Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Samahan naomba kuuliza
Hivi korodoni zikiwa michubuko na zimesinyaa kila mda ni dalili za nn au ni ugonjwa gan na tiba yake ni ipi
 
Ninamtoto wangu anamiaka mitatatu aliugua degedege na kupona lakini sasahivi amekua akizimia kilabaada ya muda mfupi tatizo litakua nini
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako. Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.

Ugonwa wa Corona (COVID-19)

MPYA: Jinsi ya kujenga kinga ya mwili

Je papai inaweza kuwa na Corona?

Ugonjwa wa Kisukari

Chanjo ya Corona

Kuendelea kupata dondoo za Afya kwa kupitia video, Bofya Hapa: Subscribe

Naomba msaada: nina vipele vidogo sana visivyotoa maji maji wala haviwashi vipo mwisho wa kichwa cha uume. Je tatizo ni nini na tiba yake ni ipi
 
Attachments

  • 1607065604996771897326.jpg
    1607065604996771897326.jpg
    96.2 KB · Views: 9
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako. Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.

Ugonwa wa Corona (COVID-19)

MPYA: Jinsi ya kujenga kinga ya mwili

Je papai inaweza kuwa na Corona?

Ugonjwa wa Kisukari

Chanjo ya Corona

Kuendelea kupata dondoo za Afya kwa kupitia video, Bofya Hapa: Subscribe

oky tatizo la vipele vidogo vidogo kwenye kichwa cha chini ch uume
 
Naomba msaada: nina vipele vidogo sana visivyotoa maji maji wala haviwashi vipo mwisho wa kichwa cha uume. Je tatizo ni nini na tiba yake ni ipi

Picha haioneshi vizuri ila kama haviwashi wala kutoa maji vinaweza kua vipele vya kawaida tu either kutokana na joto au kubadili mazingira
 
Wakuu msaada wenu please nina vipele kwenye kisogo Ni tatizo la muda mrefu Sana toka 2004 mpk leo nimetumia Sana za hospital na miti shamba pia sijapata nafuu wakati mwingine zinawa na zinauma mwenye kujia tiba please
 
Naomba msaada: nina vipele vidogo sana visivyotoa maji maji wala haviwashi vipo mwisho wa kichwa cha uume. Je tatizo ni nini na tiba yake ni ipi
Mkuu huo sio ugonjwa, ni maumbile, kila mwanaume anavyo, vipo kwa ajili ya kumkuna mwanamke na hutokeza immediately baada ya kubalehe
 
Bwana DR. mimi nina maswali yafuatayo:
1.Je kula vyakula vyenye asili ya sukari kama vile miwa/juice ya miwa/pipi/ ndizi sukari/soda/Chai n.k huchangia kupata ugonjwa wa kisukari?
2.Ndugu yangu anatoa harufu mbaya kinywani pamoja na kuwa anapiga mswaki kila siku kabla na baada ya kuamka, je huu ni ugonjwa au tatizo gani? Nini tiba yake?
3.Nilishauriwa kunywa maji mengi ili kuepuka magonjwa kama vile mawe kujaa kwenye figo, lakini kila ninapojitosa kunywa maji ya kutosha najikuta nafrequent toilet! Nimejaribu kupima kisuksri lakini naambiwa sukari ipo normal, Je tatitzo ni nini?
4.Katika miaka ya karibuni kumeibuka maduka mengi ya dawa za aili kalibu za kila aina, Je ni dawa zipi zilzo borz kwz matumizi kati ya dawa za asili na za viwandani?

Thanks!
 
Nina mdogo wangu kamfanyia tohara mwanae wa miaka sita toka siku ya jumanne trh 26 ila mpaka leo mtoto kavimba korodani..alimpigia simu dkt alikuja nyumbani ila baada ya kumchunguza akasema haina shida ..je dkt yupo sahihi au tutafute suruhisho
 
Kula sukari hakusababishi Kisukarii hata siku mojaaaa mkuuu kisukari husababishwa na mambo mengine kabisa.

Unapokula chakula usiku na kulala bhasi wale bacteria waliopo mdomoni hushambulia yale mabaki ya chakula hasa mabaki ya vyakula vyenye sukari na hii hupelekea kuzalisha Acid na chemical zingine zinazotoa Harufu mbaya wakati mwingine husababisha hata meno kuharibika.. kuepuka harufu hii mbaya piga mswaki kila baada ya kumaliza kula.

Unapokunywa Maji mengi kweli husaidia sana kusafisha figo lakini unapaswa ujue mwili huwa hautunzi maji ya ziada so yakizidi lazima yatolewe ndio maana Ukinywa maji mengi lazima ukojoe sana kama sehemu za baridi na kama sehemu za joto kama dar utasweat sana na pia sio tatizo kabisa pia ni Afyaa.

Dawa za viwandani zina ubora zaidi sababu zimefanyiwa majaribio juu ya magonjwa zinazotibu na Kuonesha uboraa zaidi pia na usalama kwa mtimiaji. Mitishamba mingi kweli ni mimea ya asili lakini ubora wake bado ni changamoto japo inawezekana ni salama. Japo hata dawa za viwandani nyingi hutokana na chemical za Mimea.
 
Nina mdogo wangu kamfanyia tohara mwanae wa miaka sita toka siku ya jumanne trh 26 ila mpaka leo mtoto kavimba korodani..alimpigia simu dkt alikuja nyumbani ila baada ya kumchunguza akasema haina shida ..je dkt yupo sahihi au tutafute suruhisho
Tohara haiwezi sababisha korodani zivimbe kama uvimbe haupungui bhasi kuna tatizo dawa za maumivu pekee hazitoshi mrudishe mtoto hospital.
 
Wakuu msaada wenu please nina vipele kwenye kisogo Ni tatizo la muda mrefu Sana toka 2004 mpk leo nimetumia Sana za hospital na miti shamba pia sijapata nafuu wakati mwingine zinawa na zinauma mwenye kujia tiba please
Tafuta dawa inaitwa SKYDERM hii ni kibokooo...!! Pole sana
 
Ninamtoto wangu anamiaka mitatatu aliugua degedege na kupona lakini sasahivi amekua akizimia kilabaada ya muda mfupi tatizo litakua nini
Hakuponaa Huyo mtoto ila alipata naafuu...!! So inapotokea mazingira au hali inayochochea degedege kurudi bhasi inarudi. Vitu kama Homa..stress. Mpeleke mtoto hospital wakaangalie kama ana physical damage yoyote kwenye Ubongo kama sio kubwa bhasi anatibika utapewa dawa. Pole sana usipuuzie hali itazidi kuwa mbaya mbele ya safari.
 
Samahan naomba kuuliza
Hivi korodoni zikiwa michubuko na zimesinyaa kila mda ni dalili za nn au ni ugonjwa gan na tiba yake ni ipi
Mchubuko ni dalili ya Fungus... tafuta cream inaitwa Terbinafine cream alafu kila ukiogaa hakikisha Unajikaushaa vizuriii kabisa. Na uwe unabadilisha boxer mzee sio siku tatu upo nayoo tuu
 
Back
Top Bottom