Mtandao Wa Wezi Wa Laptop | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtandao Wa Wezi Wa Laptop

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Aug 1, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nilifanikiwa kuingilia mtandao wa wezi wa laptop pamoja na simu za mkononi mtandao huu ni mkubwa sana kuna baadhi ya watu ambao ni askari kanzu , wamiliki wa maduka ya computer na vifaa vyake pamoja na vijana wengine ambao kazi yao ni kuletewa vifaa hivi kuvibadilisha na kuuza kwa mara ya pili kwa bei chee .

  KATIKATI YA JIJI

  - DARSKENDO ( JINA LAKE KAMILI HAJULIKANI ) HATA ANAPOENDA VITUO VYA POLISI HUWA HAANDIKI JINA LAKE SIJAWEZA KUJUA NI KWA SABABU GANI , YEYE NI MWENYEJI WA MWANZA MENO YAKE KWA MBELE KAMA YAMEOZA HIVI – ANAPATIKANA MARA NYINGI MTAA WA SAMORA KARIBU NA FUNDI MMOJA MAARUFU WA SIMU ANAITWA ABDALAH JUU YA KIGOROFA PAMOJA NAYE WAKO VIJANA WENGINE 2 AMBAO NI RAFIKI ZAKE .

  - ABUBAKARI ( JINA LINGINE NI ANODI ) YEYE NI MFUPI ANANYWELE NDEFU NI MWENYEJI WA MWANANYAMALA MARA NYINGI ANAPATIKANA FERI NA HUWA ANALALA HUKO HUKO , HUYU NI MWIZI ZAIDI WA SIMU ZA VIGANJA .

  - COMPTRONIX ( HILI NI DUKA MAARUFU KWA UUZAJI WA VIFAA YA ELECTRONIKI NA COMPUTER ) LIKO SAMORA PIA , UKIFIKA HAPA UTAONA VITU NI BEI RAHISI SANA KAMA LAPTOP NA VINGINE WENGI WANAOIBA LAPTOP HUENDA KUUZA KATIKA DUKA HILI KWA BEI ZA KUTUPA KWAHIYO USISHANGAE LAPTOP YAKO IMEIBIWA UKAENDA KUUZIWA TENA KATIKA COMTRONIKX.

  JAMHURI - AZAM TAKE AWAY ( HAPA KUNA WATU WENGI WANAOJISHUGULISHA NA UUZAJI NA UNUNUZI WA LAPTOPS HATA SIMU ZA MIKONONI , WENGI HUJIFANYA ZIMETOKA NJE YA NCHI HASWA AFRIKA YA KUSINI NA ULAYA MMOJA WA WATU MAARUFU WANAOUZA HIZI LAPTOP NI TOM ( HILI SIO JINA HALISI ) ILA NDIO JINA ANALOTUMIA PAMOJA NA MWINGINE ANAITWA MSANGI NA RAJABU .
  CHIEF PRIDE

  - NYUMA YA HOTELI HII KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA FREDY , HUYU NDIO WATU WENGI WANAMPELEKEA LAPTOP KWA AJILI YA KUBADILISHWA BAADHI YA VITU NA KURUDISHWA SOKONI , KAMA HARDDRIVE NA RAM HATA KUFUTA NA KUINSTALL VITU UPYA MARA NYINGI AMEWAHI KUTIWA HATIANI NA ASKARI LAKINI KESHO YAKE AU BAADA YA MASAA FULANI YUKO MITAANI ANADUNDA .

  NJE YA JIJI

  - MOROCCO ( KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA ZABRON ) HUYU NI MTOTO WA MWALIMU MSTAAFU WA CHUO KIKUU CHA DSM LAKINI SASA NI MAREHEMU , AMEWAHI KUWA SEHEMU YA KUKODISHA VIDEO NA KUTENGENEZA VIDEO SEHEMU ZA UPANGA , YEYE NI MNENE MREFU ANAISHI MAKONGO JUU HAJAWAHI KUSOMEA MASUALA YA ICT WALA MAWASILIANO .

  - KIJITONYAMA MABATILI ( JAMES CID ) HUYU NI ASKARI KANZU HUWA ANAENDESHA GARI AINA YA MARINO YEYE ANAJIFANYA MSUKUMA ILA NI MWENYEJI WA MBEYA , MARA NYINGI ANAPENDA KUTEMBELEA MOROGORO INAHISIWA NDUGU ZAKE WENGI WANAISHI MOROGORO ( LAPTOP NYINGI AMBAZO ANAZISHIKA KWA WATU AU KATIKA MATUKIO MBALI MBALI HUWA ANAZIHIFADHI KATIKA NYUMBA MOJA YA WAGENI AMBAYO IKO KARIBU NA KITUO CHA POLISI MABATINI HUYU PIA HAJUI CHOCHOTE KUHUSU ICT WALA KUWASHA KOMPUTER WEZI WOTE WA LAPTOP SEHEMU ZA KIJITONYAMA MAKUMBUSHO NA MWENGE WANAMJUA HUYU HUWA ANAWASAIDIA SANA KATIKA MAMBO YAO POLISI .

  - LUFUNGIRA ( SAM NUJOMA ROAD ) HAPA KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA AMBROSY YEYE ANAISHI CHUO KIKUU ENEO LA ARDHI ANAJULIKANA KWA KUTOA LAPTOP NA SIMU TOKA KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU NA YEYE KUZIUZA SEHEMU ZINGINE .

  CELTEL - KIJITONYAMA
  HAPA KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA IBRA , NI MTU WA UMRI WA MIAKA KAMA 30 AU 35 , KABILA LAKE NI MJITA , ANA UNDUGU NA MMOJA WA MAASKARI PALE KITUO CHA POLISI OBEY NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM , LAPTOP NYINGI ZINAZOIBIWA KATIKA STORES ZA KAMPUNI YA CELTEL HUYU NDIO MHUSIKA MKUU ANAJUA MENGI , INAONYESHA SIO MFANYAKAZI RASMI WA CELTEL MANAKE HAVAAGI KITAMBULISHO ILI KUWEZA KUJUA NAMBA YA KITAMBULISHO CHAKE
  AFRICARE – ADA ESTATE

  KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA TOM , HUYU NI NDUGU YAKE IBRA ANAYEFANYA KAZI CELTEL NA NDIYE ANAYELETEWA HIZI LAPTOP KWA AJILI YA KUTAFUTA WATEJA , RAFIKI YAKE MKUBWA ANAITWA JOHN AMBAYE NI DEREVA WA ANOLD KILEO MWENYEKITI WA CTI .

  WEZI HAWA WOTE HUIBA LAPTOP NDANI YA MAGARI AU KATIKA MAOFISI NA NYINGI ZAO HUWA ZIKO BILA POWER ADAPTOR , BADO NAENDELEA KUTAFUTA WENGINE NA KUFANIKIWA KUJUANA NAO ILI KULETA HABARI ZAIDI .

  PAMOJA NA HAYO SIWEZI KUKUHAKIKISHIA UPATIKANAJI WA KIFAA AU VITU VYAKO HII NI KWA AJILI YA KUPEANA TAARIFA TU SINTOHUSIKA NA UTAFUTAJI WA VIFAA VYAKO KAMA VIMEPOTEA AU KUIBIWA KATIKA MAENEO YALIYOTAJWA HAPO JUU .
   
  Last edited: Aug 1, 2008
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Shy,
  Thanks kwa kutujuza hayo mkuu nilikuwa na plan ya kununua laptop nadhani nahitaji kuwa makini zaidi...
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Go on Shy!!!
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Aug 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Karibu Na Uwe Makini Usije Ukafuatwa Offisini Kwako
   
 5. m

  mzeewadriver Member

  #5
  Aug 1, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ahsante sana Shy ujumbe umefika, wahusika waufanyie kazi. Tusipende kununua vitu vya kuruka jamani.
   
 6. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaa wanaliza watu hata makanisani, ukipaki gari laptop ndani, make sure unaingia misa karibia kwisha tena jicho moja kwa mchungaji moja kwa gari!!!!!
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,595
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wanavunja kioo kidogoo(jiwe lililowekwa kwenye kitambaa) cha mlango wa nyuma kwenye magari madogo(saloon),then wanafungua mlango na kuchukua laptop wanatokomea...wengine hata wanathubutu kuiba laptop nje ya Hotel ya Movenpick....uki park gari yako uwe makini sana Jijini dar/na hata mikoani...vijana wanataka short cut faster....kwa kweli mtandao wao unazidi kukua siku hadi siku.....sijui itakuwaje...
   
 8. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kweli siku hizi kuna mtandao wa wezi sio wa laptop tu hata wa vifaa vingine. Hivi karibuni kuna jamaa yangu aliibiwa gari zima pale Mlimani city, siku hizi wezi wamekua wengi.

  Pamoja na kuwa na utawala wa sheria kwamba watuhumiwa wanapokamatwa wanastahili kupata dhamana, hii imechangia kwa watu kuendelea kufanya vitendo vya wizi pale wanapoachiwa kwa dhamana pindi wanapopelekwa polisi.

  Kuna nchi kama vile Pakistani wao uvumilivu uliwashinda wakapitisha sheria kwamba mtu yoyote atakayekamatwa ameiba auwawe kwa kupigwa risasi kichwani, hii ilisaidia sana na kufanikiwa kuondokana na wezi.

  Mimi nimeshuhudia watu kila siku wanaibiwa Power Windows za magari yao, na wezi wanaendelea kudunda tu barabarani tena skuzi naskia kuna maduka kabisaa yanayouza Power Windows za wizi huko kariakoo.

  Mi nashauri ianzishwe opreshen maalum ya kukamata na kuwaua kabisa hawa wezi, wanarudisha nyuma maendeleo kweli. Hebu asssume mtu aibe Laptop yako, kinachouma sio thamani ya hio laptop but some information zinapotea moja kwa moja na unaweza usizipate tena.
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Shy Mungu Akubariki Na Akulinde !!!!!lazima Tuwe Makini Na Hao Jamaa Hiyo Comptronix Wanaiheshimu Sana Kwa Bei Rahisi Kumbe Ni Wezi Hivyo Oooooooo

  \tuwe Makini Jamani Na Tunaumba Bwana Kova Nenda Uklifwailie Lile Dubwasha Au Ukiri Kama Uko Pamoja Na Hao Mabwana Na Utuletee Taarifa Mzee
   
 10. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  THANKS shy kwa kuvunja ukimwa wiki 2 zilizopita tumeibiwa laptop ofisini
  Jamaa kachomoa kaacha begi na adapter hawa jamaa wanatisha
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Shy asante sana mkuu na pole kwa uchunguzi mzito kama huo.Kwa wale tuliosoma hapa umetufungua macho kwa Kiasi kikubwa.
  Ingekua vema kama watu wengine wanaofahamu Mitandao kama ya
  1.Wezi wa Magari
  2.Wezi wa viwanja na kadhalika wangetudondoshea hapa hii ingetusaidia sana.
   
 12. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shy hii ripoti nafikiri pia ingemfaa IGP Mwema, sasa hapo naona umesha wa alert wahusika!...Polisi wetu wangeongeza "useriousness kidogo tu" tungeona maajabu. Mitandao ya wezi ipo nje nje tu. Talking of Polisi jamii...
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Shy;

  this is the reason we read JF, always "spot on" - Kuna mwingine mweupe na athletic figure anaonekana upanga na Rose Garden

  Cheers na Mungu akuzidishie
   
 14. J

  Jobo JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa taairfa hii. Mwaka jana mwishoni nimeibiwa kwenye gari langu katika maeneo unayoyataja, nadhani hii lead inaweza kusaidia kuangusha baadhi ya mitandao hiyo
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Thanks shy kwa tahadhari, Ila mtandao huu kuumaliza ni vigumu sana ntaeleza kwa nini

  1. Umasikini unaolinyong'onyeza taifa letu ndio chanzo kikubwa sana, vijana hawana ajira maisha yanazidi kupanda, kila mtu anataka kuishi mjini

  2. Kutokana na ukata unaolikabili taifa hasa unaosababishwa na ufisadi, serikali inashindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara ya kukidhi mahitaji, polisi na mahakama kama sehemu ya waathirika hao, wanaamua kujiunga kwenye mitandao ya wizi ili kukidhi mahitaji yao.

  3. Utamaduni tulionao watanzania wa kupenda vitu rahisi, unatoa soko la uhakika kwa vibaka kuuza mali za wizi, hebu tuache kununua vitu vya wizi muone kama wizi utaendelea. Tatizo ni utamaduni tubadili utamaduni wa kununua vitu mitaani, lakini kutokana na point ya 2 je tutaweza?

  4. Wengi wetu tunapenda kuwasifu wizi hasa kama wale mafisadi kuwa ni wajanja, na hiyo hufanya kila mtu afikirie hivyo.

  5. Sheria zetu haziko wazi kuhusu kununua vitu vya wizi, japo kuna watu huko nyuma wamewahi kufungwa kwa kununua laptop za wizi lakini je ni wangapi katika siku za karibuni wameadhibiwa?

  6. Mtandao huu hauanzii mitaani tu, unaanzia IKULU, ambapo watu wanapora mali ya Taifa kwa ujanja hawachukuliwi hatua yoyote hata wakijulikana unashuka mpaka wizarani. idarani, mpaka mitaani. Kwa ujumla Taifa letu ni Taifa la wezi, nasema hivyo kwa sababu ni utamduni uliojengeka kwa kasi hivi karibuni.

  Ushauri

  Tuanze na mafisadi, tushuke mpaka mitaani kuvunja mitandao hii. hatuwezi kukata matawi wakati shina lipo yatachipua tena, tuanze na shida. Itapatikana hela ya maendeleo, tukuze uchumi, vijana wapate ajira hawatakuwa na mawazo ya kuiba. Nina hakika 90% ya sisi humu kama tusingekuwa na misingi ya kujipatia riziki tungekuwa sehemu ya mitandao hii.
  SAFARI BADO NI NDEFU,
   
 16. b

  baraka1 Member

  #16
  Aug 4, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Du Jamani, rafiki yangu kavunjiwa kiyoo hapo millenuim towers kama mwezi umeisha hivi sasa na wakachukua laptop yake yaani aliingia benk amerudi only after 4 minutes akakuta wemeishamchukulia. Itabidi tumtafute huyo mwana-mtanadao wa hapo celtel atakuwa ndie aliichukua!!!
   
 17. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ninashukuru kwa ushauri wako. Tulionalaptop tunaogopa kwenda nazo ofisini. Tatizo ni kuogopa kukabwa na kuibiwa. Kwa uliyosema tutakuwa makini zaid. Mungu akubariki kwa ushauri wako.
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Aug 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Namba moja katika mtandao huu DARSKENDO yeye anashikiliwa kituo cha polisi kati kule mjini na asubuhi hii ndio anafanyiwa mahojiano na askari --- mmoja wa askari wanaomlinda huyu darskendo anaitwa Issa sijajua bado huyu issa makao yake ni wapi hata yukoje yukoje
   
Loading...