TANZIA Mtangazaji Maarufu wa RTD Abissay Stephen amefariki dunia asubuhi hii

Buriani Kamanda. Nikiripoti hapa Mbeya mimi ni Abbysai Steven wa Radio Tanzania, enzi zile za kipindi cha majira RTD saa Tatu usiku.
 
TBC wametoa update kwenye taarifa yao ya habari ya saa 2 usiku.

Marehemu atazikwa kijijini kwao Hai mkoani Kilimanjaro siku ya Jumanne.

Heshima za Mwisho ni Jumatatu saa 4 asubuhi nyumbani kwake Temeke Mikoroshoni na baadae kusaliwa Kanisa la KKKT Temeke Vetenari.

Abysai Steven alizaliwa mwaka 1951 huko Moshi. Aliajiriwa na RTD mwaka 1970 kama Mtangazaji Msaidizi Daraja la III. Alipanda ngazi mpaka mauti yalipomkuta akiwa ni Mtangazaji Mwandamizi Mkuu Daraja la I.

Marehemu ameacha mjane, watoto 3 na mjukuu 1.

Rip Abysai Stephen.
 
Huyu ni mwandishi mahiri kabisa , may he RIP , its unfortunate sijasikiliza radio TZ muda sasa, hazina hizi za waandishi aina yake ni very rare
 
UPDATE 3.
Msiba umehamishiwa kwenye nyumba yake nyingine iliyoko Banana Kitunda.
Ili kupunguza mahangaiko, mwili wa marehemu utatoka hospitali ya Muhimbili saa 5 asubuhi moja kwa moja kanisa la KKKT Vetenari kwa misa na heshima za mwisho.
Baada ya hapo, safari ya kuelekea Hai, Moshi Kilimanjaro kwa mazishi, itaanza.
 
Watangazaji wa maana wote wanaisha, wanabaki maDJ's tu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe, pumzika kwa amani Steven!
 
UPDATE:3.
Heshima za mwisho kwa Abysai Stephen zimemalizika hapa kanisa la KKKT Vetenary Temeke ambazo zimehudhuriwa na record ya umati wa watu kwa mtangazaji wa RTD.

Umati huo umejumuisha viongozi wa vyama na serikali, wafanyakazi wa TBC, waandishi na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari na kukolezwa na idadi kubwa ya watangazaji wakongwe wa iliyokuwa RTD.
Msafara kuelekea Hai Kilimanjaro umeanza.

RIP A.S
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom