hata dunia ifanyeje, hili halizuiliki. WHO imeshasema kuna uwezekano mkubwa Corona itaendelea kuwapo na tukubali hilo. Wengine wanasema vifo vingi kama hivi ni mzunguko wa kawaida katika dunia katika suala la kubalance mambo, kwamba kwa sasa idadi ya watu duniani ni bilioni 7.6, hivyo hata watu bilioni 2 wakifa sio tatizo, hatutakwisha wote!

Kwa sasa juhudi kubwa zinafanywa kutafuta chanjo, lakini hadi itakapopatikana, mtazamo ni kwamba watakaokufa watakufa na watakaopona watapona, lakini dunia itaendelea kuwa na watu kama ilivyokuwa kwenye tatizo la homa ya Hispania.

It is every man for himself now!

Mumiani wana roho ngumu sana labda kuliko roho za paka.

Ngoja tusubirie pigo la 10.

Uliyoyaandika hapa yana apply Uganda, Rwanda au hata Kenya? Je china, UK, USA, italy, Germany, Spain, Australia, New Zealand nk?

Msitake kutuhalalishia vifo mumiani nyie.
 
Wewe muongo sana,wewe unafikiri caranteen au lockdown zimeanza leo?
Hivi hujawahi kusikia kwamba tokea zamani yalipotokea magonjwa hatari kama ndui,hiyo sehemu ilitengwa hadi pale ugonjwa ulipodhibitiwa.

Wewe una uhakika gani law of the jungle yaani survival for the fittest ndio solution?
Uoni kusafiri wa ndege labda hujapanda ndege ya masafa marefu,unaposema wasafiri wavae masks kwa muda wote wakiwa angani je wakati wa kula hawatavua barakoa?

Uoni social distancing katika ndege kwa kipindi kirefu itakuwa gharama kubwa kwa owners,kwamba ndege itabeba theruthi ya wasafiri itakayopelekea watu wengi kushindwa gharama za kusafiri na ndege?

Je, mkishajichanga kila mahali si ndio mwanzo wa kuwa na intermediate lockdown na caranteen kwa kipindi kirefu.

Kwa Afrika mashariki kwa pammoja na kwenye nia mmoja tungefunga real lockdown kama Uganda ya Museveni kwa siku 15 hadi 20 huo ugonjwa ungetokomea kabisa,kuliko haya maigizo ya kupoteza muda.

Unaposhindws ku solve equation simply you dont know,usiseme ni impossible wape wengine wakuonyeshe njia.
kwa hiyo Uganda ugonjwa umeisha wote?
 
Back
Top Bottom