Mzee wa Shughuli,
JK alipokuwa njiani kwenda Havana alipitia Spain na alikwenda Santiago Bernabeu, ule uwanja maarufu wa Real Madrid, na alikabidhiwa jezi yenye jina lake. Makamu wa rais wa Real Madrid akamwambia kuwa timu yake itatembelea Tanzania kama si mwaka huu, basi mwakani.
Suala la JK kutembelea Real Madrid unaweza ukalichambua kwa mitazamo mbalimbali. Wengine walisema anatafuta "popularity", wengine wakasema inasaidia kuitangaza Tanzania katika soka, na pengine kama Real watakuja Tanzania bila shaka watatembelea vivutio vyetu vya utalii, hivyo kusaidia kukuza sekta hiyo nchini. Unaweza kuhusisha ziara hiyo na "Mtandao wa Kikwete" pia, ambayo ndiyo mada tuliyonayo, kwamba mtandao wake ni mpana ndani na nje ya nchi, ukiwa pia katika maeneo kama kandanda. We' unaonaje?