Nakapanya
JF-Expert Member
- May 22, 2012
- 2,096
- 709
Mtani jembe inaendelea kama kawa,watu wanazidi kuhamisha mipesa wenyewe wanasema unawaibia wapinzani.Mwanzoni mwa zoezi hili Simba walionekana kuiba pesa nyingi sana kutoka Yanga kwani mashabiki wao walikuwa wakituma sana sma kwa utaratibu uliowekwa,cha kushangaza hadi leo hii matokeo yanaonyesha Yanga wamewapiga bao kubwa Simba kwani wanaongoza kwa mbali sana.
Matokeo yenyewe yansomeka hivi:-
42,990,00 57,010,000
SIMBA YANGA
Kwa matokeo hayo ya hadi leo inaonyesha simba bado wanaendelea kuwa mdebwedo katika kila jambo,maneno meengii kama mwenyekiti wao halafu vitendo sifuri,usajili mnapigwa bao,hata hili pia mnapigwa baoo.....hahaaaa....Simbaaaa