Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu | Page 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by theriogenology, Aug 31, 2017.

 1. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2017
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Habari Wakuu....
  Nipo mbele yenu kujibu maswali yenu mbalimbali kuhusiana na tiba na ushauri wa magonjwa yanayosumbumbua mifugo yetu mbalimbali na hivyo kupelekea uzalishaji kupungua....

  Na pia kwa wale wakazi wa Dar es salaam na viunga vyake wanaohitaji huduma za ki veterinarian natoa huduma za chanjo na kutibu kwa wanyama wote wa nyumbani kama vile ;
  • Pets (Dog and cat)
  • Cattle (Ng'ombe)
  • Shoats (Mbuzi na Kondoo)
  • Fresh water fish (samaki)
  • Poultry (Kuku)
  • Rabbit (Sungura)
  Pia nafanya surgical operation kwa pets (mbwa na paka) kama vile castration and ovariohysterectomy (kufunga vizazi kwa madume na majike) and many other surgical operation kwa mifugo ya nyumbani tu.....

  Updates.....

  Vaccination schedules for Chicken......

  Siku ya kwanza : Chanjo dhidi ya Marek's na chanjo hii huchanjwa nyuma ya shingo chini ya ngozi but mara nyingi chanjo hii huchanjwa kiwandani (Hatchery)

  Siku ya Kumi: Chanjo dhidi ya Gumboro (1st dose) hii huchanganywa na maji

  Siku ya kumi na nane: Chanjo dhidi ya Gumboro (2nd dose) hii huchanganywa na maji

  Wiki ya tatu: Chanjo dhidi ya Newcastle (1st dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho

  Wiki ya sita: Chanjo dhidi ya Ndui Hii huchanjwa kwenye bawa (Inahitaji mtaalamu)

  Wiki ya nane: Chanjo dhidi ya Newcastle (2nd dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho

  Wiki ya kumi na nane: Chanjo dhidi ya Newcastle (3rd dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho (Baada ya Hii chanjo ya tatu unashauriwa kuchanja kuku wako kila baada ya miezi 3)

  Wiki ya kumi na tisa: Wape kuku wako dawa ya Minyoo, Mara nyingi hupewa kwenye maji (Baada ya Hii chanjo ya tatu unashauriwa kuchanja kuku wako kila baada ya miezi 3)

  ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

  MAELEZO MUHIMU KUHUSIANA NA LISHE KWA MBWA NA NAMNA YA KUANDAA CHAKULA CHA MBWA

  ★ Utangulizi

  Lishe/chakula/mlo kamili kwa mbwa ni muhimu sana kwani humpa mbwa afya nzuri na pia huwakinga mbwa na mashambulizi mbalimbali ya magonjwa na hivyo kuwafanya wavutie muda wote

  Kwa sasa vyakula vingi vya mbwa hupatikana madukani kutoka viwandani maana vimefanyiwa utafiti na kuzingatia afya ya mlaji ambaye ni mbwa na wanasayansi wameenda mbali zaidi wameweza kutengeneza chakula kutegemea aina ya breed ya mbwa

  Lakini hayo yote hayakuzuii wewe mmliki wa mbwa kujitengenezea chakula mwenyewe ambacho kitakuwa kimekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa mbwa ili kuepuka gharama ya chakula kwa namna moja ama nyingine kama nitakavyoelezea hapa chini

  ★ Umuhimu wa maji kwa mbwa

  ✓ Vyakula vyote hata vile ambavyo hukaushwa na hewa maalamu kiwandani huwa na kiwango kidogo cha maji, ingawa mbwa anaweza jipatia maji kwa njia ya kunywa lakni kiwango kingine cha maji kinatokana na chakula

  ✓ Mbwa anaweza kukaa muda mwingi bila kula chakula ( Hunger tolerance) lakni hawezi kukaa muda mrefu bila kunywa maji kwa maana hiyo mbwa asipokula chakula hutumia mafuta na baadhi ya nyama za mwili kama mbadala wa kupata nishati ya nguvu lakni akipoteza moja ya kumi ya maji yake mwilini mbwa hupoteza maisha

  ✓ Bila maji ya kutosha mbwa hatoweza kumeng'enya chakula chake na hata kama akifanikiwa kwa hilo chakula hakitoweza kunyonywa vizuri katika mfumo wa chakula hivyo anahitaji maji muda wote na unywaji wa maji hutegemea na mazingira na wingi wa chakula

  ★ Sifa za mlo kamili wa mbwa

  ✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuwa na ladha na harufu ya kuvutia

  ✓ Chakula kikidhi kiwango cha nguvu (wanga) kinachohitajiwa na mbwa

  ✓ Chakula kiwe na kiwango cha protini cha kutosha kuwezesha ukuaji wa mbwa na kumkinga na magonjwa

  ✓ Chakula kiwe na kiwango cha madini na vitamini cha kutosha

  Zingatia: Mbwa ni jamii ya wanyama wanaokula nyama (carnivores) lakni tukija katika suala la mchanganyo wa chakula ulio kamili ni lazma uwe na protini, wanga, vitamini na madini na hata mbwa mwitu wanapowinda mbugani mara nyingi wanawinda jamii ya wanyama wanaokula majani na wakifajikisha kumuua hula kitu ukijumuisha matumbo ambayo huwa na majani yaliyomeng'enywa na mifupa yote hivyo kuwawezesha kupata madini na vitamini kwa njia hiyo hivyo basi kwa mbwa wanaofungiwa ndani ni lazma wapate mlo kamili kama nitakavyoelezea hapa chini

  ★ Vyakula vinavyotakiwa na mbwa na jinsi ya kuandaa vyakula hivyo

  a) Nyama

  Nyama ndio chanzo kikubwa cha protini kwa mbwa na katika mchanganyo inatakiwa kuwa zaidi ya 50%. Nyama hii yafaa ichemshwe kwanza ingawa mbwa wanapendelea nyama mbichi lakni kwa hili lazma ichemshwe na baada ya hapo ndio inatakiwa kuchanganywa na vyakula vingine

  Kama nyama ina mifupa ni vyema mifupa ikaondolewa hasahasa kama nyama ni ya mbuzi/kondoo au kuku maana mifupa yao huwa ni midogo na hivyo inaweza kuleta shida katika mfumo wa chakula wa mbwa baada ya kuondolewa mifupa inatakiwa kuchemshwa pekee hadi pale itakapotoa supu ambayo itatumiwa kuchanganywa na vyakula vingine

  b) Maziwa na Mayai

  Maziwa na mayai hutumiwa kama mbadala wa nyama pale nyama inapokosekana hapa unatakiwa kuchukua maziwa kiasi cha lita 1.8 yachemshe yaache yapoe kisha changaya na mayai mawili yaliochemshwa vizuri then malizia kwa kuchanganya na vyakula vingine

  c) Wali

  Wali hutumika kama chanzo cha wanga na mchele unaotakiwa hapa ni ule unpolished (mchele mchafu) maana huwa na virutubisho vingi zaidi tofouti na ule Polished (mchele safi) na unaadaliwa kwa kuchemsha na maji kutengeneza bokoboko ambalo huchanganywa na vyakula vingine

  d) Unga wa ngano

  Unga wa ngano hutumika kama mbadala wa mchele endapo utakosekana hapa unatakiwa kuuchanganya kutengeneza uji mzito ambao utatumiwa kuukaanga kutengeneza chapati au pancakes ambazo utazikatakata na kuchanganya na vyakula vingine

  e) Uji

  Uji pia hutumika kama mbadala wa mchele na uji unatakiwa hapa ni ule ambao umetengenezwa na unga wa mahindi ambao haujakobolewa unauacha upoe kisha changanya na vyakula vingine. Mbwa wanaupenda sana uji huu.

  f) Mbogamboga

  Ingawa mbwa hawapendi mbogamboga lakni ni muhimu kuwemo kwenye mchanganyo maana ndio chanzo cha vitamini na madini mbalimbali mboga kama sukumawiki, chinese ni nzuri lakni ukikosa hizo unaweza chemsha carrot au beetroots na ukachanganya kwenye vyakula vingine na ikumbukwe kuwa kiwango cha mboga kitengeneze 1% ya mchanganyo wote

  ★ Vitu vya kuzingatia katika ulishaji wa mbwa

  ✓ Kwa kawaida tumbo la mbwa ni kubwa kulinganisha na viungo vingine vya mfumo wa chakula hivyo anatakiwa kula ambacho kitaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu na kwa kawaida mbwa anayakiwa kula mara moja kwa siku ingawa watu wengine huwalisha mara mbili ambapo hutenga chakula kama chakula cha kawaida (light diet) au chakula cha kutosha (heavy diet)

  ✓ wali kidogo na mbogamboga huandaliwa kivyake baada ya hapo huchanganywa na supu na nyama kidogo na hii tunaita light diet na chakula kamili huwa na nyama,mbogamboga,wali au chapatti na vyote hivi huchanganywa na supu ya mifupa

  ✓ Na mbwa aina ya chakula kutegemea na majukumu yake yako muda gani ' Kama mbwa analinda usiku basi asubuhi anatakiwa kula heavy diet na jioni masaa machache kabla ya kuingia lindoni anatakiwa kula light diet na kama mbwa anaingia lindoni mchana basi jioni anatakiwa kula heavy diet na asubuhi kabla ya kuingia lindoni ale light diet

  ✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuandaliwa muda kidogo kabla ya mbwa kula na kama chakula kikibakizwa na mbwa hatakiwi kulazimishwa kula na chakula hicho kiondolewe ndani ya dakika 10-15

  ✓ Vyombo vya chakula na maji vinatakiwa kuwa safi na salama muda wote na hakikisha maji hayaishi ndani ya chombo cha maji na kinatakiwa kuwa karibu na bakuli la chakula muda wote

  ✓ Mbwa wasipewe vyakula vya sukari au chumvi maana vyakula hivyo huwapunguzia umri wa kuishi na pia huwasababishia magonjwa mbalimbali ya ngozi

  ✓ Muda na mahali pa kulia chakula uwe/pawe sehemu moja hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula kama ni asubuhi ya saa 11 na jioni ya saa2 iwe hivyo muda wote hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula

  ✓ Kwa siku mbwa anatakiwa kuwa gm 350 za chakula na mara moja unaruhusiwa kumpa mbwa maji yaliyochanganywa na glucose na iwe kila siku

  ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

  MAELEZO KUHUSU UGONJWA WA (PARVOVIRUS INFECTION) KWA MBWA

  ★ Utangulizi

  Ugonjwa huu huenezwa na virusi wanaoitwa parvovirus aina ya 2b, na ni miongoni magonjwa hatari sana kwa mbwa maana huambukiwa kutoka kwa mbwa mmoja kwenda mwingine na uligunduliwa miaka ya 1970's...

  Ugonjwa huu huwa na tabia ya kushambulia seli maalamu ambazo hupatikana katika mfumo wa chakula hivyo (GIT) na hivyo kumsababisha mbwa kuonesha dalili kama vile kuharisha au kutapika. Na kupitia kuharisha virusi hawa hutolewa kwa wingi mno kwa wiki kadhaa baada ya mnyama kuugua na hivyo kuongeza uwezekano wa mbwa mwingine kuugua ugonjwa huo.....

  Ugonjwa huu hushambulia mbwa wa umri wowote lakni kwa asilimia kubwa mbwa ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni wale wadogo wenye umri kati ya wiki 6-20 na jamii ya mbwa ambao hushambuliwa sana na ugonjwa huu ni Doberman pinscher na Rottweiler na hadi sasa haijajulikana kwanini kinga yao haiwasaidii sana wanapo shambuliwa na ugonjwa huu ( sio hao tu jamii nyingine pia hushambuliwa na ugonjwa huu mfano German shepherds, pit bull na Labrador retriever).....

  ★ Njia za uenezaji wa ugonjwa huu

  Ugonjwa huu huenezwa kwa njia kuu mbili nazo nitaziweka katika makundi mawili njia ya moja kwa moja (directly) na njia isiyo ya moja kwa moja (indirectly)

  a) Njia ya moja kwa moja (directly)

  Ugonjwa huu huenezwa moja kwa moja iwapo mbwa asiye mgonjwa atagusana (manyoya au miguu wakati wa kucheza) na mbwa ambaye ni mgonjwa na hivyo kupelekea yeye kuwa na ugonjwa huo

  b) Njia isiyo ya moja kwa moja (indirectly)

  ✓ Kama nilivyoelezea hapo mwanzo virusi hawa hutolewa kwa wingi kupitia kuharisha hivyo mbwa anaweza kupata ugonjwa huu baada ya kunusa au kula/kunywa chakula/maji ambayo yamechangamana na kinyesi hicho

  ✓ Pia mbwa anaweza kupata ugonjwa huu kupitia viatu, mara nyingi katika matembezi ya kawaida mmliki anaweza kukanyaga kinyesi cha mbwa mgonjwa na hivyo kubeba virusi hao nyumbani ambapo katika kuingia ndani ya banda anaweza sababisha mbwa kupata ugonjwa huu

  ★ Dalili za ugonjwa huu

  Baada ya mbwa kuambukizwa ugonjwa huu itamchukua siku kati ya 4-5 kuonesha dalili za ugonjwa huo nazo ni kama ifuatavyo;

  ✓ Siku za mwanzo mbwa atakuwa mnyonge na atapoteza hamu ya kula

  ✓ Mbwa atatapika na kuharisha ( mara nyingi maharisho haya huwa na mchanganyiko wa damu/kamasi au vyote kwa pamoja)

  ✓ Baadhi ya mbwa huwa na joto kali linalofika 41.1 °C na wengine huwa na joto la kawaida

  ✓ Wakati wa uchunguzi wa mnyama katika maeneo ya tumbo huonesha dalili za maumivu na mara nyingi hupindisha mgongo na kuwa kama upinde hii ni dalili ya kwamba anasikia maumivu maeneo ya tumbo

  ✓ Mbwa huishiwa maji na hivyo kufanya ngozi kuvutika kirahisi na mwisho wa siku mbwa hupoteza uzito maana huwa hawezi kula tena

  Kwa hapo mashambulizi ya moyo yalikuwa mengi kwa mbwa wagonjwa lakini kwa sasa njia hiyo ya mashambulizi kwa moyo imezuiwa na kufanikiwa baada ya chanjo zinazotolewa kwa mbwa jike mwenye mimba kati ya wiki 2-4 kabla ya kuzaa, Chanjo hii huongeza antibodies kwa mama ambazo mwisho wa siku hutumika kumlinda mtoto pindi anapozaliwa hivyo kuondoa mashambulizi ya virusi hawa kwa moyo wa mbwa wadogo (puppies)

  ★ Njia za kugundua ugonjwa huu

  Zifuatazo ni njia zinazokuwezesha mmliki wa mbwa kujua mbwa wako kapata shambulizi la parvovirus;

  ✓ Dalili ya kutapika na kuharisha kinyesi kilichochangamana na damu au kamasi au vyote kwa pamoja

  ✓ Njia mbalimbali za maabara kama vile ELISA na IFAT hii ni baada ya kuchukua damu ya mgonjwa kwa uchunguzi zaidi ingawa matokeo yanaweza kuwa negative/postive

  ★ HITIMISHO

  ✓ Kama mjuavyo magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tiba na ikumbukwe ugonjwa huu ni hatari sana hivyo ikitokea mbwa wako kaugua ni vyema kumjulisha Veterinarian kwa msaada na mbwa wako anaweza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa zaidi ya 80%

  ✓ Kumbuka kuwachanja mbwa wako kwa wakati kuepuka kumpoteza mbwa wako ingali bado unampenda (Siku zote chanjo ni bora zaidi kuliko tiba)

  ✓ Usiruhusu kuwachanganya mbwa wako wadogo na mbwa wakubwa hadi
  watakapo maliza ratiba za chanjo na inatakiwa wakae wiki mbili mbali na wakubwavbaada ya chanjo ya mwisho....

  ✓ Ratiba ya chanjo ni kama ifuatavyo wiki 6,9 na wiki 12 (Na kwanini kuanza na wiki sita hii ni kwa sababu wiki 2-4 za mwanzo mbwa huwa yuko chini ya ulinzi wa antibodies za mama hivyo ukiwachanja kwa wiki hizo za mwanzo ile chanjo itahisiwa kama shambulizi kwenye mwili wa mbwa mdogo hivyo kuliwa na hivyo inashauriwa kuanzia wiki ya 6 maana baada ya wiki 4 antibodies za mama huwa zinaanza kupungua kwenye mwili wa mbwa mdogo.

  ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

  Utahitaji vifuatavyo ili kuwa na duka la mifugo

  Site
  Mtaji

  VYETI VIFUATAVYO

  Daktari aliyesajiliwa cheti
  Chet cha msaidizi enroled or enlisted
  TIN
  TRA LESENI
  TFDA
  TPRA
  FIRE
  VCT for veterinary facility
  BRELA

  Kwa mahitaji ya cheti cha daktari aliesajiliwa tunaweza wasiliana.....

  Karibuni sana....
   
 2. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #281
  Mar 16, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Just twice a day mkuu
   
 3. NJUGHU

  NJUGHU JF-Expert Member

  #282
  Mar 16, 2018
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 357
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Asante sana kwa Leo kiongozi. USIKU mwema.
   
 4. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #283
  Mar 16, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Halafu dawa ya minyoo (ascarten P) unaanza wapa wanapofikisha wiki4 then 6 and 8 wiki ya kumi na mbili unawapa ivermectin na unarudia kila baada ya miezi 3
   
 5. Kuziwa

  Kuziwa JF-Expert Member

  #284
  Mar 17, 2018
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Asante sana mkuu! Umekua msaada sana tangu ulipoleta uzi huu! Je naweza kuwapa chanjo ya newcastle sambamba na hayo maelezo hapo juu? Au nimalize kwanza ESB3 then ndio niwachanje?
   
 6. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #285
  Mar 17, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Wape kwanza ESB3 then waachae kwa wiki moja then uwachanje mkuu....
   
 7. ABiClever Junior

  ABiClever Junior JF-Expert Member

  #286
  Mar 24, 2018
  Joined: Dec 14, 2016
  Messages: 874
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 80
  Aisee kuku wangu wanapooza miguu na kufa ndani ya siku moja je ni ugonjwa gan nawapa ile dawa nahic inaitwa t.o.c niliambiwa ni ant-biotic (cjui ndio hvy) lakin aikufanikiwa wanakufa daily.
   
 8. baiser

  baiser JF-Expert Member

  #287
  Mar 24, 2018
  Joined: Dec 29, 2014
  Messages: 720
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 180
  Dr uko vizur sana katika kutoa ushaur kwa wafugaji nakupongeźa kwa hilo majibu yako yanaonesha vet.uliisoma vizur na pia ujuzi wa mtaani umekusaidia sanaa kutatua changamoto mbalimbali za mifugo ilaa ningeomba unapowashaur wafugaji ni vyema ukawaambia watafute watàalamu wa mifugo ili wakajiridhishe kabla ya kununua dawa na kutibu in medicine kuna kauli wanasema telephone diagnosis is not always rewarding .
   
 9. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #288
  Mar 27, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Njoo PM Mkuu
   
 10. m

  marvinpm Member

  #289
  Apr 13, 2018
  Joined: Mar 11, 2018
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hello..... Karibuni Sana Katika group linalohusu ufugaji wa nguruwe

  Karibu Sana wewe mtaalamu wa mifugo, mfugaji, mnunuzi, pamoja na Wale wenye kiu ya kujifunza zaidi kuhusu ufugaji huu wenye tija na kipato cha uhakika.....

  Click link ifuatayo kujiunga......

  Zingatia kujitambulisha pindi tu uingiapo katika group hili
  ZINGATIA KUJITAMBULISHA PINDI TU UINGIAPO KATIKA GROUP HILI... JINA, MKOA, SHUGHULI

  TSA- PIG FARMING
   
 11. A

  Astej New Member

  #290
  Apr 21, 2018
  Joined: Apr 2, 2018
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  .m
   
 12. tpaul

  tpaul JF-Expert Member

  #291
  May 3, 2018
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 14,020
  Likes Received: 4,352
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakushukuru kwa kujitoa kwako kuwashauri wafugaji katika nchi hii. Huu ndio uzalendo wa kweli unaopaswa kuigwa na kila mtanzania mwenye mapenzi mema. Ubarikiwe sana.
   
 13. L

  Leompasa Member

  #292
  May 5, 2018
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 11
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Dr nataka kuanza Kufuga Kuku was nyama naomba ushaur Kuku aina gani ni wazuri na vifaranga vyake navipata WAP mm npo sumbawanga
   
 14. Jini Kisiranii

  Jini Kisiranii JF-Expert Member

  #293
  May 5, 2018
  Joined: Feb 20, 2018
  Messages: 1,158
  Likes Received: 994
  Trophy Points: 280
  Link haifungui Screenshot_20180505-171339.jpg
   
 15. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #294
  May 5, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Broiler aina ya cornish cross breed wako vizuri....

  Na vifaranga wazuri kachukue euro poultry hawa wako maeneo ya airport au mkuza chicks hawa wako ubungo hapo....
   
 16. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #295
  May 5, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana mkuu na karibu sana...
   
 17. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #296
  May 5, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
 18. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #297
  May 5, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Karibu mkuu....
   
 19. L

  Leompasa Member

  #298
  May 5, 2018
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 11
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Asante Dr maeneo ya mbeya hawana tawi mana usafir dar mpaka sumbawanga mbali
   
 20. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #299
  May 5, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,344
  Likes Received: 8,178
  Trophy Points: 280
  Kwa mbeya sijafahamu mkuu but na imani kutakuwa na kampuni moja wapo au kampuni nyingine zinazosambaza vifaranga kanda hiyo....
   
 21. L

  Leompasa Member

  #300
  May 5, 2018
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 11
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Nashukuru Dr ngoja nifanyie kazi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...