Mtanzania afariki Denmark nduguze wanatafutwa

mtz one

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
4,275
Reaction score
1,226
Ndugu wanabodi mwana husika na kichwa cha habari hapo juu,

UPDATES ZA MTANZANIA MWENZETU ALIYEFARIKI MPAKA SASA:

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze kuhudhuria mazishi yake.
 
Inshaalah soon nitaanza kumuona balozi watu wasikose picha yangu pia.
 
Poleni wafiwa wote..huko Denmark hakuna ubalozi wa Tanzania? nchi nyingine zinajali sana raia wake hata kama ni mmoja mfano Israel,Marekani n.k
 
''BREAKING NEWS''

UPDATES ZA MTANZANIA MWENZETU ALIYEFARIKI MPAKA SASA:

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze kuhudhuria mazishi yake.
 
Kweli jamani hebu jaribuni kwenye ubalozi wa nchi yetu huko mliko.
 
Watanzania wa Denmark fanyeni kumstiri mumzike wenyewe asizikwe na manispaa.
 
hua sijumuiki na watu kabisa japo najua ni tatizo nakua mmbishi tu

Ila mwaka ujao inshaalah nitaanza kumuona balozi kwanza watu wasiseme hawanijui
Kuwa mwangalifu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom