Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Wanabodi,

Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli pande hizi CCM ina hali mbaya sana, huku CCC Imechokwa sana mpaka basi!.

Siku zote nimekuwa nikisema humu, kuwa kuna baadhi ya maeneo CCM imechokwa ila bado CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika sana, hapana!, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi kwa sababu ya mazoea tuu wengi wakiichagua CCM kwa sababu ndicho chama pekee walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu kama asante ya kutupatia uhuru, kwa sasa ni oldguards, wamezeeka, wanazidi kupungua na wachache waliobakia their days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance, sasa wameanza kuerevuka na wameanza kuamka!.

Tabia za Maeneo CCM ya Stronghold za CCM na Stronghold za Opposition.
Stronghold ni eneo lenye nguvu ya chama fulani. Mfano CUF Stronghold yake ni Pemba, Chadema Stronghold yake ni Kanda ya Kaskazini, na CCM inamiliki maeneo mengine yote. Tabia za maeneo wanayochagua wapinzani, ni maeneo yenye maendeleo, watu wake wanajiweza kidogo kiuchumi hivyo wamesoma na kuelimika, hawawezi kudanganyika kirahisi rahisi. Kanda ya Kaskazini, ndio inayoongoza kwa high literacy levels ikifuatiwa na Bukoba, Mbeya Mwanza na Iringa, majiji yote yameshikwa na upinzani sababu watu wana nguvu ya kiuchumi hivyo wameelimika na kufuta ujinga hivyo wamechagua upinzani.

Maeneo ya Stronghold ya CCM, ni maeneo yote yenye umasikini uliotope na low literacy levels, hivyo ni rahisi kudanganyika na kuna wanaoichagua bila kujua wanachagua nini!. Hivyo CCM itazidi kuchaguliwa as long as umasikini unaendelea.

Majaaliwa ya CCM Kanda ya Kaskazini
Kwa mujibu wa kada mbalimbali za wale niliozungumza nao, wamenithibitisha pasi shaka kuwa hakuna jinsi yotote wagombea wa CCM wa kanda hii kama Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nang'uro wataweza kusalimika, sehemu pekee salama kwa CCM mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu kwa sababu ya Lowassa!, na maeneo ya upareni nako CCM bado ni salama kwa sababu ya umasikini uliotopea, lakini kungine kote, Kanda ya Kaskazini, CCM haina chake, CCM haipati kitu!.

Kama kasi ya upepo wa mwamko kama huu wa Kanda ya Kaskazini kuichukia CCM, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then amini usiamini, hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015, CCM inakwenda kupigwa chini!. Kwa vile hili CCM pia wanalijua, mtashuhudia juhudi za ziada kwa CCM kuelekeza nguvu nyingi na nguvu kubwa ya ziada
kwenye kanda hii ya Ziwa na kwa vile tayari kuna majimbo matatu Kanda ya Ziwa yako chini ya Chadema, kama Chadema itaendelea kuyas
hikilia na kuongeza kasi ya Chadema kukubalika na kupendwa kanda ya Ziwa, kiukweli kabisa, CCM itakuwa kwenye hali mbaya sana kwenye kanda hii hivyo inakwenda kuandika!.

Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na mshishangae, ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.

Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utaimlilki kanda ya Ziwa.

Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.

Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.

Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.

Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!

Wasalaam.

Paskali
Kirua Vunjo, Moshi Vijijini
Kilimanjaro na Arusha CCM ipoipo tu.Labda utawala huu unaweza kukiimarisha chama hicho huko.Manyara nako wanaendelea kuiga huko.Tanga bado CCM inapendwa sana tu.Kwa Arusha na Kilimanjaro ni shughuli pevu kwa CCM
 
Pascal naona umerudi kuzunguka na Lowasa kwenye kampeni za udiwani kwa kazi ya PR ya kujenga image nzuri ya Chadema at a fee.kuukosa ukurugenzi wa habari ikulu kama lowasa angeshinda naona bado uko unauwewesekea.
Mkuu Yehodaya, watu waliofilisika, ndio wanaomjadili mtoa hoja badala ya kuijadili hoja iliyoko mezani.

Hili la kuukosa Ukurugenzi, kwa vile Lowassa amekosa, ni mawazo yako tuu, mimi sio team Lowassa, wala sijawahi kuwa team Lowassa wala team yoyote, kwa sababu sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote, bali ni supporter wa watu ninaowakubali, na Edward Lowassa ni mmoja wao, ila mimi sio mtu wake, ila kwa bahati nzuri sana, nina pacha wangu ni mtu wa inside wa Lowassa ambaye ndiye angekuwa mkurugenzi na sio mimi, labda kitu pekee ambacho mimi ningefaidika nacho ni kupata mapande tuu ya tenda za publicity za serikali.

Tembelea nyuzi hizi, halafu uniambie kama mwandishi ni mtu aliyekuwa akisubiria ukurugenzi toka kwa Lowassa
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi ...
Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa ...
Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais ...
ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote ...
Lowassa: Je, alikosea wapi? Akiamua kuendelea, arekebishe wapi ...
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha Uwezo ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
Paskali
 
Hili la polisi kupiga mabomu ya machozi Moshi, halikuanza leo Lowassa, lilianzia enzi za Omari Mahita ikiwa RPC wa mkoa wa Kilimanjaro alimvurumishia mabomu ya machozi Lyatomga Mrema, hadi mahita kupewa u IGP.

Angalia hapa

Natoa wito kwa watu wa Kanda ya Kaskazini kuipenda CCM ili kuepuka mabomu ya machozi.
Paskali
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Pascal naona umerudi kuzunguka na Lowasa kwenye kampeni za udiwani kwa kazi ya PR ya kujenga image nzuri ya Chadema at a fee.kuukosa ukurugenzi wa habari ikulu kama lowasa angeshinda naona bado uko unauwewesekea.
Ww ni Akili ndogo, huwezi kumwelewa Paskali akili kubwa. Dic in altum katika mada zake utamwelewa ila kama IQ yako ni ndogo sahau kumwelewa Paskali.
 
Umenena vyema, ila dola nayo haina marobot ni watu..watachoka! Kinachoendelea Zimbabwe kwa mtu wa kujifunza angeishapata funzo!
Ni ufinyu wa fikara na mtazamo hasi kulinganisha siasa Tanzania na Zimbabwe. Yamkini ndiyo maana tunagubikwa na umaskini katika nchi tajiri.
 
Ni ufinyu wa fikara na mtazamo hasi kulinganisha siasa Tanzania na Zimbabwe. Yamkini ndiyo maana tunagubikwa na umaskini katika nchi tajiri.
Kwa werevu wako na fikra za ki PHD tufananishe siasa za Tanzania ya kina sezonje na siasa za Marekani siyo? Ama tuzilinganishe na za ulaya kabisa?
 
Kwa werevu wako na fikra za ki PHD tufananishe siasa za Tanzania ya kina sezonje na siasa za Marekani siyo? Ama tuzilinganishe na za ulaya kabisa?

Katika jibu langu hakuna nilipotaja PhD. Kama hukwenda shule jilaumu mwenyewe tu maana hakuna wa kukupa akili. Akili ni nywele, kila mtu anazo zake.

Rejea jibu lako kama ni la mtu aliyefikiri nje ya kisandugu. Hakika umethibitisha kiwango chako cha kufikiri.
 
Huwa sifanyi argument na wapumbavu! Tafuta jambo ambalo unaona unauwezo nalo si lazima utake niwe na msimamo wako!
 
Huwa sifanyi argument na wapumbavu! Tafuta jambo ambalo unaona unauwezo nalo si lazima utake niwe na msimamo wako!

Mh! Nimekuelewa.

Nikushauri tu, ujikite kwenye mada kuu, ukitaka kuchangia na uchangie kwa hoja siyo hisia. Nitakuwepo muda wote humu jamvini kukujibu, kwa jinsi utavyochangia kwa hoja za ndani ya kisanduku.
 
Ulikuwa na sababu gani ya kunifundisha namna ya kuchangia kwani wewe ndo umeanzisha thread? Wewe ungebaki na mawazo yako ya kwenye kisanduku na wengine wabaki na misimamo yao tofauti ili maisha yaendelee....watu wengine mpo kuharibia wengine mood tu!
 
.....CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.
 
Hawakawii kutupatia "Mnangagwa"
 
...........CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.

Pascal Mayalla ulituaminisha huyu jamaa ndio masiha na 2020 upinzani huna haja ya kuweka mgombea,kwa kipi haswa?!

Ukaja ukatuhubiria kuwa Makonda anafaa 2025 baada ya ajali ya Chato,bado una imani na mahubiri ya watu wako?!
 
.....CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.
Angalia tarehe ya bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
P.
 
...........

Pascal Mayalla ulituaminisha huyu jamaa ndio masiha na 2020 upinzani huna haja ya kuweka mgombea,kwa kipi haswa?!

Ukaja ukatuhubiria kuwa Makonda anafaa 2025 baada ya ajali ya Chato,bado una imani na mahubiri ya watu wako?!
Mkuu Kipumbwi, kwa vile 2020 bado, Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ... bandiko hili bado liko valid
ila kama ni upinzani kusimamisha mgombea ili kushiriki tuu, then nimeshauri Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha Uwezo ...

Na kwa vile 2025 bado ni mbali sana, bandiko hili pia bado liko valid, 2020 huyu dogo anachukua jimbo na kupewa vizara nyeti. Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana ...

P.
 
Back
Top Bottom