Mtatiro aanza 'kufaidi mafanikio' hata kabla ya kujiunga rasmi CCM

Mi nawaonea huruma wale waliokaa mda mrefu ccm awapati nafasi ila wanaotoka upinzani wanakula shavu nahisi hata mtatiro atakula bonge la nafasi tutashangaa ngoja tuone
Hee ! maajabu yaani wewe chadema unawaonea huruma ccm unawaepnda Sanaa?!
 
Wapinzani wenyewe wanajikanyaga walishindwa kusimamisha mgombea mmoja mpaka mtatiro akakosa jimbo

Hii hoja yako ingekuwa na maana iwapo wabunge wa upinzani wasingehama. Kama ambao ni wabunge tayari wamehama nini asiye mbunge?
 
Hawa ndio aina ya wasomi tulionao. Naamini Mtatiro alikuwa upinzani kwa kazi maalumu, na kazi imeisha tyar
 
Katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF Julius Mtatiro alisikika akijivunia mafanikio ya kuhama CUF na kutangaza tu nia yake ya kujiunga na CCM hata kabla ya kujiunga na chama hicho rasmi.

Mafanikio aliyojivunia Mtatiro ni kupigiwa simu na viongozi wa CCM na kupongezwa kwa uamuzi wake huo. Mtatiro amesema kuwa leo hii atawasilisha barua/maombi yake rasmi ya kujiunga na CCM na anatumai kuwa atakubaliwa.

Yajayo yanafurahisha, mko tayari?
mwanasiasa yoyote katika maneno yake kumi anayosema amini moja tu tena kwa shingo upande...
 
Mi nawaonea huruma wale waliokaa mda mrefu ccm awapati nafasi ila wanaotoka upinzani wanakula shavu nahisi hata mtatiro atakula bonge la nafasi tutashangaa ngoja tuone
Hii ndio safi sasa maana itaondoa unafiki maana wengine hawana output kwenye chama iwe upinzani ama chama tawala yaani wanachofanya ni upambe na fitna kwa watu wao ili wale.sometimes ni heri kuwapa hao hao wapinzani ambao walipiga kelele kuikosoa serikali ili kuwapima kama yale waliokuwa wanayasema wanayaishi (wakifanikiwa ni pongezi kwao na wakichemsha ndio usemi wa wa ni rahisi kusema kuliko kutenda utakapodhihirika)
 
Watu wameshasahau kuwa hata Lowassa ambaye chadema walikuwa wanamwita fisadi namba 1, baada ya kuhamia chama hicho wakaanza kumwita mzee wa maamuzi magumu, jembe, na kadhalika. Hivyo siyo kitu cha ajabu alichokuwa anakisema mtatiro juu ya ccm na serikali yake. Hiyo ndo siasa.
Ni kweli mkuu..wakati mwingine heri hata Mtatiro na Lowasa ambao hawana nafasi zozote zitakazogharimu nchi lakini hawa wanaohama wakiwa wabunge na nchi yetu ilivyo ya kimasikini (of course kikatiba wapo sawa) najaribu kuangalia gharama za uchaguzi kwa jimbo moja zinakuwa double na mbunge yule yule anarudi kwa kuchaguliwa kupitia vyama viwili, kikatiba ni sawa na kisiasa hali kadhalika lakini kiuchumi hapo kasheshe maana bado tupo katika Taifa la kufanya shughuli za maendeleo kwa kipaumbele.
 
Kwa miaka mingi mtatiro kabaniwa sana huko upinzani.
Hata yaliyomkuta uchaguzi wa 2015 ni makubwa na magumu.
Mambo ambayo Lowassa alishindwa yavumilia ccm
Ikumbukwe, Mtatiro alipata fursa ya kugombea lililokuwa jimbo la ubungo awali na akapoteza kwa aliyekuwa mbunge kwa wakati huo yaani John Mnyika.

Alichokuwa akibaniwa ni kipi????
 
Katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF Julius Mtatiro alisikika akijivunia mafanikio ya kuhama CUF na kutangaza tu nia yake ya kujiunga na CCM hata kabla ya kujiunga na chama hicho rasmi.

Mafanikio aliyojivunia Mtatiro ni kupigiwa simu na viongozi wa CCM na kupongezwa kwa uamuzi wake huo. Mtatiro amesema kuwa leo hii atawasilisha barua/maombi yake rasmi ya kujiunga na CCM na anatumai kuwa atakubaliwa.

Yajayo yanafurahisha, mko tayari?
ohhohohhhoooooo!
 
Back
Top Bottom