Mtanzania la leo 30/1/2010

Mtanzania la leo 30/1/2010

Amina Thomas

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2008
Posts
272
Reaction score
130
jamani mmeliona mtanzania la leo? hivi rostam ameamua kugeuka au si mmiliki wa gazeti hilo kuanzia leo?
 
Si RA ni Bashe na waandishi wake, Bashe ameamua kutaka kufanya biashara kama CEO wa New Habari, RA aliwatosa akawa hawapi pesa wajiendeshe huku anawapa maagizo ya habari, sasa wameamua kuangalia soko ili wajilipe na walipe madeni
 
hebu fafanueni vizuri nini kimejiri kwenye hilo gazeti, wengine tuko safarini jamani na kwenye net hatulipati hilo gazeti
 
Mhh!!! Lakini bado RA akitaka lake liandikwe huandikwa bila pingamizi kutoka kwa Bashe au yeyote. Wako Balile na Mayage wanoendelea kulamba viatu vya RA.

Mfano, RA akitaka lake liandikwe basi hutuma Headline tu na vibwagizo -- na kutoa agizo kwa mhariri (balile au Mayage) aandike/atunge stori kufuatana na headline na vibwagizo hivyo.

Mfano anaweza kutoa Headline 'Imedhihirika wa kulaumiwa malipo ya Dowans ni Sitta' basi ni lazima stori itafutwe au itungwe kufuatana na headline hiyo.

Kuna uandishi wa kiajabu ajabu sana pale New Habari na sijui Baraza la Habari linalijua hili.
 
jamani si muweke hicho kilichoandikwa hili na sisi tuliombali na upeo wa hilo gazeti tuweze kuona
 
gazet la mtanzania na mengine yote yaliyo chini ya rostam hayafai kusomwa na Watanzania! hata wajikoshe namna gani hatuyanunui, hatuwezi kuendelea kumuongezea huyo fisadi fedha zetu.
wanao anzisha thread za namna hii wanataka kukupandisha mori ili ilinunue gazeti lao!
 
ameniudhi kweli..kama hutaki tujue kilichoandikwa si ukae kimya? au na mimi nisipokueleza kilichomtokea JK kule davos utajisikiaje/?
 
Headline yao kubwa inasema hivi:

Kikwete mambo mazito
  • Makundi CCM, bungeni, serikalini yamuumiza kichwa
  • Upepo wa siasa wavuruga utendaji, washusha uchumi
  • Lowassa asema ajira ni bomu linalosubiri kulipuka
Stori ya pili inasema:

... Askofu Nzigilwa amvaa
  • Asema kimya chake kinashangaza
  • Ahofia uvumilivy kutoweka nchini
 
kama hutaki basi. ila heading kama 'kikwete mambo mazito'! askofu nzigilwa amvaa'! sio za kawaida kwa gazeti mtanzani
 
Mhh!!! Lakini bado RA akitaka lake liandikwe huandikwa bila pingamizi kutoka kwa Bashe au yeyote. Wako Balile na Mayage wanoendelea kulamba viatu vya RA.

Mfano, RA akitaka lake liandikwe basi hutuma Headline tu na vibwagizo -- na kutoa agizo kwa mhariri (balile au Mayage) aandike/atunge stori kufuatana na headline na vibwagizo hivyo.

Mfano anaweza kutoa Headline 'Imedhihirika wa kulaumiwa malipo ya Dowans ni Sitta' basi ni lazima stori itafutwe au itungwe kufuatana na headline hiyo.

Kuna uandishi wa kiajabu ajabu sana pale New Habari na sijui Baraza la Habari linalijua hili.

Hapa Tanzania Rostam Aziz ana uwezo wa kuamua lolote lile. Kama tukitaka kuwa na uandishi wa habari professional tumuombe Rostam, tukitaka ufisadi uishie tumuombe Rostam. Ni mtu pekee mwenye nguvu za kuweza kufanya hayo Tanzania. Baraza la habari ni bendera tu.
 
Mhh!!! Lakini bado RA akitaka lake liandikwe huandikwa bila pingamizi kutoka kwa Bashe au yeyote. Wako Balile na Mayage wanoendelea kulamba viatu vya RA.

Mfano, RA akitaka lake liandikwe basi hutuma Headline tu na vibwagizo -- na kutoa agizo kwa mhariri (balile au Mayage) aandike/atunge stori kufuatana na headline na vibwagizo hivyo.

Mfano anaweza kutoa Headline 'Imedhihirika wa kulaumiwa malipo ya Dowans ni Sitta' basi ni lazima stori itafutwe au itungwe kufuatana na headline hiyo.

Kuna uandishi wa kiajabu ajabu sana pale New Habari na sijui Baraza la Habari linalijua hili.

Ningekuwa na uwezo ningefutilia mbali vigazeti vya aina hii.
 
Competition ni kubwa siku hizi na walikuwa washasomeka kama Gazeti la Rostam,not even la chama,ni lazima wabadilike nafurahi wameona umuhimu wa kubadilika kabla hajabaki Rostam mwenyewe wa kununua hilo gazeti:coffee:
 
We should take care anyway. Mara chache ambazo nimeona wanaandika hbr neutral, ni kuwa cku 2 au 3 baadae wanafyatuka na stor kubwa ya uchochezi, ama udini au kuichafua cdm. So wanafanya kama vile kujikosha kwanza ili wakitoa hy stor, ionekane kama nayo ni neutral.
 
I agree with you....:coffee:
 
ameniudhi kweli..kama hutaki tujue kilichoandikwa si ukae kimya? au na mimi nisipokueleza kilichomtokea JK kule davos utajisikiaje/?

come down. Tujuze yaliyompata jk huko davos. Natamani nisikie kaamua kubaki huko huko!
 
Competition ni kubwa siku hizi na walikuwa washasomeka kama Gazeti la Rostam,not even la chama,ni lazima wabadilike nafurahi wameona umuhimu wa kubadilika kabla hajabaki Rostam mwenyewe wa kununua hilo gazeti:coffee:

Nakubali Michelle, lakini trust katika biashara hasa ya habari kwa zama hizi ni kitu kigumu kupata kwa chapisho moja moja tu. Nadhani watahitaji muda mrefu wa kujisafisha hadi watu kurudisha trust kwamba hii mara moja moja siyo marketing strategy. Mimi binafsi itamichukua muda sana. Afterall habari za uhakika zinapatikana sources mbalimbali, why gamble with RA?

Kitu kimoja RA anastahili sifa kutoka moyoni kwangu. Amefanikiwa kuwafanya watanzania kusoma habari kwa mashaka kwamba isijekuwa ya kupikwa. Miaka ya nyuma watz walikua wanaamini kila kilichochapishwa na vyombo vya habari 100%. pia amefanya watz kujua namna ya kuamua watumie pesa yao kununua gazeti gani, hata kama kichwa cha habari hakivutii kama mengine. Awali tulikuwa tunakimbilia the most sensational headline.
 
gazet la mtanzania na mengine yote yaliyo chini ya rostam hayafai kusomwa na Watanzania! hata wajikoshe namna gani hatuyanunui, hatuwezi kuendelea kumuongezea huyo fisadi fedha zetu.
wanao anzisha thread za namna hii wanataka kukupandisha mori ili ilinunue gazeti lao!

Nilikuwa mpenzi wa Rai kweli lakini tangu limeenda kwa Rost tamu sina hamu nalo kabisaaa!!!!!!! Na sijui haka kazee nako kwa nini kaliuza magazeti yake!! Yaani sasa hivi kusoma hayo magazeti inahitaji moyo!! Jamani tumsusieni magazeti yake ili kampuni imfie mikononi!!
 
Headline yao kubwa inasema hivi:

Kikwete mambo mazito

Stori ya pili inasema:

... Askofu Nzigilwa amvaa

ameniudhi kweli..kama hutaki tujue kilichoandikwa si ukae kimya? au na mimi nisipokueleza kilichomtokea JK kule davos utajisikiaje/?

Haya sasa ni zamu yako kutuambia nini kimemtokea JK.........
 
Back
Top Bottom