Mtanganyika (Mtanzania bara) anaweza kugombea ubunge Zanzibar? Katiba inasemaje?

Tusimzungumzie Mwalimu, tuzungumzie utaratibu. Tukimzungumzia Mwalimu tutakosa maarifa kwani itikadi inaweza ikatamalaki kutoka pande hasimu pasipo kujali weledi.

Unajikosha tu mkuu....

Lakini nina hakika reference ya hoja yako ni Salim Mwalimu (mgombea wa kiti cha ubunge, jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA) ambaye asili yake ni Zanzibar....

Acha tu hoja ijadiliwe na mwenye kujenga hoja kwa kumtumia Salimu Mwalimu na uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Kinondoni, afanye hivyo na mimi kwa upande wangu sioni tatizo lolote!!
 
Hii mada ni nzuri sana, ila ngoja wakati muafaka utakapofika ndipo utaona waliojificha pangoni wakiibuka!

Nawaza hawa CDM wana maana gani kumuweka Mwalimu pale Kinondoni?

Ngoja kampeni zianze uone watu watakavyoweweseka
Haha Chadema na Maalim was wanadai hawataki muungano lakini kwenye ubunge wanataka kugombea wasikotaka,sisi wakazi wa Kinondoni hatumjui huyu Mpemba
 
Nadhani wewe sio tu bila shuka, ni zaidi ya hapo. Rais wenu? Ndio nini, wewe ni wa wapi? Eti dagaa, wewe hivi unajitambua kweli? Kagua gwaride, kwani cha ajabu ni kipi hapo? Hata wa Kenya anaweza likagua gwaride la JWTZ, je ana mamlaka ya kuliamrisha? Je,naye ni Amiri jeshi mkuu?

Mambo mengine hayahitaji ujuaji, Zanzibar sio nchi, ni sehemu tu ya JMT, full stop. Mengine yote mbwembwe tu.

Katiba ya znz inamtambua Shein ni Amir Jeshi Mkuu, Ndio maana mnahaha usiku n mchana kwa katiba ya znz, Kamuulize pinda atakujibu khs znz km nchi au sio n kithibitisho juzi tu Shein kaonesha nyie malofa n wapumbavu wote mmeufyata baada ya kupigiwa mizinga n kukagua gwaride, bisha nikiwekee video pengine kwenu hamjarejeshewa umeme n serikali yenu Ndio maana hujaona
 
Zanzibar wana marais wawili,yani rais wa nchi ya Zanzibar,na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Lakini Tanganyika au Tanzania bara wana rais mmoja tu ajulikanae kama rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Hivyo basi Zanzibar ni jamuhuri ya muungano wa Tanzania,na ndiyo maana wana haki zote ktk jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Hii mada ni nzuri sana, ila ngoja wakati muafaka utakapofika ndipo utaona waliojificha pangoni wakiibuka!

Nawaza hawa CDM wana maana gani kumuweka Mwalimu pale Kinondoni?

Ngoja kampeni zianze uone watu watakavyoweweseka
Lengo la chadema ni kutaka kuwabaini wanafiki na misukule.
 
Ili ugombee ubunge nchini Zanzibar ni lazima uwe mzanzibari,wakati Tanzania bara ili ugombee ubunge ni lazima uwe mtanzania.Hivyo basi kwakuwa kigezo cha ubunge huku bara ni lazima uwe mtanzania na ndiyo maana mzanzibari anaruhusiwa kugombea kwasababu na yeye ni mtanzania.
 
Unajikosha tu mkuu....

Lakini nina hakika reference ya hoja yako ni Salim Mwalimu (mgombea wa kiti cha ubunge, jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA) ambaye asili yake ni Zanzibar....

Acha tu hoja ijadiliwe na mwenye kujenga hoja kwa kumtumia Salimu Mwalimu na uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Kinondoni, afanye hivyo na mimi kwa upande wangu sioni tatizo lolote!!

Kweli kabisa, duniani tupo watu wa aina nyingi. Watu wa kujikosha kama mimi na watu kwenye maarifa na thabiti kabisa kama wewe. Uwepo wetu unaifanya dunia sehemu bora ya kuishi maana tunategemeana.
 
Sio kweri wapo wa Tanganyika wengi wamegombea Zanbar na ni viongozi mpaka Leo ,mfano waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi ni mzaramo wa Mkuranga lakini ni mbunge wa jimbo la Kwahani Zanzibar , alikuwepo hayati baba yake Wema balozi Issack Sepetu ni mtu wa Singida lakini alishika nyadhifa mbali mbali ktk serikali ya Smz ,na wengine wengi tu,kwhyo hoja kubwa ni uraia wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania regardless una gombea wapi ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tz
 
Mimi siko CHADEMA ila MUUNGANO HUU wa TANGANYIKA na ZANZIBARI sijawahi kuuelewa maana MTANGANYIKA ukiwa ZANZIBAR wewe ni Mtanganyika sio raia wa Zanzibar na hupati haki zote kama anazopata MZANZIBARI ila MZANZIBARI akiwa TANGANYIKA, yeye ni MTANZANIA hivyo anapata haki zote kama walivyo WATANGANYIKA.

Mimi Naona muungano huu unatupa hasara WATANGANYIKA unawapa faida kubwa WAZANZIBARI yaani kiukweli kwa muungano huu, WAZANZIBARI wanatutawala WATANGANYIKA kupitia sisi wenyewe nadhani Katiba mpya ikiija iifute ZANZIBAR kama ilivyofutwa TANGANYIKA ili wote tuwe sawa na tuwe na serikali moja ili tuijenge nchi moja yaani TANZANIA moja.

Vinginevyo, WATANGANYIKA na sisi tutaidai TANGANYIKA yetu iwepo kama ambavyo ZANZIBAR ipo ili usawa uwepo. Futeni ZANZIBAR kama mlivyoifuta TANGANYIKA wote tubaki na uraia mmoja wa TANZANIA na tuongozwe na raisi mmoja Wa serikali moja ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Wazanzibari wengi hawaupendi muungano, ndiyo maana wale jamaa wa uamsho wapo ndani hadi leo, sijamuona hata mtanzania bara mmoja mwenye kupinga muungano kama wanavyoupinga wazanzibari. Ikiwa tumekubali muungano wa serikali 2 hayo ndiyo matokeo yake. Baada ya muungano vyama vyote vya siasa vilivunjwa na kuundwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), nchi iliyofanya mapinduzi ni Zanzibar huku kwetu bara hatujapindua serikali yoyote, kwa mantiki hiyo CCM ni chama kinachowahusu sana wazanzibari.
 
Katiba inasema hivi
fc58e17cf4c81bd8bb7de63a8daf43fc.jpg
 
ukawa walikuwa wanataka serikali tatu lakini kiuhalisia walikuwa wanaongea kujifurahisha kama kweli ni waumini wa serikali tatu wasingemteua Salum mwaimu kugombea ubunge bara na kuwaweka kando watu wao wa bara
 
Ukiwa mkaazi wa Zanzibar unagombea, ila kama sio mkaazi huwezi hata piga kura.
 
Back
Top Bottom