Kumiliki laptop Bora kwa Sasa!

Dave official

Member
Jul 27, 2022
28
51
Habari na JF, now days kumekuwa na wingi wa laptop, hivyo kupelekea ongezeko la wauzaji wa vifaa hivyo hasa mtandaoni.

Waswahili wasema kwenye mengi Pana mengi, laptop zimekuwa very cheap kila Kona zinapewa promo kila social network.

Jambo la msingi, kipi Cha kuzingatia au ni mambo yapi ya kuzingatia wakati wa kununua laptop Bora kwa soko hili la Sasa Ili usilie kwa baadae.
 
Habari na JF, now days kumekuwa na wingi wa laptop, hivyo kupelekea ongezeko la wauzaji
Pamoja na laptop kuwa nyingi, mpaka sasa hakuna laptop zilizoripotiwa kuwa kanyanga.

Laptop mbovu zilitokea miaka ya 2010,2011,2012.. hapo, na nyingi zilizokuwa mbovu zilikuwa zinakuja zikiwa mpya kwenye box.

Baada ya watu kugundua na kuanza kununua used za UK,Us, etc sijasikia tena laptop feki. Kuwa nyingi mtaani ni sababu ya oyaoya bandarini.

Ila % kubwa ya laptop zinafaa, itategemea unataka kufanyia nini.., hayo mambo ya Coi7, sijui Generation ya ngapi ni mbwembwe tu za wabongo, na wengi hawajui hata maana yake wanafata mkumbo tu.
 
Hivyo vigezo ulivyotaja hapo ni muhimu sana mzee kwenye performance.

Sio mbwmbwe hizo.
Nitakwambia kwanini ni mbwembwe, kwanza watumiaji wengi wa laptop matumizi yao ni kama wanafunzi, kuangalia movie, internet, pdf MS word, Excel etc ambayo wala hayahitaji mambo mengi, wachache wenye kazi za graphics, autocad, games zinazohitaji mashine kubwa. Ila sasa, kila anayetafuta laptop ya kununua utasikia hiyo ni generation ya ngapi!?,kama unabisha waulize maana yake, wengi hata hawaelewi. Iwe Coi3,5,7, ... 1st, 2nd,... 8th generation, kwa matumizi ya walio wengi zote hizo zinawafaa tu. Ila ubishoo tu na mbwembwe za wabongo tu. Ni kama Xiaomi,Oppo,Infinix,Samsung, Nokia, Iphone X,12, 14 sijui ProMax, zote zinafaa tu, zinabakia mbwembwe za nyongeza kwa mtu binafsi kutegemea na kipato chake. Ila kwa matumizi ya kawaida ya Smartphone zote zinafaa sana tu.
 
Kwangu mi huwa nataka laptop yenye pafomansi kubwa Kwa ajili ya KAZI na pia ukaaji WA chaji.

Kwa kama nikitaka kununua laptop Kwa sasa nitaangalia CPU, Intel angalau 12700h au Ryzen 7 6800h Kwa upande WA AMD, Kwa Apple angalau Apple M1

Laptop iwe inasapoti angalau RAM ya DDR4 na ukubwa WA ram uwe GB 16 na kuendelea, pia ram frequency iwe kubwa kuanzia 3200

Storage iwe NVMe ya walau GB 512 na USB nataka iwe inasapoti angalau USB 3.0 pia kuwe na usb-c
 
Pamoja na laptop kuwa nyingi, mpaka sasa hakuna laptop zilizoripotiwa kuwa kanyanga.

Laptop mbovu zilitokea miaka ya 2010,2011,2012.. hapo, na nyingi zilizokuwa mbovu zilikuwa zinakuja zikiwa mpya kwenye box.

Baada ya watu kugundua na kuanza kununua used za UK,Us, etc sijasikia tena laptop feki. Kuwa nyingi mtaani ni sababu ya oyaoya bandarini.

Ila % kubwa ya laptop zinafaa, itategemea unataka kufanyia nini.., hayo mambo ya Coi7, sijui Generation ya ngapi ni mbwembwe tu za wabongo, na wengi hawajui hata maana yake wanafata mkumbo tu.
Unless kwako kazi ya laptop ni kuinstall VLC huwezi andika hii comment, umepotosha sana. Utanunua laptop ya Celeron umpe mtu afanye video editing? Utanunua core i3 gen ya kwanza utumie kwenye Autocad ama uchezee games?
 
Nitakwambia kwanini ni mbwembwe, kwanza watumiaji wengi wa laptop matumizi yao ni kama wanafunzi, kuangalia movie, internet, pdf MS word, Excel etc ambayo wala hayahitaji mambo mengi, wachache wenye kazi za graphics, autocad, games zinazohitaji mashine kubwa. Ila sasa, kila anayetafuta laptop ya kununua utasikia hiyo ni generation ya ngapi!?,kama unabisha waulize maana yake, wengi hata hawaelewi. Iwe Coi3,5,7, ... 1st, 2nd,... 8th generation, kwa matumizi ya walio wengi zote hizo zinawafaa tu. Ila ubishoo tu na mbwembwe za wabongo tu. Ni kama Xiaomi,Oppo,Infinix,Samsung, Nokia, Iphone X,12, 14 sijui ProMax, zote zinafaa tu, zinabakia mbwembwe za nyongeza kwa mtu binafsi kutegemea na kipato chake. Ila kwa matumizi ya kawaida ya Smartphone zote zinafaa sana tu.
Hata wanafunzi mkuu, kuna wanafunzi wa engineer, computer science, Ardhi, hesabu etc. Wote wa nahitaji computer nzuri kutokana na program zinazotumika shule. Si kila mwanafunzi anasomea political science ama public relation.

Windows za kisasa tu zinataka generation za karibuni.
 
Nadhani hapa unamaanisha Intel Core 2 Duo ambazo Intel hawazisapoti tena Kwa updates
inakutosha kabisa,processor 1.8GHZ disc ni optional
Kuliko kuwa na Intel core 2 ni nafuu kuwa na pc yenye intel i3 zinazoishia na herufi U mfano intel i3 8130u ambazo zina ulaji mdogo WA umeme na pafomansi nzuri kuliko core 2 huku ukiwa na uhakika WA updates, wakati core 2 zinakula umeme mwingi na utendaji mdogo bila kujali Aina ya kazi
 
Unless kwako kazi ya laptop ni kuinstall VLC huwezi andika hii comment, umepotosha sana. Utanunua laptop ya Celeron umpe mtu afanye video editing? Utanunua core i3 gen ya kwanza utumie kwenye Autocad ama uchezee games?
Kuna jamaa ana laki 5. Ipi laptop inamfaa. Yuko chuo.
 
RAM ni muhimu sana usinunue chini ya 4, CPU ni muhimu sana usinunue chini ya i5 Kwa intel kama unataka speed na processing power kubwa, Kwa Storage please please nunua yenye SSD usinunue HDD inasaidia sana na speed wakati unapohamisha big files, mengine kama batter,operating system,graphic cards etc ni juu yako na unataka kuitumia vipi laptop yako, muhimu ni RAM,CPU na storage( make sure ni SSD)
 
Back
Top Bottom