Mtatiro: Nawakumbusha vijana hasa wa CCM kuwa vyeo siyo maisha

UMENIFADHAISHA SANA...

Yupo kijana mmoja wakati tuko UDSM alikosa mkopo akiwa na vigezo, akakata rufaa mara mbili zikatupwa, akaja ofisini DARUSO akiomba asaidiwe kuandika barua ya kuahirisha masomo, mimi nikiwa Waziri Mkuu wa DARUSO nikakuta mawaziri wanasaidia kumuandikia ile barua.

Nikawaomba wakimaliza waje naye ofisini kwangu. Walipomaliza wakaja, basi nikamuomba yule kijana avumilie hadi Jumatatu aje DARUSO na nikamtaka ile barua ya kuahirisha masomo aniachie, akaniambia hata nauli ya kujia hana (alikuwa anakaa kwa mjomba wake Yombo), basi nikampa Shs 2,500 zilikuwa pesa zangu binafsi.

Jumatatu hiyo akaja, nikamchukua mguu kwa mguu, tukapanda daladala kituo cha KONTENA hadi Mwenge, Mwenge hadi BODI YA MIKOPO. Tukaingia kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa bodi ya mikopo, Mzee Nyatega, nikawasilisha kesi ya yule kijana na nika DEMAND kuwa lazima apewe mkopo, nikampa Nyatega ile barua ya mwanafunzi kwenda kwa DVC - AC kuahirisha masomo.

Nyatega akaniomba wiki nzima ashughulikie suala hilo. Basi yule kijana akarudi Yombo, akakaa wiki mbili na kwa kweli sikuwa na uwezo wa kumsaidia nauli ya chuo wala pesa ya chakula kwa siku hizo.

Siku moja akanipigia simu analia, alikuwa amepata mkopo. Basi akakimbia NBC ku-draw fedha, akaja DARUSO kuniletea tzs 50,000, nikazikataa (na ilikuwa kawaida yangu). Akaja Hill Park siku moja akanikuta nakula, akataka kunilipia BILL, nikakataa.

Nilipomaliza chuo tukapoteana, karibu miaka 10, nimekuja kukutana na huyu kijana wiki kadhaa zilizopita, Mlimani CITY, akiwa na vijana wenzake wa UVCCM wana gari yao XTRAIL, basi tukasalimiana, hata kunipa mkono anaogopa, nasikia hivi sasa yeye ni DAS. Basi, jana kanimaliza nguvu, kwenye POST ya Tamko la Vyama Vitano kuonya mwenendo wa uchaguzi, kaja kanitukana kweli kweli, nikamblock.

Nachojivunia ni kuwa, amefika hapo alipo kwa sababu Mungu alinipa nguvu na akili za kutatua tatizo lake. Na kama nisingelifanya kazi hiyo mimi, Mungu angelimtuma mtu mwingine amsaidie, he was just a POOR BOY, poorer just like I was. And right now he is still poorer in the brain unlike to what I am.

Kwamba kuwa DAS au CCM ndiko kumemfanya leo asahau kabisa kuwa kuna watu ana historia nao? Probably the next time I meet him, he will be a RC and will not look into my eyes.

Nawakumbusha vijana hasa wa CCM kuwa vyeo siyo maisha. Utu wa mtu unapimwa kwa namna mtu huyo anavyoishi na wengine kwa heshima, uadilifu, kusaidiana na kutakiana mema.

Wapo mawaziri wa CCM tukipishana nao barabarani wanasimama, wanashuka, tunasalimiana na hawa walipokuwa Chuo Kikuu tulikuwa hatujazaliwa. Na mko nyinyi vijana msiojua kesho yenu ambao u DAS, u DC au u RC unawafanya muone dunia imekwisha.

Kalabaghaho, meseji hii ikufikie na iifikie jamii!

Mtatiro J
Mku unaweza kuwa na kila kitu lakini ukawa Bado yaani mashamba na hawa wako wengi.Unakuta mtu amealikwa ktk hafla ya kijamii ya kuotesha miti au ufunguzi wa kikombe cha mpira alafu mtu anakuja sehemu ya tukio kuvaa suti.
 
Unapokutana na mtu mnapaswa kusalimiana...hapa namaanisha ni wajibu wa kila mmoja kumuanza mwenzake kumsalimia. Tena kama mmepotezana kwa muda mnaweza kujikuta mnarukiana na kukumbatiqna kwa pamoja.

Sasa hapa inategemea, na Mtatiro hajaeleza chochote...kwamba:-
1. Je, Mtatiro alimsalimia jamaa akagoma kujibu salaam?
2. Ama Mtatiro alijivika ufalme na kusubiri kusalimiwa kwakuwa aliwahi kumsadia siku za nyuma?
Kama namba 1 ilifanyika Jamaa ana matatizo na anastahili kulaumiwa na kulaaniwa. Kama namba 2 ilifanyika Mtatiro hakwepi lawama na laana hapa.
Mtatiro kataja xtrail, ina maana xtrail ndo ilifanya huyo kijana asimsalimie? Lakini aliyeanza kumwona.mwenzake ni yeye mtatiro, kwa hiyo ilikuwa vyema angemsalimia halafu aone kama jamaa hataitikia.
 
Mh.Mtatairo kuna maneno yanasema kwenye biblia kuwaa, "Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu"Hawa vijana wanasahu kuwa cheo ni dhamani tu.
 
Unapokutana na mtu mnapaswa kusalimiana...hapa namaanisha ni wajibu wa kila mmoja kumuanza mwenzake kumsalimia. Tena kama mmepotezana kwa muda mnaweza kujikuta mnarukiana na kukumbatiqna kwa pamoja.

Sasa hapa inategemea, na Mtatiro hajaeleza chochote...kwamba:-
1. Je, Mtatiro alimsalimia jamaa akagoma kujibu salaam?
2. Ama Mtatiro alijivika ufalme na kusubiri kusalimiwa kwakuwa aliwahi kumsadia siku za nyuma?
Kama namba 1 ilifanyika Jamaa ana matatizo na anastahili kulaumiwa na kulaaniwa. Kama namba 2 ilifanyika Mtatiro hakwepi lawama na laana hapa.
Mkuu kilichoonekana hapa ndugu DAS hakupenda vijana wenzake wa uvccm waone kuwa anafahamiana vizuri na mpinzani.
 
Hatupotoshi tunamuelimisha Yeye na Wenye akili Kama zake ukiwemo Wewe!
Kumpa Mwanafunzi Tsh elf mbili Mia Tano Miaka 10 iliyopita na kuja kuhadithia kwa lengo la kumdhalilisha ni ulimbukeni na Ushamba wa Hali ya juu sana!

Nani angemjua Lipumba ndani ya CUF Kama sio Prof Lipumba? Tena Mtatiro anajua kabisa wale Wapemba wa Seif walikuwa hawamtaki Kabisa kumuona Buguruni Mbona Lipumba hazungumzi hayo kuonesha alivyomsaidia?
Huyu Mtatiro angemsaidia kumlipia Mtu Walau Ada ya robo semester si angetaka aabudiwe?
Ukimsadia Mtu kidhati hutakiwi kutumia Kama reference ya kumdhalilisha aache ushamb
Hakumdhalilisha ila UKWELI ndio umemdhalilisha. Asante sana kwa kugundua kuwa amedhalilika kwa kitendo alichofanya! Na... mind you.... msaada wa sh 100 unaweza kuwa mkubwa kuliko msaada wa sh milioni moja!
 
Na hapo ndipo tunapobishana. Ubongo wako hauoni cha kujifunza kwenye hii thread! Basi nitakusaidia: Fahari na mali ya ulimwengu HAISHINDI utu!


Tunajenga Tanzania mbaya sana sana sana kwa vizazi vijavyo kwa sababu tu ya kujikweza na fahari za madara hasa haya yanayopatikana kwa kupeana kirafiki.

Watanzania tukumbushane kuhusu Katiba mpya ili tujenge nchi kwa misingi ya utu ,haki, usawa na utawala bora.
Kwa sasa ni kwamba yule anayeonyesha juhudi kubwa ya kumchikia mpinzani wake na hata kumkata mapanga na kuunda vikundi vya kutesa wengine ndio anatunukiwa madaraka yenye mishahara na marupurupu kibao kwa kodi ya hao hao anawatesa.

Nchi inakoelekea sio kuzuri kwa umoja wa taifa.
Lakini ki vyeo ndani ya CCM.
Sijui kwa nini CCM wameamua kuja na siasa za kitalebani katika nchi yenye umoja na demokrasia kama Tanzania.

Kwa muda mrefu CCM walikua na siasa za kifisadi lakini tuliwavumilia sana na kuwaona kama ndugu zetu lakini sasa wamebadilika kwa namna nyingine ya siasa za chuki na uhasama ili wasiulizwe kuhusu haki za watu.

Sula la huyo kijana limenitia huzuni na simanzi kubwa kwa sababu ndipo tulipofikia kisiasa.
 
Vyama vipo tu ila Utu ni wakuheshimu sana, Mimi sitakuja kuwa mshabiki wa chama chochote kutoka Moyoni mwangu mana Hao tunaowashibikia hata wao hawaeleweki na misimamo yao Leo mtu Angesimama kidete kuhakikisha Anna mwigira haibiwi kula hata kwa Kutoka Damu Lakini Anna huyo huyo hana Msimamo na Kuhama Chama kwa masilahi yake binafsi nasema ivi hakuna mwanasiasa mkweli hata mmoja Tusidhubutu Kupigana au kutukanana kisa hawa wanasiasa ambao Familia zao ziko safe mimi mwanasiasa akishakuwa jukwaani na Haongei habari za kuniletea maji au Umeme badala yake Anaiponda CCM au CUF basi huyo hanifai hata kidogo...Tumuunge mkono Rais kwa Target yake ya maendeleo bila kujali Chama.
Kuna Rais alikuwa akileta maendeleo kwa kujali vyama?
 
Mtatiro, kumsaidia mtu haina maana kwamba sasa ndiyo atakuwa mtumwa wako. Midhali yeye alipopata mkopo alikuja ofisini kwako kukushukuru tena akiwa amebeba elfu 50, na baadaye Hill Park akataka kulipia msosi na vinywaji, lkn kwa maadili yako ukakataa. Basi it is over between wewe na yeye.

Haina maana kuwa kwa kuwa ulimsaidia basi awe anakusujudia. Na kwa malalamiko haya msaada wako ni batili, huo siyo msaada. Maana mtoa msaada husahau. Wewe uliweka msaada benki ili siku ya siku upate riba ya kuabudiwa. Ni hayo tu mazee.

Ni mm mwanaUKAWA mwenzio.
Soma post upya
 
Mtatiro, kumsaidia mtu haina maana kwamba sasa ndiyo atakuwa mtumwa wako. Midhali yeye alipopata mkopo alikuja ofisini kwako kukushukuru tena akiwa amebeba elfu 50, na baadaye Hill Park akataka kulipia msosi na vinywaji, lkn kwa maadili yako ukakataa. Basi it is over between wewe na yeye.

Haina maana kuwa kwa kuwa ulimsaidia basi awe anakusujudia. Na kwa malalamiko haya msaada wako ni batili, huo siyo msaada. Maana mtoa msaada husahau. Wewe uliweka msaada benki ili siku ya siku upate riba ya kuabudiwa. Ni hayo tu mazee.

Ni mm mwanaUKAWA mwenzio.

Hayo maneno niliyoya-bold yote umetoa kichwani kwako na hujui maana yake..............
 
BVOTnOvjzxf.jpg
 
Duh! Huyo jamaa alichofanya ni kitu cha hovyo sana. Siasa zisitufanye tuwe maadui. Kuna maisha baada ya siasa.
 
kunawatu huwa hawaoni kama kuna maisha inje ya vyeo,tabia hii wanayo watu wengi saana,wapo na uroho na njaa kali
 
L
Sawa! Je ni mawaziri wakuu wangapi waliokuwa ama wenye ujasiri kama aliouonesha Mh. Mtatiro?
Alichokifanya Mtatiro ni kutimiza majukumu yake kwa weledi na upendo mkubwa. Ndiyo kusema Mtatiro ni kiongozi mzuri sana. Lkn uungwana na weledi wake huo havipaswi kuwa deni kwa mhudumiwa.
 
Sina chama na pia namuomba Mungu anitenge na siasa ktk maisha yangu yote.Mtatiro ametoa jambo zito sana na lina fundisho kwa vijana.
Haiingiii akili hata kidogo huyo kijana kama emesahau wema na moyo wa Mtatiro hadi kufikia kumpa maneno makali kiasi hicho hadi aje humu kuanzisha uzi Jf.
Vyeo ni dhamana na pia cheo hakidumu .Yuko wapi yule kijana meya wa Ilala namjua kwa jina moja tu SLaa.

Mungu niepushe na siasa ktk maisha yangu kama utavyoniepusha dhambi zingine.
 
Mtatiro, usishangae huo ndiyo ulimbukeni wa maisha. Inawezekana u-DAS kwake ni 'Dream Job' hivyo atautetea kwa nguvu zote. Hakupaswa kukutukana hata kama vyama vyenu bi tofauti, mngebishana kwa hoja tu!
 
Back
Top Bottom