Mtatiro: Nawakumbusha vijana hasa wa CCM kuwa vyeo siyo maisha

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,112
2,000
Vijana wa miaka 30 mkianza siasa za visasi kwa sababu ya Kulinda wazee ambao wameona kuwa siasa hizo zitawanufaisha wao kupata muda wa kustaafu hakika mnajidanganya sana.
Nina imani kabisa kuwa kijana wa miaka 30 anayewaza kuwa CCM ndio baba yake na mama yake kwenye karne hii basi hana akili kabisa.
Hayo tuwaachie akina Mzee Kinana ambao walitoka ujanani na chama hicho mpaka leo hata hivyo bado wanaheshimu watu wengine wanaotofautiana nao kiitikadi.
Wazee walikotoka wanajua kabisa kuwa CCM ilikua na wanachama kwa 100% kwa wakati huo mana kila mtu ilikua ni lazima awe na kadi ya CCM lakini tangu waliporuhusu mfumo wa vyama vingi chama hicho kimekua kikipoteza umaarufu siku hadi siku.
Kwa hiyo hao vijana wenye umri under 35 wanaojifanya kuwa wao ni watoto wa miungu watu na kuwaona wengine ni maadui zao watambue kabisa kuwa kabla hawajafikisha miaka 50 watauona Mkono wa Mungu wa kweli ukiwainua wale ambao leo wanawadharau na kuwatendea ukatili na kiburi ; watajikuta siku moja wanaishia gerezani kumalizia viinua mgongo vyao na maisha yao huko.
Siioni CCM ya miaka 15 ijayo kwa hizi siasa za kuwanyima watu uhuru wao wa asili ya mwanadamu ambao hata Yesu aliupigania mpaka kufa.
Yesu alisema kuwa mwana akiwaweka huru mtakua huru kweli kweli maana kweli itawaweka huru.
Sasa leo uhuru umekua ni wa masharti ya kuisifia CCM as if CCM ndio Mungu asiye na makosa.
Maadam haya yanatendeka kwenye nchi ya watu wanaomtaja Mungu Muumba wa vitu vyote basi ninaamini liko jibu la Mungu kwa watu wake wanaodhalilishwa kwa sababu ya wengine kupenda madaraka na utukufu.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,247
2,000
Mtatiro, kumsaidia mtu haina maana kwamba sasa ndiyo atakuwa mtumwa wako. Midhali yeye alipopata mkopo alikuja ofisini kwako kukushukuru tena akiwa amebeba elfu 50, na baadaye Hill Park akataka kulipia msosi na vinywaji, lkn kwa maadili yako ukakataa. Basi it is over between wewe na yeye.

Haina maana kuwa kwa kuwa ulimsaidia basi awe anakusujudia. Na kwa malalamiko haya msaada wako ni batili, huo siyo msaada. Maana mtoa msaada husahau. Wewe uliweka msaada benki ili siku ya siku upate riba ya kuabudiwa. Ni hayo tu mazee.

Ni mm mwanaUKAWA mwenzio.

HAPANA!!

Nina hakika kwa 150% hujaielewa mantiki ya hoja ya Julius Mtatiro unless wewe ndiwe uwe huyo bwana aliyetolewa kama reference hapa...

Kama unabisha, jaribu kusoma tena na tena alichokiandika Bw Mtatiro, then linganisha na reaction yako utagundua kuwa, you are off the shore...!!
 

Sueky

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
320
250
Nimependa ulivyoipangilia hii story kwakweli inasisimua.
Kiukweli watanzania wengi tu malimbukeni sana.
Niwepesi sana kwa mambo mengi ..
mtu atakutafta sana akiwa na shida baada ya shidakwisha yuko tayr akutoe roho.
Hata kiimani nimeona kwa hapa Tz waumini waziri ni wale wenyeshida ...shida zikipungua na wao huwaoni nyumba za ibada
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,473
2,000
HAPANA!!

Nina hakika kwa 150% hujaielewa mantiki ya hoja ya Julius Mtatiro unless wewe ndiwe uwe huyo bwana aliyetolewa kama reference hapa...

Kama unabisha, jaribu kusoma tena na tena alichokiandika Bw Mtatiro, then linganisha na reaction yako utagundua kuwa, you are off the shore...!!
Angalia mwenyewe maneno ya Mtatiro haya:-
"Kwamba kuwa DAS au CCM ndiko kumemfanya leo asahau kabisa kuwa kuna watu ana historia nao? Probably the next time I meet him, he will be a RC and will not look into my eyes"
Mtatiro alitaka kijana wa watu afungwe na historia ya kwamba aliwahi kusaidiwa na Mtatiro kwahiyo anyenyekee.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,473
2,000
Hakungoja shukrani ndio maana alikataa elfu 50.. Hujaelewa somo lake wewe uvccm usiye na akili kuchwani
Kama alikataa elfu hamsini kwann analilia kupewa mkono wa salaam? Huoni kwamba alikataa elfu 50 ili riba/malipo yake ya "fadhila" yaongezeke?

Zingatia hapo, nimeiita "fadhila", maana fadhila haina riba wala malipo
 

SACO

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
1,473
2,000
Posho ulikuwa unalipwa kwa kazi hiyo, isiwe kuwa umepata ridhaa ya kuwanyanyasa
 

pongwa yusufu

Senior Member
Jul 28, 2016
189
250
dunia hii ina maajabu mengi sana kama mtu anahukumiwa kunyongwa then hukumu inabadilishwa mpaka kifungo cha maisha the end of the game mtu yupo huru na familia yake akiwa mzee kabisa tena masikini tu so lolote linatokea keep in waiting ccm!
 

Nanaa jolie

Senior Member
Aug 9, 2017
145
500
Umenikumbusha wtz si watu wa kusaidia hata kidgo.
Nilimsadia dada mmoja kupata kazi ilikuwa niende mimi nikampa yeye hio nafasi kutokana shida alizokua nazo nilimuachia kiroho safi matokeo yake maneno yaliyozuka hapo alinigombanisha na mabest.. Nashukuru Mungu nilipo kwa sasa hanipati
 

charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
437
225
kwenye maswala ya uchaguzi, NEC ndio arbiter wa vyama vyote vya siasa. ipo kwa ajili ya vyama vya siasa na wanasiasa kwa maswala ya uchaguzi. niseme tu kwamba election is not an event, its a process that is defined in our constitution. an election process involves players and in this case political parties which must be treated equally and fairly. in other words political parties are stakeholders in an election process which is managed by NEC, therefore for NEC to refuse to consider concerns raised by very same stakeholder then it has no business existing. election is not a big deal but credibility of an election is what matters. NEC is there to ensure credibility of an election process by addressing such concerns.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,247
2,000
Angalia mwenyewe maneno ya Mtatiro haya:-
"Kwamba kuwa DAS au CCM ndiko kumemfanya leo asahau kabisa kuwa kuna watu ana historia nao? Probably the next time I meet him, he will be a RC and will not look into my eyes"
Mtatiro alitaka kijana wa watu afungwe na historia ya kwamba aliwahi kusaidiwa na Mtatiro kwahiyo anyenyekee.

Well. Inawezakana ikawa hivyo kwa kadiri ulivyoelewa....

Lakini ukimsoma jamaa kwa umakini mkuu, logic ya hoja yake ni kuwa hata tukifanikiwa ktk namna mbalimbali ikiwemo hata hii "mafanikio ya kivyeo".....

Kwamba, mtu hahitaji kujiona ameshapanda mlima hata kusahau tulikotoka na kwamba atang'ang'ania huko huko milele na kuwatazama walio chini bondeni, na kuwaona kama sisimizi tu.....

Kwamba, tunahitaji kuheshimiana na kutambuana pasipo kujali "status" zetu ktk jamii ama tofauti zetu za kiitikadi...

Na kwa hili la historia, unabisha bure. Hakuna kitu kisicho na historia yake yakiwemo mahusiano yoyote yale na kuyasema kama reference ya kitu flani haina maana kuwa tunafungwa ktk hayo isipokuwa kutambua tu tulikotoka, tulipo na tunakokwenda...

Hakuna ubaya ktk hili
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,247
2,000
Kama alikataa elfu hamsini kwann analilia kupewa mkono wa salaam? Huoni kwamba alikataa elfu 50 ili riba/malipo yake ya "fadhila" yaongezeke?

Zingatia hapo, nimeiita "fadhila", maana fadhila haina riba wala malipo

Halilii kupewa mkono, msome tena vizuri...

Logic ya hoja yake ni kuwa, hakuna haja ya kubadili mfumo wako kimahusiano ktk jamii bila kujali madidiliko ya kihadhi ktk jamii....

Mbona unakataa kabisa kulielewa hili kana kwamba watu wa namna hii hawamo ktk jamii zetu mkubwa?

Wako wengi mno. Na wako wengine hutafuta vyeo ama mali ili viwe/ziwe fimbo ya kuchapia wengine wasio nacho.

Kwa lugha rahisi kabisa, hutumia uwezo wao wa kimadaraka ama kifedha kwa lengo la "kutambuliwa" kwa njia hasi badala kutumia mabadiliko hayo kupata positive recognition..

Sijui umenielewa hapa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom