Kwenye Maisha unaweza kufanya jambo bila kuangalia standard yako, sio kusudi but hua inatokana na kutokufahamu uwezo wako na umuhimu wako katika maisha yako na jamii inayokuzunguka.
Lengo langu hasa ni kumhusu jamaa mmoja ambaye kapewa nafasi ya juu kwenye Chama cha siasa nchini (CUF), Nlisoma nae UDSM, alikua kiongozi imara na asiye tetereka kwa wale mnaomjua nadhani mtakubaliana nami, jamaa anajulikana kwa jina la Julius Mtatiro.
Kipindi tuko University alikua waziri mkuu na aliweza kusimamia mambo mengi bila woga na hata alipopata upinzani toka kwa raisi na waziri wa mikopo(Bush) jamaa hakujali na kuweka misimamo kwa manufaa ya wanafunzi wa hali ya chini. Sakata la wakati huo lilikua Kuanza kwa 40%. Wanafunzi wote tulipinga kwa msaada mkubwa wa Bwana Mtatiro Julius tulifanikiwa na kuanza kwa mean testing.
Rais wa Chuo na waziri wa Mikopo walipewa namna na serikali ya CCM, ili kusimamisha migomo na kutushurutisha wanafunzi wote tuache migomo, but Julius alikataa na kuwa pamoja nasi, mpaka ikamsababishia matatizo baada ya kusimamishwa chuo.
Kitu kinachoniuma mpaka kukaa kitako na kuchora waraka huu ni kutokana na Julius kujiunga na chama chenye nguvu hafifu kwa na kusababisha kupoteza nia yake.
Hua naamini kama angekua kwenye chama pinzani chenye nguvu basi hata mtu kama ZZK angekua anafuta nyuma tu, sababu jamaa yuko halisi sana.
Hayo ni mawazo yangu na maono binafsi.