Mtanganyika (Mtanzania bara) anaweza kugombea ubunge Zanzibar? Katiba inasemaje?

Dr Hussein Mwinyi amekuwa mbunge kwa miaka kadhaa kupitia jimbo mojawapo mkoani Pwani (Mkuranga nadhani).
Sasa hivi ni mbunge wa jimbo fulani hapa Unguja.
Nadhani sasa swali haliwezi kuwa kama anaruhusiwa ama la.
 
Dr Hussein Mwinyi amekuwa mbunge kwa miaka kadhaa kupitia jimbo mojawapo mkoani Pwani (Mkuranga nadhani).
Sasa hivi ni mbunge wa jimbo fulani hapa Unguja.
Nadhani sasa swali haliwezi kuwa kama anaruhusiwa ama la.

Kuna mengi ya kujiuliza! Dr Hussein Mwinyi ana sifa ya uzanzibar mkazi kama alikuwa mbunge bara kabla hajaenda Zanzibar basi hakuwa na sifa ya uzanzibar mkazi
 
Mimi sina uhakika sheria inasemaje, lakini hili litaweka doa sana kwenye huu muungano wetu iwapo kutakuwa na pingamizi. Na kama cdm wataweza kutumia vizuri iwapo pingamizi litawekwa basi itakuwa ni kete muhimu ya kuhalilisha kuuvunja muungano. Siku za nyuma Hussein Mwingi aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga kama sijakosea, lakini yeye anatambulika kama Mzanzibar na kuna hadithi za chini ya pazia huenda akapewa nafasi ya kugombea urais Znz baada ya Dr. Shein. Yote kwa yote hili litasababisha maswali ya kutosha kuhusu muungano na huenda watakaocheza kete hiyo ikaja kuwaumiza sana huko mbeleni. Hapa pia mbegu ya ubaguzi wa kikabila inaweza kuchochewa tusipokuwa makini.
Tindo mungu akubariki sana mkuu. Mzee mwinyi alikulia hku bara. Alikuja kuwa raisi wa zanzibar kisha jmt. Mtto wa mwinyi leo ni wazir wa ulinzi ila anatokea unguja. Wazir mbarawa huyu anatokea unguja na ni waziri.timdo muungano mgumu huu
 
Kwani huwezi kujadili hoja tu bila kuweka u ccm au kumshutumu mtu? Mi naona una hoja nzuri lakini unaziharibu kwa kuingiza kushutumiana baada ya kuelimisha.

Ungeweza kusema tu binge in LA jmt na ccm kwa kuwa ipo madarakani hawatapenda hilo jambo lijadiliwe kwani litawaumiza kwa one two three.

Naamini ukiwa unajadili nna hiyo itakujenga kwani hats ukienda katika mijadala isiyotaka use ccm au chadema utajadili kirahisi. Ushauri tu!
Ushauri bora kabisa, kuna watu nje ya Ccm na Cdm kisiasa hawana hoja kabisa. Sijui hawajui kwamba kuna tabaka neutral ktk hii nchi, nadhani hawawezi hata kuli convince hili tabaka.
 
Wataalamu wa sheria na katiba naomba mnijulishe. Hivi Mtanganyika, yaani Mtanzania bara anaweza kugombea ubunge Zanzibar? Sheria imekaaje?

Vipi Mzanzibari anaweza kugombea ubunge Tanzania bara? Hapa napo sheria na katiba inasemaje?

Wenye weledi tafadhali.
Dhambi ya ubaguzi na ikutagune wewe na uzao wako popote ulipo.
 
Kama tutajikita kujadili taratibu halali za kisheria na tukazifahamu uzuri itakuwa rahisi kuyaona mengine yalitendekaje. Sio kila muda no kubishana kihisia kutokanako na itikadi, wakati mwingine maarifa yashike hatamu tupate faida kubwa
Halafu kuna muungwana hapo juu alishalijibu, kwamba Ubunge ni wa Tanzania. Hata ufanyike ktk majimbo ya upande wa pili, sheria na taratibu zote na hata utararatibu wa usimamizi wake. Kwahiyo, sheria ni ileile imuwezeshayo mpare ama mchaga ama msukuma kuwa Mbunge wa Kinondoni ama Ukonga.
 
Mtanganyika hata kumiliki ardhi kule Zanzibar sheria inamkataza.

Mzanzibar anaruhusiwa kugombea popote kwenye ardhi ya Tanzania, ila Mtanganyika haruhusiwi kugombea Zanzibar, iwe Urais, Uwakilishi na hata ubunge.

Mtanganyika haruhusiwi kuajiriwa kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa hiyo huu Muungano umekaa kiunyonyaji zaidi.

Cha kwao chao, cha kwetu chao

Suala la ardhi hata Moshi kama sio mchaga kupata ardhi issue
 
Huu muungano unatumika kama mbeleko kwa wazanzibar, hata huyo mwalimu lazima tumjadili hata kama kuna upande utanufaika na mjadala huu.

Hawa wanatubagua watanganyika sana, aende kwao bumbwini huko akagombee. Nitawashangaa watanganyika wachache watakao mpa kura walau kwa uchache. Tusiwe wanafki wakati tunajua juzi juzi tu wametoka kutuita machogo.

Mwalimu Noooooo!
 
Kugombea ni ruksa ukiwa CCM pekee mfano wa mwana CCM aliyefanya hivyo ni HUSSEIN MWINYI.
Lakini ukigombea kupitia CDM ni haramu na utapingwa na kuitwa raia wa nchi jirani mfano ni SALUM MWALIMU
 
Serikalini ya mapinduzi Zanzibar haina wajumbe bali ina viongozi! Serikali si kamati ya chama cha siasa au bodi ya wakurugenzi au kamati za chama au kamati za bunge hadi iwe na wajumbe. Serikali huundwa na baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu tarafa na makatibu kata. Hao wote ni viongozi, si wajumbe. Kwenye Civics au DS mnasomaga nini nyie wapumbavu?

Asante, ulimi umeteleza kama kwenye kuandika kuna ulimi. Nilitaka kusema wajumbe wa baraza wawakilishi. Naomba uniwie radhi kwa mkanganyiko!
 
Wala wabara sio wabaguzi mbona kubenea alishinda??

Tatizo ni moral authority of a person to stand and asks jamii imchague wakati sio mkazi wala hajawai kuishi wala kujiandikisha kupiga kura..hana political legitimacy ya kusimama hapo kino
 
Mbona Hussein Mwinyi aliwahi kutumika kama Waziri wa afya bara enzi za JK? Na Naibu waziri wa afya bara enzi za Mkapa? Na hamkulalamika? Wizara ya afya si ya Muungano lakini Husein Mwinyi alisimamia wizara hiyo? Acheni upuuzi! Mmekosa grounds ya pingamizi kwa Mwalimu sasa mmebaki na fitnaa! Wachawi kabisa

Inawezekana ni kweli, na pia inawezekana makosa yalifanyika. Jf ipo kwa vile si kila mtu anafahamu, ni jukwaa la mijadala. Tukijifunza kujadili masuala pasipo kuingiza ukada tutafika kwa kuwa lengo letu ni moja, kuijenga Tanzania bora
 
Huu muungano una vioja. HAWEZI kugombea hata kuajiriwa serikalini hakiwezekani. Ila mbunge wa Zanzibar eg Hussein Mwinyi anaweza kuteuliwa kuwa waziri bara ila mbunge wa bara eg Mwigulu ya Chemba haiwezekani kuteuliwa kuwa waziri Znz.
Serkali ya Zanzibar kwa wa Zanzibari na Serikali ya Mungano kwa watu wote Tanzania.

Mza nzibari pekee ndiye anaye weza kufanya kazi katika Serikali ya Zanzibar na Mtanzania yeyote anafaya kazi serikali ya Muungano
 
Back
Top Bottom