Nilichokiona mimi huku kanda yetu ya ziwa ni dhahili Lowasa ameshindwa kwa haki na hajaibiwa kura yoyote,CDM ktk kipindi kijacho wajitahidi sana kuondoa uongozi wenye vinasaba vya ukanda mmoja,lakini pia kama wapinzani wawe wanaangalia na kauli za kuwaaminisha watanzania alafu baada ya muda wanageuka tena na kwa jambo lile lile na kulisafisha,hapo nazungumzia kauli walizozitoa za ufisadi wa EL na kisha kuja kumsafisha tena,kuna watanzania siyo waongeaji ila wanajua kupima mambo na wanaamua kupitia sanduku la kura.swala la ukanda liwepo au lisiwepo lakini limeleta madhara makubwa kwao kwa sababu mimi binafsi nilikua nasikia kauli nyingi kwa watu vijiweni hapa Mwanza kua na sisi tutampigia kura wa kwetu kanda yetu,hili jambo ni baya hapa Tanzania likipamba moto,ikumbukwe kwamba kanda ya ziwa ina watu wengi sana na wakiamua kupiga kura kwa wingi juu ya chama fulani lazima chama hcho kitoboe,lakini pia jambo hli tukubali lina ukweli ndani yake na liepukwe,jaribu kufikili ukiitamka CCM pamoja na mabaya yake lakini huwezi ona CCM ni ya wapi kwa maana ya ukanda,utaiona CCM pote Tanzania,lakini ukiitamka CDM katika masikio ya watu na ufahamu wao wanaiona picha ya ukanda wa Arusha na Kilimanjaro,hili ni kosa kubwa,nchi hii ni kubwa mno ya makabila kwa makabila na ktk chama chochote wanapaswa kuiondoa hii picha.ASANTE