Mtanzania, wekeza na kufanya biashara Comoro

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
59,909
2,000
Fursa za Biashara zilizopo Moroni nchini Comoro

Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda nchini Comoro kufanya visual assessment ya fursa ziliopo kule lakini vile vile kuzungumza na wafanyabiashara wanaokuja Tanzania kununua bidhaa na kufanya biashara nchini.

Ndugu zangu Watanzania, Comoro kuna fursa nyingi kwa Watanzania hasa wenye nguvu kiuchumi na zipo fursa nyingi kwa wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.

Zifuatazo ni baadhi ya Fursa ziliopo Moroni (capital city) nchini Comoro:

1. Biashara ya chakula na vinywaji

Asilimia kubwa ya vyakula inatoka kwetu Tanzania. Kwa mfano mchele, nyama ya ngo’mbe na mbuzi, mbogamboga na matunda nk. Kwa mfano papai la kawaida tu kwa Moroni linauza Tsh 7,000. Bado viungo mbalimbali kama hiliki na karafuu bado vina soko kubwa. Vinywaji kama maji ya kunywa na juice pia zinatoka Tanzania.

2. Biashara ya Gereji /ufundi magari

Hadi hii leo Comoro hakuna gereji yenye uzoefu zaidi ya kukuta magari yanatengenezewa tu mtaani na sio gereji kama tulizokua nazo hapa Tanzania. Kwa mafundi na vijana wa Tanzania hii ni fursa kama mtu ataenda kufungua gereji maana atakua kiproffessional zaidi hivyo kuaminika kibiashara na kutengeneza mtaji na ajira

3. Biashara ya Bima

Hii ni biashara kwaajili ya waTanzania wanaofanya biashara Comoro na kwa Wacomoro wenyewe. Kwa mfano namna wafanyabiashara wa Tanzania walivyopoteza ngombe na mbuzi ambao walikufa wakiwa baharini hivyo kupata hasara hivyo akawaasa wafanyabiashara kufungua insurance agencies maana wateja wapo.

4. Biashara ya Hoteli

Kwa wale wenye mitaji mikubwa ni fursa adhimu sana kwao na hakuna urasimu ndani ya siku moja unakamilisha usajili. Moroni kuna hoteli kubwa moja five star na inamilikiwa na waTanzania. Zipo fursa kubwa kwa WaTanzania wanaotaka kuekeza hata kwenye Lodges

5. Fursa ya kufundisha Kiswahili na Kiingereza

Kwa upande wa Lugha, Comoro wanahitaji sana Walimu haswa wa Kiswahili. Tayari kuna Watanzania waliochangamkia fursa wanafundisha English na Kiswahili.

6. Biashara ya usafirishaji

Zipo fursa za kuanzisha safari za meli kutoka Tanzania mpaka Moroni. Asilimia kubwa sana ya cargo inatoka Tanzania lakini kuna uhaba wa vyombo vya kusafirisha licha ya kuwepo kwa soko kubwa sana na wakati mwingi wamiliki wa vyombo huwa fully booked kwa miezi in advance.

Pia, usafiri wa anga kuna fursa kubwa haswa hivi vi fly charter ni biashara kubwa sana na Cargo

7. Biashara ya nishati ya umeme

Comoro wanatumia umeme wa jenereta na heavy fuel. Grid yao ya taifa ni umeme unaozalishwa kwa jenereta hivyo si umeme wa uhakika. Tanzania inaweza ikazalisha umeme wa gas kisha ikawauzia Wacomoro. Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza wakafanya biashara ya majenereta na vifaa vyake kwa wingi au kuingia ubia na kampuni kuzalisha vyanzo vingi nishati

8. Biashara ya magogo na mbao

Hii ni fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani Comoro kuna uhaba mkubwa sana wa mbao na magogo kwaajili ya kuchania mbao. Hivyo kama mtu atapeleka magogo huko maana yake hata mashine za kuchania Mbao bado ni deal. Nchi ya Comoro miti ya mbao ni michache sana hivyo ndugu zangu Watanzania tuamke tuchangamkie fursa.

9. Biashara ya furnitures

Comoro wanategemea sana furniture kutoka Tanzania kama sofa, meza, luxury items n.k Kwahiyo kwa Watanzania ambao ni mafundi sofa au wenye viwanda vya furniture wanaweza kuchangamkia hii fursa. Pia mafundi sofa na mafundi serelemala wa furniture wanaweza wakaji organise kisha wakafungua kiworkshop chao wakapiga hela nzuri tu.

10. Biashara ya Vanilla

Comoro ni mzalishaji mkubwa sana wa vanilla duniani na kwao vanilla ni kama dhahabu na inabei kubwa wastani wa USD 500 per KG. Wakati wakulima wetu Bukoba na sehemu zingine Vanilla haifiki hata TSH 200,000 kwa KG. Hivyo basi mtu anaweza akanunua Vanilla Bongo kwa bei ya chini sana na akaenda kuiuza Comoro kwa bei ya juu sana.

11. Biashara ya screpa na spare za magari

Hili ni moja kati ya tatizo kubwa kwa Comoro maana magari mabovu ni mengi sana na hii inatokana na wao kutokua na gereji za kisasa na mafundi wa kutosha. Hivyo basi unaweza ukapeleka spare za magari Comoro na unaporudi zako Tanzania unarudi na spare used na screpa hivyo unatengeneza pesa mara mbili yake

Ndugu zangu Watanzania, tusisubiri kuletewa fursa kiganjani. Nawausia tutumie fursa hii maana Tanzania na Comoro ni saa moja na nusu kwa ndege. Vile vile tuna uhusiano mzuri wa Kibiashara na Comoro. Hata Bank yetu ya Exim Tanzania imefungua Branch Comoro.

Historia ya Tanzania na Comoro inatueleza kuwa Tanzania tuliwasaidia sana Comoro kupata uhuru wao pia hata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwaka 2008 Tanzania ilimsaidia sana Rais wa Comoro kurudishwa madarakan maana wanajeshi wetu walitumika kuzima mapinduzi hayo. Hivyo basi, niwaombe tuamke tuchangamkie fursa maana zipo fursa nyingi mnooo na tuna maelewano mazuri na nchi ya Comoro.

Tutumie changamoto zilizopo katika uchumi wa nchi jirani ili tufaidike nazo. Je tunawezaje kugeuza changamoto kuwa fursa?

Kuhusu Comoros
Comoro ina idadi ya watu 770,000 na Mji mkuu wao ni Moroni. Lugha zinazozungumzwa ni Comorian (Kiswahili cha Comoro, lugha ya Kibantu), Kifaransa, na Kiarabu. Uislamu ni dini rasmi ya nchi, 98% ya idadi ya watu ni Waislamu wa Sunni.

Asanteni sana na weekend njema

Abdulsamad Abdulrahim
Mwenyekiti wa ATOGS
 
Jan 16, 2020
18
45
Fursa za Biashara ziliopo Moroni nchini Comoro

Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda nchini Comoro kufanya visual assessment ya fursa ziliopo kule lakini vile vile kuzungumza na wafanyabiashara wanaokuja Tanzania kununua bidhaa na kufanya biashara nchini.

Ndugu zangu Watanzania, Comoro kuna fursa nyingi kwa Watanzania hasa wenye nguvu kiuchumi na zipo fursa nyingi kwa wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.
Mwandishi tunahitaji mawasiliano yako ...!
 
Tareq20

Member
Mar 22, 2017
24
45
Fursa za Biashara ziliopo Moroni nchini Comoro

Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda nchini Comoro kufanya visual assessment ya fursa ziliopo kule lakini vile vile kuzungumza na wafanyabiashara wanaokuja Tanzania kununua bidhaa na kufanya biashara nchini.
Non

Hospital bora pia inaeza kuwa fursa nzur sanaa kwa comoro nimefanya kazi aga Khan nimeona wateja wengi wanatoka comoro kuja tanzania kupata matibabu hasa cancer cases
 
Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,153
2,000
Wakenya na wanaijeria wakiona huu uzi watakazana sana huko.

Nasikitika sababu sisi tutaenda wakati nafasi zimeisha,watu wasioenda na muda au wazee wa kulalamika.

Mleta mada hongera sana
 
Premij canoon

JF-Expert Member
May 27, 2018
465
1,000
Nyie watu mnaoulizia namba ya mleta uzi kwa lengo la kumuuliza maswali kwanini msiulize hapa hapa jukwaani?! Acheni uswahili, mleta uzi kaileta taatifa hapa julwaani na sio huko kwenye namba ya simu. Ulizeni hapa hayo maswali ili kuepusha usumbufu wa kurudiwa kwa maswali.q
 
Said S Yande

Verified Member
Mar 16, 2013
677
500
Fursa za Biashara ziliopo Moroni nchini Comoro

Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda nchini Comoro kufanya visual assessment ya fursa ziliopo kule lakini vile vile kuzungumza na wafanyabiashara wanaokuja Tanzania kununua bidhaa na kufanya biashara nchini.
Asante kwa taarifa brother
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,767
2,000
Fursa za Biashara ziliopo Moroni nchini Comoro

Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda nchini Comoro kufanya visual assessment ya fursa ziliopo kule lakini vile vile kuzungumza na wafanyabiashara wanaokuja Tanzania kununua bidhaa na kufanya biashara nchini.

Ndugu zangu Watanzania, Comoro kuna fursa nyingi kwa Watanzania hasa wenye nguvu kiuchumi na zipo fursa
Kwahiyo hao watu 770,000 wacomoro wenyewe wanajishughulisha na nini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom