Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 61,023
- 36,875
Bwana ametoa, Bwana ametwaa
Wakati nipo njiani nampeleka mtoto hospitali ya TMJ baada ya kupata homa kidogo,sasa wakati tunakaribia kufika daraja la Mlalakuwa nikaona walinzi wa Royal Oven pale Kawe wakiwa wamelazwa chini.Tulipita darajani kwa mwendo wa kasi sana bila kutoa msaada.
Wakati tunarudi baada ya kumaliza matibabu tukamkuta RPC na wenzake wakiomboleza vijana wamepiga kazi,na pembeni tukaona gari aina ya Toyota Noah imezungukwa pembeni kuna tobo la risasi.
Chini ya gari hilo kulikuwa na damu nzito,kumbe kuna mtu kauawa muda mchache uliopita wakati akinunua vitafunwa..
Sina cha kusema zaidi ya kumwachia Mungu tu ajuaye.