Wanabodi,
Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli pande hizi CCM ina hali mbaya sana, huku CCC Imechokwa sana mpaka basi!.
Kama CCM Imechokwa, Mbona Inachaguliwa na Inashinda?
Siku zote nimekuwa nikisema humu, kuwa kuna baadhi ya maeneo CCM imechokwa ila bado CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika sana, hapana!, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi kwa sababu ya mazoea tuu wengi wakiichagua CCM kwa sababu ndicho chama pekee walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu kama asante ya kutupatia uhuru, kwa sasa ni oldguards, wamezeeka, wanazidi kupungua na wachache waliobakia their days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance, sasa wameanza kuerevuka na wameanza kuamka!.
Tabia za Maeneo CCM ya Stronghold za CCM na Stronghold za Opposition.
Stronghold ni eneo lenye nguvu ya chama fulani. Mfano CUF Stronghold yake ni Pemba, Chadema Stronghold yake ni Kanda ya Kaskazini, na CCM inamiliki maeneo mengine yote. Tabia za maeneo wanayochagua wapinzani, ni maeneo yenye maendeleo, watu wake wanajiweza kidogo kiuchumi hivyo wamesoma na kuelimika, hawawezi kudanganyika kirahisi rahisi. Kanda ya Kaskazini, ndio inayoongoza kwa high literacy levels ikifuatiwa na Bukoba, Mbeya Mwanza na Iringa, majiji yote yameshikwa na upinzani sababu watu wana nguvu ya kiuchumi hivyo wameelimika na kufuta ujinga hivyo wamechagua upinzani.
Maeneo ya Stronghold ya CCM, ni maeneo yote yenye umasikini uliotope na low literacy levels, hivyo ni rahisi kudanganyika na kuna wanaoichagua bila kujua wanachagua nini!. Hivyo CCM itazidi kuchaguliwa as long as umasikini unaendelea.
Majaaliwa ya CCM Kanda ya Kaskazini
Kwa mujibu wa kada mbalimbali za wale niliozungumza nao, wamenithibitisha pasi shaka kuwa hakuna jinsi yotote wagombea wa CCM wa kanda hii kama Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nang'uro wataweza kusalimika, sehemu pekee salama kwa CCM mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu kwa sababu ya Lowassa!, na maeneo ya upareni nako CCM bado ni salama kwa sababu ya umasikini uliotopea, lakini kungine kote, Kanda ya Kaskazini, CCM haina chake, CCM haipati kitu!.
Kama kasi ya upepo wa mwamko kama huu wa Kanda ya Kaskazini kuichukia CCM, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then amini usiamini, hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015, CCM inakwenda kupigwa chini!. Kwa vile hili CCM pia wanalijua, mtashuhudia juhudi za ziada kwa CCM kuelekeza nguvu nyingi na nguvu kubwa ya ziada
kwenye kanda hii ya Ziwa na kwa vile tayari kuna majimbo matatu Kanda ya Ziwa yako chini ya Chadema, kama Chadema itaendelea kuyas
hikilia na kuongeza kasi ya Chadema kukubalika na kupendwa kanda ya Ziwa, kiukweli kabisa, CCM itakuwa kwenye hali mbaya sana kwenye kanda hii hivyo inakwenda kuandika!.
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na mshishangae, ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.
Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utaimlilki kanda ya Ziwa.
Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.
Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.
Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.
Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!
Wasalaam.
Paskali
Kirua Vunjo, Moshi Vijijini
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...