Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mkuu habari naomba unielekeze namna ya kutengeneza funza kama chakula cha kuku maana kuna sehemu nilipita nkaona huo utaalamu mkuu
Kesho nitaleta somo kuhusiana na utengenezaji wa slikworm na faida zake kuwa mvumilivu mkuu
 
Mkuu habari, bata wangu anakula mayai yake. Alitaga mayai kumi na tatu kila siku anakula moja moja hili tatizo naweza litibu vipi
Mkuu kwa tatizo lako kuku wako ana mapungufu ya madini ya ca/P hivyo basi ningeomba uongeze DCP katika chakula chao..... Na imani tatizo lako litakuwa solved

Goodluck mkuu
 
Habari yako mkuu.
Naomba kufahamu ni tatizo gani linapelekea mpk Vifaranga vyangu vinakuwa vinabakiwa na kinyesi makalioni(yanajishika mengi sio kawaida) na tiba yake ni nini?
Ningependa kujua unawapa chakula cha aina gani vifaranga wako mkuu
 
Habari dr, mbwa wangu wana viroboto tena vikubwa, nilitumia ile tunayoweka kwenye kuku haijawatibu, je nitumie dawa gani kali iue hivyo viroboto? Huwa nawaogeshea na tiktik
 
Sipo Dar Mkuu natamani ungekuwa Dr wa papi Wangu, japo ungenijibu humu pia ingekuwa faida kwa wana Jamii Forum. Kwa sasa nawapa maziwa ya Ngombe na Supu.
Ndio ratiba zao hizo kesho nitatoa maelezo kwa kina kuwa na amani
Screenshot_20180302-125336_1.jpg
Screenshot_20180302-125324_1.jpg
 
Habari dr, mbwa wangu wana viroboto tena vikubwa, nilitumia ile tunayoweka kwenye kuku haijawatibu, je nitumie dawa gani kali iue hivyo viroboto? Huwa nawaogeshea na tiktik
Tumia amitraz mkuu itawaondoa wote...
 
Wape uji uliotengenezwa na unga wa mahindi ulichanganywa na maziwa iko vizuri sana mkuu
Mlo Mara ngapi maana hats USIKU naamka! Kwa kifupi napenda sana mbwa,hawa niliwakuta Sokoni wamezaaliwa na mama yao wasamaria wema wakasema hajaonekana siku mbili ikabidi waniuzie Mwenye banda walipo zaliwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom