Mtangazaji wa 360 Clouds TV, Hassan Ngoma aitaka Bodi ya Mikopo isiwakopeshe Watanzania Masikini

Tomito Tomato

Senior Member
Feb 11, 2017
167
444
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa mtangazaji wa Kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha Clouds tv Bwana Hassan Ngoma asubuhi hii wakati akichangia mawazo yake juu ya Sheria mpya za mikopo kwa Wanaufunzi wa Vyuo Vikuu alisema kwamba Watoto wa Masikini wasikopeshwe.

Mtangazaji huyo ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akiingia sana matatani hasa kwa Wasikilizaji mbalimbali hasa kutokana na Kauli zake ambazo nyingi zina harufu ya dharau, sanifu na kejeli alienda mbali na kusema kwamba Bodi ya Mikopo badala yake ingekuwa inajikita mno kuwakopesha Watoto wa Matajiri kwani mwishoni huwa na uwezo wa kulipa kuliko Watoto wa Masikini ambao ulipaji wao ni haba na wa kuunga unga huku wakiwa na shida kibao.

" Mimi siafiki kabisa huu mfumo mpya wa Bodi ya Mikopo nchini HESLB wa kuwaacha Watoto wa Matajiri au wale wanaojiweza kidogo Kiuchumi na kung'ang'ania kuwakopesha tu Watoto wa Masikini ambao kiukweli wamejaa shida nyingi, hawaajiriki haraka na wengi wao hata maisha yao ni ya kuunga unga mno hali ambayo itaichelewesha Bodi kukusanya mapato yake haraka ili kuweza kusaidia Watoto wengine " alisema mtangazaji Hassan Ngoma.

Ikumbukwe tu kuwa ni jana tu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini HESLB imekuja na utaratibu mpya wa Mwanafunzi kupata mkopo ambapo kwa sasa wale Watoto ambao wanatoka katika zile Familia zenye uwezo mkubwa na zile zenye uwezo wa kati hawatapata mikopo isipokuwa mikopo ya sasa itatoka tu kwa Wanafunzi wanaotoka hasa katika Familia duni au za Kimasikini.
 
" Mimi siafiki kabisa huu mfumo mpya wa Bodi ya Mikopo nchini HESLB wa kuwaacha Watoto wa Matajiri au wale wanaojiweza kidogo Kiuchumi na kung'ang'ani kuwakopesha tu Watoto wa Masikini ambao kiukweli wamejaa shida nyingi, hawaajiriki haraka na wengi wao hata maisha yao ni ya kuunga unga mno hali ambayo itaichelewesha Bodi kukusanya mapato yake haraka ili kuweza kusaidia Watoto wengine " alisema mtangazaji Hassan Ngoma.

OMG
Hata aibu hana DUH!!!!
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa mtangazaji wa Kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha Clouds tv Bwana Hassan Ngoma asubuhi hii wakati akichangia mawazo yake juu ya Sheria mpya za mikopo kwa Wanaufunzi wa Vyuo Vikuu alisema kwamba Watoto wa Masikini wasikopeshwe.

Mtangazaji huyo ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akiingia sana matatani hasa kwa Wasikilizaji mbalimbali hasa kutokana na Kauli zake ambazo nyingi zina harufu ya dharau, sanifu na kejeli alienda mbali na kusema kwamba Bodi ya Mikopo badala yake ingekuwa inajikita mno kuwakopesha Watoto wa Matajiri kwani mwishoni huwa na uwezo wa kulipa kuliko Watoto wa Masikini ambao ulipaji wao ni haba na wa kuunga unga huku wakiwa na shida kibao.

" Mimi siafiki kabisa huu mfumo mpya wa Bodi ya Mikopo nchini HESLB wa kuwaacha Watoto wa Matajiri au wale wanaojiweza kidogo Kiuchumi na kung'ang'ani kuwakopesha tu Watoto wa Masikini ambao kiukweli wamejaa shida nyingi, hawaajiriki haraka na wengi wao hata maisha yao ni ya kuunga unga mno hali ambayo itaichelewesha Bodi kukusanya mapato yake haraka ili kuweza kusaidia Watoto wengine " alisema mtangazaji Hassan Ngoma.

Ikumbukwe tu kuwa ni jana tu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini HESLB imekuja na utaratibu mpya wa Mwanafunzi kupata mkopo ambapo kwa sasa wale Watoto ambao wanatoka katika zile Familia zenye uwezo mkubwa na zile zenye uwezo wa kati hawatapata mikopo isipokuwa mikopo ya sasa itatoka tu kwa Wanafunzi wanaotoka hasa katika Familia duni au za Kimasikini.
Mkuu watu wengi Sana ambao wako Kwenye utumwa wa kifkra basi wapatapo nafasi fulani fulani huwa na dharau sana....ukimchunguza huyo mtangazaji usishangae kukuta kwamba chimbuko lake ni sawa tu na hao anaowadharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom