Mtanzania mwenzangu kwanini unampenda rais wa marekani obama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania mwenzangu kwanini unampenda rais wa marekani obama?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Teamo, Feb 19, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Waheshimiwa wanajamii.Nadhani ninauliza swali ambalo pengine tulio wengi tunaona kama LIMEPITWA NA MUDA.

  Ninaomba ridhaa yenu turudi hatua chache kidogo nyuma,ingawa tutachelewa.Ninapenda tujaribu kuzifanyia tathmini hisia zetu.

  Wewe MTANZANIA,naomba uniambie kwa nini ulimpenda sana au pengine bado unampenda sana rais wa marekani bwana Obama?Kuna wengine tulinunua hadi t-shirts na kofia zenye nembo yake.

  Naomba sababu ya msingi sana UKIWA KAMA MTANZANIA!unadhani obama unampenda kwa sababu zipi?????
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  binafsi ninamhusudu sana KAKA OBAMA. huyu jamaa ni bonge ya role model kwani ameonyesha rangi ya mtu si kikwazo cha kufikiaq mafanikio kwa ajili ya watu.

  ninaendelea kumfatilia kwa karibu na kumuombea afikie mafanikio ya uongozi. ameonyesha hasa kwetu sisi WEUSI kwamba sky is the limit!!!!!!!

  kwa viongozi wa kiafrika anatufundisha umuhimu wa kutambua majukumu yao kwa manufaa ya watu wao.
  akisettle na uchumi wake huenda akatoa SOMO ZURI KWA WATAWALA WA KIAFRIKA. Huyu mdudu wa kuiba rasilimali za wananchi na kombe la msaada atasidia kuwaelimisha ubaya wa kuacha na kufungua ukurasa mpya.

  THE GUY IS HOT!!!!!!!!! GO GO OBAMA!!!!
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi nilimpenda kipindi kile cha uchaguzi, just kujifariji tu na kupunguza machungu ya maisha ili siku zisogee. Yaani kwa ufupi, nilimshabikia tu kama ambavyo ninaishabikia Chelsea ya London kule Uingereza kila inapocheza, mpira ukiisha narudi home na kukuta masaa yamesogea. Inakuwa usiku inakuwa mchana, siku imeenda !!
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mswahili aliyefika mwezini, against all odds!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Feb 19, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Watu wanampenda Obama kwa sababu atatatua matatizo yote
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wengina wanampenda kwasababu ana asili ya kenya
   
 7. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I know nothing about American politics, I just like the man coz he is handsome, his life's journey is a source of inspiration and his speech gave me goose bumps on the night of nov 4th '08.
   
 8. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Nampenda sababu namuona kama ishara ya ushindi/mageuzi katika maeneo mbalimbali kwa mfano ni ile ya kuwa mtu mweusi na kuchaguliwa kuwa raisi wa marekani hili la kupigiwa mfano dunia nzima, hata bongo unapofika uchaguzi utasikia ubaguzi unaanza kama sio dini basi rangi kama alivyopigwa chini Salim A. lakini america mtu ambaye si lolote wal chochote anaweza kuwa mtu mkubwa.

  Pili jamaa anaweza na anjiamini kinoma na hakuwa na kashfa yeyote wakati bongo hapa hakuna mtu wa namna yake utatafuta sana hupati.

  Sera zake ni tofauti na mtangulizi wake, watu wengi tunalazimika kumpenda sababu ni mbadala wa george bush, hatutaki vita na tumechoka kuona watu wasio na hatia wakiuwawa na wanajeshi wa marekani kwa sababu yeyote ile kitendo ch obama kutambua kilio chetu mwana wane tutampenda lazima.

  Historia yake na jina lake,tena kukubalika U.S inaonyesha the guy is smarter na competent enough kila angependa kuona anahusika nae.

  Mwisho ameongeza thamani na muonekano wa mwafrika na mtu mweusi duniani kwa ujumla na tunatembea vifua mbele popote
   
 9. k

  katoto Member

  #9
  Feb 20, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  I like him for his brightness, eloquence and for living up to his dreams
   
 10. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mmmmm!Tafakari halafu changanua vizuri,haya unayo ongea una uhakika nayo?Pole

   
 11. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Bunafsi namkubali Obama kwani ameweza kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakuna kisichowezekana. Nadhani hatua inayofuata na waafrika kubeba Kombe la Dunia la mpira wa miguu.(Soka)
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni handsome kama JK, au mnasemaje wadau................... lol!
   
 13. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Oh,handsome,everybody is handsome.By the way how does that help you? As to his success in life,it is surely not of his own making!It was planned,organized and implemented by the Illuminati.Unfortunately you guys don't want to read,this is an open secret!And his speech,it 'sounded" great yes,but was actually nothing but another orchestrated illusion to confuse the unsuspecting including you!


   
 14. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #14
  Feb 20, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Obama is clever. Watu waliosoma Harvard wanayo reputation ya kuwa clever. Harvard is one of The Big Four Universities of The USA.
  Halafu Obama anatoka Kenya,ambayo ni East Africa, au kama utamwamini Prof Sarungi, grandparents wa Obama wanatoka Rorya.
  What we do here in East Africa is very important kwake yeye,to enhance his reputation. Na watu wa Kenya ni very clever. Inasemekana kwamba IQ za watu wa Kenya zinafananafanana na IQ za nchi zilizoendelea.
  Obama is clever. Kazi ya Rais ni kutuambia tufanye nini.Huyu Obama ni Rais wa Dunia. Katika kazi yake he has more reources,in terms of experts he can employ,kwa hiyo he is better able to help us. Kama tukiweza kumsikiliza na labda kufaidika na hekima zake,this will be good. Jana saa tano usiku nilikuwa namsikilza katika ile Press Conference na Canadian Prime Minister Harper,safari yake ya kwanza out of the United States.
  He spoke very. The man is speaking like a Messiah. Of course he is not The Messiah. Lakini watu wamemchangamkia Obama. They should not be discouraged. In the end,they will save themselves,they cannot be saved by anyone else. Lakini any enthusiasm they have for anything makes them work harder.
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkulu Tikeraa.
  Nina uhakika sana na hayo ninayoyaamini kuhusu jamaa OBAMA.

  Kama umemfuatilia kwa karibu jamaa yuko smarter!!! na kwa hawa viongozi wa kiafrika nina imani siku atakayokutana nao pamoja na usugu wao wa kutokuelewa atawaachia funzo kwa utawala ni kwa ajili ya watu. ni mzaliwa wa KENYA anaongoza the most powerful nation on earth politically and economically.

  hotuba zake zipo very consistency kuhusu anachokiamini na hayo ndiyo malengo yake.
  afterall ushindi wake kwa rangi nyeusi ni UKOMBOZI WA KIFIKRA NA KIUTENDAJI.

  Stay tuned!!!!!
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pamoja na maelezo mengi na mtazamo finyu kwamba others don't read but probably only you umenithibitishia kitu kimoja. Na if this was an exam ungechomoka na sufuri I mean 0.00000.

  Kumbuka thread inasemaje/ inaulizaje

  "Mtanzania mwenzangu kwanini unampenda rais wa marekani obama?"
   
 17. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Press conference ya jana Canada binafsi niliifuatilia jamaa yupo eloquent kishenziii
  nimejiuliza kwa nn viongozi wetu hawaongei kwa authoity with statistic well documented kuhusu maendeleo na changamoto zetu.

  jamaa anaielezea marekani yenye watu 300m, 51states, kama kuelezea duka la jumla la vinywaji!!!!

  sijawahi kumsikia mkuu hapa akichambua hii nchi by sectors kama elimu au afya kwamba kwa mikoa 21, wilaya 113, tarafa .....watu .....watapata huduma ya walimu, madarasa, wauguzi, na zitachochea ajira kiasi fulani, pato... na bajeti tulotenga inauwezo wa kufanya kiasi hiki???????

  jamani presidency si taasisi na mkulu ana watu kibao wakumpa mambooooo??? TUJIFUNZE HAPA...
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  So John Kerry, David Ax, Michele Obama etc. are illuminati? The problem with guys like you ni kwamba huwa mnarukia jambo linapokuwa tayari obvious ( He is gonna win). Na mkisoma vijiarticle vya 2 pages then you think you are pundits or news analysts I should say.

  Nakushauri upitie vizuri hayo maandiko yako It is likely hukuelewa maana kama unashindwa kuelewa kijiswali cha one sentence. What will then b for a paragraph?
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280

  Duuh..sio mchezo!! Umenifurahisha sana mkuu. Unanikumbusha hatari ya kufanya mambo kwa mazoea
   
 20. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hili ni swali muhimu sana. Kimsingi ushabiki juu ya viongozi unapaswa kuwa juu ya sera zao na tathimini ya yale waliyotenda kabla ya kugombea nafasi fulani pamoja na uhalisia wa sera wanazo zipropagate. Suala la uhandsome, colour, etc hayana tija kwa kiongozi wa nchi bali katika 'model' industry. Mi naomba pia nikurudishe nyumbani kidogo. Kikwete alipendwa kuliko maelezo wakati anagombea kiasi cha kushawishi wananchi kuwachagua hata wabunge waliokuwa wamechokwa na wananchi. Lakini ukiuliza watanzania walimpendea nini unaweza ukakosa jibu la msingi.

  Binafsi nina ushabiki wa siasa za kidunia. Hivyo huwa ninamtazamo wangu tofauti ninapotizame wanasiasa wa marekani kwani wanaimpact kubwa sana katika dunia yetu (mnaweza bisha) lakini huo ndio ukweli. Nadhani, hili liwe somo kwa watanzania juu ya ushabiki kwa viongozi hata hapo kwetu TZ
   
Loading...