Muhimu kwa Watanzania waishio Denmark

Muhimu kwa Watanzania waishio Denmark

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,063
Reaction score
47,048
MTANZANIA ALIYEFARIKI NCHINI DENMARK.

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze kuhudhuria mazishi yake.

#NOTE; Sambaza ujumbe huu, lakini pia uwe fundisho kwa watu wanaoishi nje bila CONNECTION na ndugu zao nyumbani au hata watu wa taifa lao huko nje.
Mtatiro J
 
Taarifa muhimu sana mmetoa watu wa Denmark, je hamuwezi kulipia tangazo la kifo TBC na Redio One kule home? Sijaona mkigusia ubalozi uliopo Sweden wamefanya nini kucheki na ukoo wa Asheli , kuna kijana yuko active sana pale Ubalozi Sweden siwezi mtaja jina hapa huwa akija sana kwenye hafla zetu
huyu kijana mstaarab sana na ni msaada mkubwa kwa watanzania waishio nordic na baltic countries.
 
TUNASHUKURU WOTE MLIOFANIKISHA MAZISHI YA UNCLE SAMUEL JOHN ASHERY.....NIPO TANZANIA....PIA TUNATAKA KUJUA KUHUSU MTOTO WAKE ALIYE DENMARK ..NA ITALY YEYOTE MWENYE TAARIFA SAHIHI....WHATSAP YANGU NI +255717920488.
 
MTANZANIA ALIYEFARIKI NCHINI DENMARK.

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze kuhudhuria mazishi yake.

#NOTE; Sambaza ujumbe huu, lakini pia uwe fundisho kwa watu wanaoishi nje bila CONNECTION na ndugu zao nyumbani au hata watu wa taifa lao huko nje.
Mtatiro J
Mtatiro j ndo kafariki au?
 
Back
Top Bottom