Mtaje Mwalimu aliyekusaidia na Hutomsahau

Mtaje Mwalimu aliyekusaidia na Hutomsahau

Wakuu, ninaamini kila mtu amewahi kuhudhuria shule kwa njia moja au nyingine na kila mtu hapa amefundishwa na Mwalimu katika ngazi mbalimbali...kuanzia msingi, Sekondari mpaka Chuo.

Ni mwalimu yupi alikuwa msaada sana kwako hadi umefika hapo ulipo?

Mtaje na ni vyema ukasema na shule aliyokufundisha.
Sitamsahau Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, yaan mpaka leo hotuba zake zinaishi ndani yangu! Natamani nipate hotuba zake zote zilizorekodiwa ili kila wakati niwe nasikiliza! Kwa kweli, alikuwa, amekuwa na atakuwa msaada mkubwa sana katika safari yangu ya maisha ya uongozi!
 
Namkumbuka sana mwl munis huyu mwalimu bhna alikuwa akiingia anataka asalimiwe kwa table ya 2-12..unaanza kuimba weeee mpka inaisha.yapata miaka zaidi ya kumi na mbili sasa hizo hesabu zake za table hazijawahi kunitoka hata kwa bahati mbaya..[emoji16][emoji16]huwa namkumbuka hadi nguo alizokuwa anapendelea kuzivaa,style anayoingia nayo,angle aliyokuwa anapendelea kukaa,aina fimbo aliyokuwa anatuchapia tukikosea.hahaha its very funny aisee.nakukumbuka mwl wangu n u know that.miaka mingi nakuombea.kama utausoma huu ujumbe..nakukumbusha tena mwl lzima nitarudi kusema asante kwa mara nyingine nakuahidi na namuomba Mungu anisaidie.ulinijengea msingi mzuri mno wa hesabu tangu darsa lanne na wew ndo uliyenifanya mimi kuipenda hesabu.ninashuku sana ninaipenda hesabu na yenyewe inanipenda mpka sasa.shukran mwl Munis
 
Ngoja niwafungue macho kidogo

Nyuzi kama hizi sio nzuri kuchangia hasa kwa wale wasiopenda kujulikana

Mfano mtu atanzisha uzi akitaka utaje shule yako ya msingi na mwalimu uliyekuwa haumpendi au unampenda na wewe bila hiyana unataja

Kesho atakuja shule uliyosoma sekondari na walimu uliowapenda na usiowapenda na wewe tena unafunguka na unaenda mbali zaidi kwa kutaja majina ya rafiki zako ambao walikuwa kampani yako.

Sasa kimbembe kinakuja ukiwa unatafutwa hawatapata shida kukupata kwa kuwa watakuwa washajua wanaanzia wapi kwa kuwa ushawaambia uliposoma shule ya msingi na mwaka uliohitimu na kujiunga shule ya sekondari ubaya zaidi unakuja pale inapotokea hiyo shule ya sekondari uliyoitaja ulichaguliwa peke yako hivyo basi moja kwa moja utakuwa ushajitia kitanzi

So ushauri wangu kwa nyie msiotaka kujulikana nyuzi kama hizi ni za kukaa nazo mbali na usitoe informations zako za kweli kwa 100% utakuja juta huko mbeleni
 
dah me sitamsahau mwalimu Mrs Makundi, alikuwa mwelewa sana na mpole pia...ticha wa sayansi huyu Mkoani Pr. school-kibaha.
ukarimu na upendo wake huyu ticha ulinifanya had nianze kujikuta naipenda sayans, nampenda yeye na kumzmia...japo nilikuwa nunda boy enz hizo!
 
Ngoja niwafungue macho kidogo

Nyuzi kama hizi sio nzuri kuchangia hasa kwa wale wasiopenda kujulikana

Mfano mtu atanzisha uzi akitaka utaje shule yako ya msingi na mwalimu uliyekuwa haumpendi au unampenda na wewe bila hiyana unataja

Kesho atakuja shule uliyosoma sekondari na walimu uliowapenda na usiowapenda na wewe tena unafunguka na unaenda mbali zaidi kwa kutaja majina ya rafiki zako ambao walikuwa kampani yako.

Sasa kimbembe kinakuja ukiwa unatafutwa hawatapata shida kukupata kwa kuwa watakuwa washajua wanaanzia wapi kwa kuwa ushawaambia uliposoma shule ya msingi na mwaka uliohitimu na kujiunga shule ya sekondari ubaya zaidi unakuja pale inapotokea hiyo shule ya sekondari uliyoitaja ulichaguliwa peke yako hivyo basi moja kwa moja utakuwa ushajitia kitanzi

So ushauri wangu kwa nyie msiotaka kujulikana nyuzi kama hizi ni za kukaa nazo mbali na usitoe informations zako za kweli kwa 100% utakuja juta huko mbeleni
Mbona hata hapa wakiamua wanakupata? Dunia ilipofika sasa hakuna siri ni kuishi kwa haki tuuu.. We leo ungejua kama mtu fulani anatumia vyeti vya mtu mwingine kama wanavyo mtuhumu? Dunia ni kijiji kwa sasa
 
Mwlimu Hidden -maths
Moddy physics & Mgote -physics
Omar hakim & Mbuga - Biology
Unga & Mbuga - Chemistry

Walikuwa ni msaada mkubwa kwa wanafunzi na Bado wanaendelea kuwa msaada.
Wamenisaidia kwenda shule ya vipaji japo Sina kipaji maalumu,Ningetamani waendelee kutufundisha mpaka chuo sababu ya mazoea
NOTE:
bila kuongeza juhudi binafsi huwezi kufanikiwa.
mchikichi down!
 
Wakuu, ninaamini kila mtu amewahi kuhudhuria shule kwa njia moja au nyingine na kila mtu hapa amefundishwa na Mwalimu katika ngazi mbalimbali...kuanzia msingi, Sekondari mpaka Chuo.

Ni mwalimu yupi alikuwa msaada sana kwako hadi umefika hapo ulipo?

Mtaje na ni vyema ukasema na shule aliyokufundisha.
mwl dasi lang1 jite
mwl cuthbert histry jite

[HASHTAG]#fundi[/HASHTAG] wa geography tz nzima Mtegetwa Mng'ala msimbazi centre!

[HASHTAG]#chuo[/HASHTAG] prof Mukundala, prof Nyirabu &Dr Bashiru Ally
 
Mr Douglas swimming teacher international school of Tanganyika...Nice dude!!
 
Mwalimu Sheshila Shekidau
Tanganyika Edu-Consult Center Enzi zile Sinza Mori
 
Back
Top Bottom