Mku unaweza kuwa na kila kitu lakini ukawa Bado yaani mashamba na hawa wako wengi.Unakuta mtu amealikwa ktk hafla ya kijamii ya kuotesha miti au ufunguzi wa kikombe cha mpira alafu mtu anakuja sehemu ya tukio kuvaa suti.UMENIFADHAISHA SANA...
Yupo kijana mmoja wakati tuko UDSM alikosa mkopo akiwa na vigezo, akakata rufaa mara mbili zikatupwa, akaja ofisini DARUSO akiomba asaidiwe kuandika barua ya kuahirisha masomo, mimi nikiwa Waziri Mkuu wa DARUSO nikakuta mawaziri wanasaidia kumuandikia ile barua.
Nikawaomba wakimaliza waje naye ofisini kwangu. Walipomaliza wakaja, basi nikamuomba yule kijana avumilie hadi Jumatatu aje DARUSO na nikamtaka ile barua ya kuahirisha masomo aniachie, akaniambia hata nauli ya kujia hana (alikuwa anakaa kwa mjomba wake Yombo), basi nikampa Shs 2,500 zilikuwa pesa zangu binafsi.
Jumatatu hiyo akaja, nikamchukua mguu kwa mguu, tukapanda daladala kituo cha KONTENA hadi Mwenge, Mwenge hadi BODI YA MIKOPO. Tukaingia kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa bodi ya mikopo, Mzee Nyatega, nikawasilisha kesi ya yule kijana na nika DEMAND kuwa lazima apewe mkopo, nikampa Nyatega ile barua ya mwanafunzi kwenda kwa DVC - AC kuahirisha masomo.
Nyatega akaniomba wiki nzima ashughulikie suala hilo. Basi yule kijana akarudi Yombo, akakaa wiki mbili na kwa kweli sikuwa na uwezo wa kumsaidia nauli ya chuo wala pesa ya chakula kwa siku hizo.
Siku moja akanipigia simu analia, alikuwa amepata mkopo. Basi akakimbia NBC ku-draw fedha, akaja DARUSO kuniletea tzs 50,000, nikazikataa (na ilikuwa kawaida yangu). Akaja Hill Park siku moja akanikuta nakula, akataka kunilipia BILL, nikakataa.
Nilipomaliza chuo tukapoteana, karibu miaka 10, nimekuja kukutana na huyu kijana wiki kadhaa zilizopita, Mlimani CITY, akiwa na vijana wenzake wa UVCCM wana gari yao XTRAIL, basi tukasalimiana, hata kunipa mkono anaogopa, nasikia hivi sasa yeye ni DAS. Basi, jana kanimaliza nguvu, kwenye POST ya Tamko la Vyama Vitano kuonya mwenendo wa uchaguzi, kaja kanitukana kweli kweli, nikamblock.
Nachojivunia ni kuwa, amefika hapo alipo kwa sababu Mungu alinipa nguvu na akili za kutatua tatizo lake. Na kama nisingelifanya kazi hiyo mimi, Mungu angelimtuma mtu mwingine amsaidie, he was just a POOR BOY, poorer just like I was. And right now he is still poorer in the brain unlike to what I am.
Kwamba kuwa DAS au CCM ndiko kumemfanya leo asahau kabisa kuwa kuna watu ana historia nao? Probably the next time I meet him, he will be a RC and will not look into my eyes.
Nawakumbusha vijana hasa wa CCM kuwa vyeo siyo maisha. Utu wa mtu unapimwa kwa namna mtu huyo anavyoishi na wengine kwa heshima, uadilifu, kusaidiana na kutakiana mema.
Wapo mawaziri wa CCM tukipishana nao barabarani wanasimama, wanashuka, tunasalimiana na hawa walipokuwa Chuo Kikuu tulikuwa hatujazaliwa. Na mko nyinyi vijana msiojua kesho yenu ambao u DAS, u DC au u RC unawafanya muone dunia imekwisha.
Kalabaghaho, meseji hii ikufikie na iifikie jamii!
Mtatiro J