Mtatiro aanza 'kufaidi mafanikio' hata kabla ya kujiunga rasmi CCM

Mi nawaonea huruma wale waliokaa mda mrefu ccm awapati nafasi ila wanaotoka upinzani wanakula shavu nahisi hata mtatiro atakula bonge la nafasi tutashangaa ngoja tuone
 
Kama chaguzi zenyewe zinasura Kama za kinondoni na buying nauhakika mwakani wabunge na karibu madiwani wote was upinzani watahamia ccm kwa kutetea tumbo zao else ndio itakuwa awamu yao ya mwisho kuingia mjengoni,inaumiza Sana inakatisha tamaa hata wapiga kura kwa matokeo yanavyokuja baada ya uchaguzi
 
Sitoshangaa jiwe kujiunga CHADEMA wakati wowote maana wako karibu na lowasa.
 
Usimwamini mwanasiasa aisee maana anaweza akafanya maamuzi mbadala muda wowote kama alivyofanya Mtatiro pamoja na kwamba ni haki yake ya kikatiba. Anaweza akaonyesha msimamo flani kuhusu chama flani alafu ndani ya miezi michache akaenda kulekule alipopaponda. Heri hata wale ambao wanaanza na kuwa kimwili kwenye chama flani huku kiroho yupo chama kingine mwisho wa siku hata akihama huwa wananchi hawajiulizi sana
Ni kweli! Hebu kumbuka Bw. Lowassa alivyokuwa akijiapiza kwamba hatahama CCM na kwamba asiyetaka yeye ndiye ahame! Lakini nini kilitokea?Japo sina uhakika kama alihama kwenda kutafuta cheo (uraisi) au alihama kwa moyo wa dhati kwamba CCM ilikuwa haina dira!
Nasubiri kuona tena atakakoelekea na genge lake pale watakaponyimwa kugombea urais 2020!
 
Sio sababu! Wale wa Siha, Ukonga, Kinondoni, mbona wao walipata hayo majimbo na bado wakatimka?
Mkuu, kosa la pili hali-justify kosa la kwanza, kukosea ni kukosea tu. Kutoachiana majimbo ile haikua good move na kumbuka ilitokea sehemu nyingi tu na zote walishindwa ingawa kwa idadi ya kura kama wasingezigawanya mgombea akawa mmoja wangeshinda.

Upinzani imara ni muhimu na unahitajika, so kwa mazingira haya haya ni lazima wawe na stategies za maana za kuwafanya wafanikiwe.
 
Katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF Julius Mtatiro alisikika akijivunia mafanikio ya kuhama CUF na kutangaza tu nia yake ya kujiunga na CCM hata kabla ya kujiunga na chama hicho rasmi.

Mafanikio aliyojivunia Mtatiro ni kupigiwa simu na viongozi wa CCM na kupongezwa kwa uamuzi wake huo. Mtatiro amesema kuwa leo hii atawasilisha barua/maombi yake rasmi ya kujiunga na CCM na anatumai kuwa atakubaliwa.

Yajayo yanafurahisha, mko tayari?

Mungu atusaidie sisi......yaani kupigiwa simu nayo ni mafanikio!!!! Daah.....
 
Wapinzani wenyewe wanajikanyaga walishindwa kusimamisha mgombea mmoja mpaka mtatiro akakosa jimbo

Angechukua jimbo angetia hasara serekali kwa kurudia uchaguzi. Bora alikosa. na inabidi asubiri mpaka 2020 akagombee buguruni na sio huku TBT hatumpi hata kwa kwa dawa.
Nibora kuchagua wabunge wanawake kuliko njemba za aina hii, vyuma vikikaza wanaweza kuuza hata familia zao ilimradi wapate sabuni ya roho
 
Usimwamini mwanasiasa aisee maana anaweza akafanya maamuzi mbadala muda wowote kama alivyofanya Mtatiro pamoja na kwamba ni haki yake ya kikatiba. Anaweza akaonyesha msimamo flani kuhusu chama flani alafu ndani ya miezi michache akaenda kulekule alipopaponda. Heri hata wale ambao wanaanza na kuwa kimwili kwenye chama flani huku kiroho yupo chama kingine mwisho wa siku hata akihama huwa wananchi hawajiulizi sana
Watu wameshasahau kuwa hata Lowassa ambaye chadema walikuwa wanamwita fisadi namba 1, baada ya kuhamia chama hicho wakaanza kumwita mzee wa maamuzi magumu, jembe, na kadhalika. Hivyo siyo kitu cha ajabu alichokuwa anakisema mtatiro juu ya ccm na serikali yake. Hiyo ndo siasa.
 
Back
Top Bottom